Araghchi: Iran haitawachana na urutubishaji madini ya urani
22 Julai 2025Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema Iran haiwezi kuwachana na mpango wake wa kurutubisha madini ya urani hata kama uliharibiwa vibaya wakati wa vita vya hivi majuzi vya Israel na Iran ambapo Marekani ilivishambulia kwa mabomu vinu vya nyuklia vya Iran.
Akizungumza Jumatatu na shirika la habari la Marekani Fox News Araghchi amesema mpango huo umesimamishwa kwa sababu uharibifu ni mkubwa na mbaya sana, lakini ni wazi hawawezi kukata tamaa na kuwachana na mpango huo kwa kuwa ni mafanikio ya wanasayansi wao wenyewe, na ni suala la fahari ya taifa.
Aragchi ameyasema hayo wakati Iran ikifanya mazungumzo leo na Urusi na China kuhusu mpangow ak wa nyuklia mjini Tehran.