You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
App
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Algeria yawakamata watu saba kwa tuhuma za ujasusi
Waendesha mashitaka wanasema uchunguzi wa mahakama umeanzishwa.
Mkutano kati ya China na bara la Afrika kufanyika wiki hii.
Nchi nyingi za Afrika zimepokea mikpo kutoka kwa China na zinakabiliwa na mizigo ya madeni.
Ukraine yalishambulia kwa makombora eneo la Belgorod
Mtu mmoja ameuwawa katika mashambulizi hayo.
Rais wa Mexico awasilisha ripoti kuhusu utendaji wa serikali
Obrador ameto ahotuba ndefu akielezea mafanikio ya utawala wake
02.09.2024 Matangazo ya Asubuhi
Katika matangazo yetu ya asubuhi hivi leo utasikia makala zetu za Mbiu ya Mnyonge, Makala yetu Leo, Mtu na Mazingira, Vijana Tugutuke na Jukwaa la manufaa+++Sikiliza ya Dunia Yetu Leo Asubuhi kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW Bonn.
Chama cha AfD chashinda uchaguzi Thuringia
Wachambuzi wana wasiwasi kuhusu kuimarika kwa chama cha AfD nchini Ujerumani.
Taarifa ya Habari ya Asubuhi 02.09.2024
Chama cha Mbadala kwa Ujerumani AfD chashinda uchaguzi wa jimbo la mashariki la Thuringia. China yautaka Umoja wa Ulaya uwe makini kuhusu masuala ya bahari ya China Kusini. Na Viongozi wa nchi za Afrika waelekea Beijing kuhudhuria mkutano kati ya China na bara la Afrika.
01.09.2024 Matangazo ya Jioni
Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya,Joseph Borrell amesema ameshtushwa na mauaji ya mateka 6 raia wa Israel waliokuwa wakizuiliwa na kundi la wanamgambo la Hamas. Miili ya watu hao ilikutwa katika mji wa Rafah katika ukanda wa Gaza.
01.09.2024 - Matangazo ya Mchana
Kampeni ya kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Polio imeanza katika Ukanda wa Gaza. Afisa wa huduma za Afya Moussa Abed wa wizara ya Afya ya Gaza iliyo chini ya Hamas amesema chanjo zimeanza kutolewa Jumamosi ingawa maafisa walisema awali kuwa chanjo hiyo ingeanza rasmi kutolewa Jumapili.
31.08.2024 Matangazo ya Jioni
Helikopta iliyowabeba watu 22 yatoweka Urusi.|Ujerumani yahitimisha shughui za kijeshi Niger|Ufilipino na China zashutumiana kwa uchokozi Bahari ya Kusini mwa China|Wahamiaji 28 waliotelekezwa waokolewa mpakani mwa Tunisia na Algeria.
31.08.2024 Matangazo Ya Mchana
Mashambulizi yaendelea kuripotiwa Ukanda wa Gaza+++Umoja wa Mataifa watoa dola milioni 100 kukabiliana na matukio ya dharura ya kibinaadamu+++Katibu Mkuu wa NATO asema uvamizi wa kushtukiza wa Ukraine katika mkoa wa Kursk wa Urusi ni halali
31.08.2024:Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Umoja wa Mataifa watoa dola milioni 100 kuzisaidia nchi 10 kukabiliana na matukio ya dharura ya kibinaadamu. WHO yaahidi kuwa Chanjo za mpox zinatarajiwa kuwasili hivi karibuni nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Idadi ya vifo yaongezeka kufuatia operesheni ya Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
30.08.2024 - Matangazo ya Jioni
Rais wa Rwanda Paul Kagame amewatimuwa jeshini maafisa 20 wa vyeo vya juu, akiwemo wa cheo cha Meja Jenerali Martin Nzaramba+++Ujerumani imesema leo kuwa imewatimua wahalifu wa Afghanistan kurejea nchini mwao kwa mara ya kwanza tangu mamlaka ya Taliban ilipoingia madarakani kimabavu mnamo mwaka 2021.
Afrika katika magazeti ya Ujerumani
Maswala ya Afrika yaliyoangaziwa na magazeti ya Ujerumani mnamo wiki hii ni pamoja na mvutano wa miaka mingi kati ya Misri na Ethopia juu ya udhibiti wa maji ya mto Nile. Mlipuko wa maambukizi ya virusi vya Mpox kwenye nchi kadhaa za Afrika. Mjerumani, Bruno Labbadia, atakuwa kocha wa timu ya taifa ya kandanda ya Nigeria.
