Armenia yamkatama waziri mkuu wa zamani kwa ufisadi
13 Juni 2025Hiki ni kisa kingine katika hatua za kupambana na ufisadi za kiongozi wa nchi hiyo mwanamageuzi Nikol Pashinyan.
Pashinyan aliyeingia madarakani baada ya mapinduzi ya amani ya mwaka 2018 yaliyowaondoa viongozi wa Armenia wa baada ya utawala wa Kisovieti, ameapa kuangamiza ufisadi katika taifa hilo lisilo na bahari.
Ijumaa, kamati ya ufisadi ya Armenia ilitangaza kukamatwa kwa Abrahamyan kwa madai ya kadhaa ya utakatishaji fedha, matumizi mabaya ya mamlaka na kuhusika kinyume cha sheria katika vitendo vya kibiashara ambavyo havijaidhinishwa.
Maarufu kwa jina la utani Muk - ambalo kwa Kiarmenia linamaanisha "panya" - Abrahamyan alihudumu kama waziri mkuu wa nchi hiyo kuanzia mwaka 2014 hadi mwaka 2016 na kama spika wa bunge kutoka mwaka 2008 hadi 2011.
Kisa hiki ndicho cha hivi karibuni katika msururu wa kesi walizofunguliwa maafisa wa zamani katika serikali ya Pashinyan, wakiwemo marais wa zamani Serzh Sarkisian na Robert Kocharyan.
Wachambuzi wanasema, kiwango cha ufisadi kilichowekwa wazi tangu kuingia mamlakani kwa Pashinyan imekuwa ni pigo kwa chama tawala cha Republican cha zamani ambacho kwa sasa ndicho chama cha upinzani.
Abrahamyan mwenye umri wa miaka 67 anaripotiwa kuwahi kumiliki biashara nyingi ikiwemo migodi ya mchanga, mashamba ya zabibu. vituo vya mafuta, casino na nyumba ya mapumziko ya msimu wa joto huko Crimea.