Asasi: Mapigano Syria yasababisha vifo vya watu 70
7 Machi 2025Taarifa hizo zimetolewa na asasi ya kiraia inayofuatilia hali ya haki za binadamu nchini Syria.
Asasi hiyo imesema makabiliano hayo kwenye mji wa mwambao wa Jableh na vijiji jirani ndiyo "makali zaidi kushuhudiwa nia utawala mpya wa Syria tangu Assad" alipoangushwa Disemba mwaka jana.
Mji huo unapatikana kwenye jimbo la pwani ya bahari ya Mediterrania la Latakia, eneo ambalo ndiyo kitovu cha jamii ya wachache ya Assad ya Alawite waliokuwa nguzo ya utawala wake.Afisa mmoja wa usalama amesema "shambulizi lililopangwa kwa ustadi kutoka wafuasi wa Assad lilivilenga vitu vya upekuzi na maafisa waliokuwa kwenye doria ya mji wa Jableh.
Taarifa zinasema wapiganaji wanaomuunga mkono Assad wamewaua maafisa usalama 28 wa utawala mpya wa Syria huku wenyewe wakipoteza pia makumi ya wapiganaji. Raia pia 4 wanne wameuua kwenye machafuko hayo.