MigogoroAfrika
Asasi: RSF imewaua watu 48 katikati mwa Sudan
15 Julai 2025Matangazo
Hayo yameelezwa jana Jumatatu na asasi ya wanasheria wanaofuatilia vitendo vya kihalifu vinavyofanywa na pande hasimu kwenye mzozo huo wa miaka miwili kati ya kundi la RSF na jeshi la taifa.
Taarifa ya asasi hiyo imesema raia hao 48 waliuawa siku ya Jumapili pale wapiganaji wa RSF walipokivakia kijiji cha Um Garfa kilichopo kwenye mkoa wa Kordofan Kaskazini, wakachoma moto nyumba na kupora mali.
Tukio hilo ni miongoni mwa mengi yaliyofanywa na kundi la RSF tangu Jumamosi iliyopita na asasi hiyo inakadiria zaidi ya watu 300 tayari wameuawa.
Kwenye kijiji kingine cha Shag Alnom karibu na mji uitwao Bara, zaidi ya watu 200 waliuawa kwa kuchomwa moto au kupigwa risasi siku ya Jumamosi.