ASEAN kufanya mikutano kuhusu Myanmar
23 Mei 2025Haya yamesemwa na katibu mkuu wa Jumuiya hiyo ya ASEAN Kao Kim Hourn.
Kim Hourn hakuweka wazi masuala yatakayojadiliwa kwenye mikutano hiyo au ikiwa kuna mapendekezo mapya yatakayotolewa. Hourn amedokeza tu kwamba mkutano huu utajihusisha na
Pendekezo la amani la ASEAN mwaka huo, lililokuwa na vipengee vitano vinavyotoa wito wa kumalizika kwa vita na pia kufanyika mazungumzo katika ya makundi pinzani. Lakini hilo hadi sasa halijapiga hatua yoyote hali iliyopelekea majenerali wa Myanmar kutoalikwa katika mikutano ya Jumuiya hiyo.
Jumuiya hiyo ya ASEAN yenye idadi ya wanachama 10, imekuwa ikitoa wito wa kusitishwa mapigano kati ya waasi na wanajeshi wanaoitawala Myanmar, ambayo yamesababisha karibu watu milioni 3.5 kuachwa bila makazi, tangu jeshi lilipomuondoa madarakani rais aliyechaguliwa Aung San Suu Kyi mwaka 2021.
Utawala wa kijeshi Myanmar wadaiwa kuwatesa raia wake
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya ASEAN Kao Kim Hourn amesema mkutano wa kwanza wa jumuiya hiyo utajumuisha nchi zilizochukua uwenyekiti mwaka uliopita uliopo na ujao, ambazo ni Malaysia Laos na Ufilipino huku mkutano wao wa pili ukiwajumuisha mawaziri wa mambo ya nchi za nje.
Awali Myanmar ilikjulikana kama soko kubwa la kiuchumi kutokana na mageuzi ya kiuchumi na demokrasia iliyokuwepo, lakini mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika mwaka 2021 yaliitumbukiza nchi hiyo katika mgogoro mkubwa wa kisiasa huku serikali ikingangana kuongoza huku ikikabiliana na vikwazo vikubwa kutoka kwa waasi wa kikabila na vuguvugu la watu wanaodai demokrasia.
Jeshi la Myanmar limekuwa likidaiwa kutekeleza mateso makubwa kwa raia wake ikiwemo mashambulizi ya angani hasa katika makazi ya watu, madai ambayo limelikanusha vikali na kudai ni propaganda ya mataifa ya Magharibi.
afp/ap