30.08.2024 - Matangazo ya Mchana
Dunia leo inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Watu Waliotoweka+++Urusi na Ukraine zimekabiliana vikali kivita usiku wa kuamkia leo, ambapo droni na mashambulizi ya anga yamesababisha watu 9 kujeruhiwa+++Israel imefanya shambulio la angani katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa leo Ijumaa wakati operesheni yake kubwa ya kijeshi ikiingia siku ya tatu
30.08.2024 - Matangazo ya Asubuhi
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer amesema alizungumzia mipango yake ya kurekebisha uhusiano na Ufaransa na Umoja wa Ulaya kwa ujumla, wakati wa mazungumzo na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mjini Paris+++Wakopeshaji wa China waliidhinisha mikopo yenye thamani ya dola bilioni 4.61 kwa Afrika mwaka jana, ikiwa ni ongezeko la kwanza la kila mwaka tangu mwaka 2016
30.08.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Israel yakubali kusitisha mapigano Gaza kwa siku 3 kupisha chanjo ya Polio kwa watoto. Mkuu wa Shirika la kimataifa la kudhibiti matumizi ya nyuklia kuelekea Ukraine wiki ijayo. Serbia yasaini mkataba wa dola bilioni 3 wa kununua ndege za kivita za Ufaransa.
Israel kusitisha mapigano Gaza kupisha chanjo ya Polio
Israel itasitisha mapigano kwa siku 3 na kampeni hiyo ya chanjo itaanza Septemba mosi katika eneo lote la Gaza.
29.08.2024 - Matangazo ya Jioni
Mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani Jake Sullivan amekutana leo na Rais wa China Xi Jinping mjini Beijing, na kukamilisha siku tatu za mazungumzo yaliolenga kupunguza msuguano kati ya mataifa hayo mawili+++Michezo ya Olimpiki kwa wanariadha wenye Ulemavu tayari imeanza kutimua vumbi jijini Paris kipyenga rasmi kilipulizwa jana jioni kwa shamrashamra.
29.08.2024 - Matangazo ya Mchana
Jeshi la Israel linasema kuwa limewaua wanamgambo wengine watano akiwemo kamanda wa Palestina mwenye umaarufu, katika operesheni kubwa ndani ya eneo linalokaliwa kimabavu la Ukingo wa Magharibi+++Ethiopia imeonya kwamba ujumbe mpya unaoongozwa na Umoja wa Afrika nchini Somalia AUSSOM, unaweza kuzidisha hali ya mvutano zaidi katika eneo hilo.
29.08.2024 - Matangazo ya Asubuhi
Mapigano yanaendelea kurindima mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo licha ya serikali kusaini makubaliano ya kusitisha vita na kundi la waasi wa M23+++Mwaka mmoja umetimia tangu yalipotokea mapinduzi ya kijeshi ambayo hayakuhusisha umwagaji wa damu nchini Gabon na yaliyomwondoa Rais Ali Bongo Odimba madarakani na kuumaliza utawala wa kifamilia uliodumu kwa miaka 55
29.08.2024 - Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani lasitisha harakati zake Gaza baada ya gari la wafanyakazi wake kushambuliwana vikosi vya Israel. Rais wa Ukraine asema kuwa wanajeshi wake wanakuchukua udhibiti wa maeneo zaidi huko Kursk nchini Urusi. Shirika la afya la Umoja wa Afrika limesema kuwa linakaribia kupata karibu dozi milioni moja za chanjo ya ugonjwa wa homa ya nyani.
28.08.2024 Matangazo ya Jioni
Waziri mkuu Keir Starmer asema Uingereza haiwezi kurudi kwenye Umoja wa Ulaya lakini inataka kurudisha mahusiano ya karibu na EU+++Shambulizi la Urusi lawauwa watu 6 Donetsk, nchini Ukraine+++Israel yashambulia kote Gaza, vifaru vyaingia ndani kabisaa ya Khan Younis
28.08.2024 Matangazo ya Mchana
Israel yaanzisha operesheni kali Ukingo wa Magharibi+++Urusi yalishinikiza shirika la AIEA kuwa na msimamo wa wazi kuhusu usalama wa nyuklia+++Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula, WFP yawachunguza maafisa wake nchini Sudan kwa ulaghai+++Waziri Mkuu wa Uingereza aitembelea Ujerumani kwa mara ya kwanza
28.08.2024 Matangazo ya Asubuhi
Wanasayansi wanasema aina mpya ya kirusi cha Mpox kinabadilika haraka kuliko ilivyodhaniwa+++Burundi mojawapo kati ya mataifa masikini zaidi duniani inakumbwa na uhaba wa mahitaji ya msingi+++Magonjwa ya kuendesha yanaua hadi watoto 54 kila siku nchini Uganda+++Mapema mwezi huu, Ujerumani na Ufilipino ziliridhia kukamilisha makubaliano ya ulinzi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Taarifa ya Habari za Ulimwengu Asubuhi 28 Agosti 2024
Sikiliza Taarifa ya Habari za Ulimwengu Asubuhi 28 Agosti 2024 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW, Bonn.
