APR yashindwa kutamba katika mashindano ya BAL
16 Juni 2025Al Ahly Tripoli kwa mara ya kwanza imetwaa ubingwa ikishiriki fainali ya kombe la ligi ya mpira wa kikapu barani (Africa League BAL 2025), kwa kuibamiza Petro de Luanda ya Angola mabingwa watetezi wa kombe hilo kwa alama 88-67. Petro de Luanda imemaliza kwenye nafashi ya pili.
Mwakilishi wa Rwanda kwenye fainali za ligi ya mpira wa Kikapu barani Afrika BAL, APR BBC imemaliza kwenye nafasi ya tatu na kujishindia medali ya shaba baada ya kuwabwaga El Ittihad ya Misiri kwa alama 123-90 kwenye uwanja wa SunBet Arena jijini Pretoria. Kocha mkuu wa APR James Maye amefurahia kuweka rekodi kwa club kutoka Rwanda kwa mara ya kwanza kushiriki kwenye fainali hizo.
Kocha James Maye amesema, "Tuna kitu cha kujivunia tunajivunia vizuri, tulianzisha muungano kutoka kwa Mwenyekiti hadi ngazi ya chini. Tulitaka kujenga kitu cha kipekee. Hatukufanikwa kutwaa ubingwa, tulifanya hivo leo kuweza kufanya historia kwa taifa la Rwanda."
Axel Mpoyo wa APR amevunja rekodi kwa kufunga alama 32 katika mchezo mmoja dhidi ya Al Ittihad. Baada ya mechi Mpoyo amesema kuna haja kubwa kumaliza katika mfumo wa hali ya juu kwenye mashindano ya BAL msimu huu.
"Nadhani ilikuwa muhimu kwetu kwenda katika mashindano haya tukiwa kwenye hali ya juu, ndio ilikuwa lengo letu kubwa la mchezo wa leo na kuwa kwenye viwango vya juu, nadhani tumefanya hivo." Alisema Mpoyo
Mabingwa mwaka huu Al Ahly Tripoli walifika kwenye fainali baada ya kuwabwaga APR kwenye hatua ya Nusu fainali ya shindano hili huku Petro de Luanda ikiifunga EL Ettihad kwenye Nusu Fainali ya shindano hilo.
Michuano ya BAL imekuwa ni ya kitaaluma kama anaovoeleza Mkufunzi Henry Mwinuka, "Usajili uko juu kwa kweli siku hizi BAL ni biashara, ukiangalia ni taaluma kabisa, Ni kwamba wewe una kuja hapa unapewa hela nyingi, ukiwa na kazi yako, unakuja kwenye michezo. Na mshahara wa mpira wa kikapu unaonekana kuwa ni mkubwa zaidi kuliko hata wa kazini."
Jean Jacques Boisy a AL Ahly Tripoli ambapo kawaida ni mchezaji wa timu ya nishati REG ya Rwanda, ametawazwa mchezaji bora wa BAL 2025.
Kabasha yabeba kombe la Amani
Na katika mchezo wa soka , timu ya Kabasha imeibuka mshindi wa Kombe la Amani katika shindano lililoandaliwa mjini Goma kwa lengo la kuhimiza mshikamano na umoja katika eneo la Kivu Kaskazini ya DRC.
Katika fainali iliyochezwa jana jumapili kwenye uwanja wa Amani mjini GOMA, AS Kabasha iliibuka na ushindi dhidi ya Klabu ya Soka ya Goma Sport ya baada ya mikwaju ya penalti (7-6), kufuatia sare tasa (0-0) katika muda wa kawaida wa dakika 90.
Mchezo huo ulikuwa wa ushindani mkubwa na uliovutia, uliwafanya mashabiki waliojitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo kubwa la michezo.
Ingawa timu zote mbili zilionyesha safu ya ulinzi, hazikuweza kutumia vyema nafasi walizopata katika dakika zote 90 za mchezo.
AS Dauphin Noir Walinyakua nafasi ya 3 huku DC Virunga wakimaliza kwenye nafasi ya nne kwenye shindano hilo.