27.08.2024 - Matangazo ya Jioni
Mchakato wa kuwania uongozi wa kamisheni ya Umoja wa Afrika umeanza rasmi baada ya Raila Odinga kuzinduliwa kuwa mwakilishi wa Afrika Mashariki+++Rais wa Ufaransa Emmanuel anakabiliwa na kibarua kigumu kuitisha mazungumzo mapya kuhusu uundwaji wa serikali, baada ya vyama vya siasa za mrengo wa kushoto kukataa kushiriki tena
27.08.2024 - Matangazo ya Mchana
Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya Atomiki – IAEA Rafael Grossi ameanza leo ziara ya kufanya uchunguzi huru wa hali ilivyo katika kinu cha nyuklia cha Kursk nchini Urusi+++Takriban watu 30 wameuawa baada ya kuporomoka kwa bwawa la Arbaat nchini Sudan kutokana na mafuriko yaliosababishwa na mvua kubwa inayonyesha nchini humo
27.08.2024 - Matangazo ya Asubuhi
Nchini Ujerumani mjadala unaendelea kuhusu kisa cha kuuwawa watu watatu walioshambuliwa kwa kisu katika mji wa magharibi wa Sölingen+++Maswali yanayojikita kuhusu raia, makaazi, kilimo na ufugaji ni miongoni mwa yale watakayoulizwa raia kwenye sensa ya kitaifa iliyoanza nchini Burundi
27.08.2024 - Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Sikiliza Taarifa ya Habari za Ulimwengu Asubuhi 27 Agosti 2024 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW.
26.08.2024 Matangazo ya Jioni
Iran leo imepongeza shambulizi la droni na makombora lililofanywa na kundi la Hezbollah+Kansela Olaf Scholz leo Jumatatu ameutembelea mji wa Solingen+Mahakama nchini Uganda imeongeza muda wa rumande wa wafuasi 36 wa chama cha upinzani FDC hadi tarehe 17 ambapo watarudi tena mahakamani kuhusiana na mashtaka ya ugaidi.
Urusi yaishambulia kwa droni na makombora Ukraine.
Watu watatu wameuwawa Ukraine na umeme ukatwa nchi nzima kufuatia uharibifu wa miundo mbinu ya nishati
Je, kanda ya mashariki ya kati imetumbukia kwenye vita kamili?
Je, kanda ya mashariki ya kati imetumbukia kwenye vita kamili?
26.08.2024 Matangazo ya Mchana
Mazungumzo ya kusaka makubaliano ya kusitisha mapigano kwenye Ukanda wa Gaza yamemalizika bila mafanikio yoyote mjini Kairo+Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amewasili katika mji wa Solingen+Kamati ya Kanda ya Afrika ya Shirika la Afya Duniani, WHO inaanza mkutano wake wa siku tano katika Jamuhuri ya Kongo.
Upinzani Tanzania waupania uchaguzi wa serikali za mitaa
Siku chache baada ya kutangazwa tarehe ya uchaguzi wa serikali za mitaa nchini Tanzania, vyama vya upinzani katika taifa hilo la Afrika Mashariki limeuvalia njuga uchaguzi huo vikionesha mwamko wao katika kushiriki ilhali vikijipanga kuondoa mikwamo wanayodhani itazuia ushindi wao. Sikiliza ripoti ya Florence Majani kutoka Dar es Salaam.
WHO kanda ya Afrika kujadili kitisho cha ugonjwa wa Mpox
WHO kanda ya Afrika inaanza mkutano wake wa siku tano katika Jamhuri ya Kongo kujadili kitisho cha ugonjwa wa Mpox.
26.08.2024 Matangazo ya Asubuhi
Katika matangazo yetu ya asubuhi hivi leo utasikia makala zetu za Mbiu ya Mnyonge, Makala yetu Leo, Mtu na Mazingira, Vijana Tugutuke na Jukwaa la manufaa. Sikiliza ya Dunia Yetu Leo Asubuhi kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW Bonn.
24.08.2024- Matangazo ya Asubuhi
Nchini Marekani kampeni za uchaguzi zinagharimu mabilioni ya dola, fedha hizo zinatoka kwa mabwanyenye pamoja na wafanyabiashara++Mfumo maalumu unaosaidia kutoa tahadhari mapema kabla ya majanga, huenda ukayasaidia mataifa kufikia malengo ya Umoja wa Mataifa++Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Nancy Faeser anataka kuanzisha sheria kali ya kuzuia kubeba visu hadharani.
25.08.2024 Matangazo ya Jioni
Ujumbe wa Israel wawasili Cairo kwa majadiliano kuhusu Gaza++Zelensky: Nitaunga mkono India kuwa mwandaaji wa mkutano wa pili wa amani++Chanjo elfu kumi za Mpox zinatarajiwa kuwasili Afrika juma lijalo
25.08.2024 Matangazo ya Mchana
Israel imesema imeshambulia Lebanon ili kuzuia mashambulizi yaliopangwa ya Hezbollah++Urusi yaishambulia Ukraine kwa makombora na droni++Burhan asema hawatashiriki mazungumzo ya amani na badala yake watapambana kwa miaka 100
24.08.2024 Taarifa ya Habari Asubuhi
Watu watatu wauawa katika shambulizi la kisu katika tamasha magharibi ya Ujerumani // Marekani yasema hatua zimepigwa katika mazungumzo ya Cairo ya usitishaji vita Gaza // Na Robert F Kennedy Jr asitisha kampeni yake ya urais na kumuidhinisha Trump
Modi amrai Zelensky kukaa mezani kumaliza vita na Urusi
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amemrai Rais Volodoymyr Zelensky wa Ukraine kukaa mezani kumaliza vita na Urusi.
23.08.2024 - Matangazo ya Jioni
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi anayeitembelea Ukraine amemtolea mwito kiongozi wa nchi hiyo, Volodoymyr Zelensky, kufanya mazungumzo na Urusi kwa dhamira ya kumaliza vita ndani ya ardhi ya Ukraine+++Afisa wa kundi la Hamas amemshtumu Waziri Mkuu wa Israel Benjamin kukataa kuafiki makubaliano ya mwisho ya kufikia mapatano ya kusitisha vita Gaza
Afrika katika Magazeti ya Ujerumani
Virusi vinavyosababisha homa ya nyani vinaendelea kusambaa kwa kasi barani Afrika.
23.08.2024 - Matangazo ya Mchana
Makamu wa Rais Kamala Harris amewataka Wamarekani kukataa migawanyiko ya kisiasa na badala yake kuchora kile alichokiita njia mpya ya kusonga mbele+++Waziri Mkuu wa India Narendra Modi anaitembelea Ukraine leo kwa mazungumzo na Rais Volodymyr Zelensky katika kile kinachotizamwa kuwa jitihada za serikali mjini New Delhi kuuonesha ulimwengu kwamba haijachagua upande
Modi ziarani nchini Ukraine kwa mazungumzo na Zelensky
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi yuko Ukraine kwa mazungumzo na Rais Volodymyr Zelensky.
23.08.2024 - Matangazo ya Asubuhi
Mkutano mkuu wa chama cha Democratic uliingia siku yake ya nne na ya mwisho hapo jana ambapo Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, alisubiriwa kwa hamu kutoa hotuba+++Rais mstaafu wa Afrika Kusini na kiongozi wa chama cha uMkhonto weSizwe Jacob Zuma, amemlaumu Rais Cyril Ramaphosa kwa kuongoza chama tawala cha ANC kinyume na malengo ya waanzilishi wa chama hicho
23.08.2024 Taarifa ya Habari Asubuhi
Kamala Harris aahidi kuwa rais wa Wamarekani wote wakati mkutano mkuu wa Democratic ukifikia tamati // Waziri mkuu wa India Narendra Modi atoa wito wa mazungumzo kuhusu mzozo wa Ukraine // Na waandamanaji walazimisha kusitishwa mabadiliko ya sheria ya uchaguzi Indonesia
22.08.2024 - Matangazo ya Jioni
Kiongozi wa upinzani na mwanasiasa mkongwe nchini Kenya Raila Odinga, ametangaza kujiondoa kwenye jukwaa la siasa za Kenya+++Waziri mpya wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araghchi anapanga kujisogeza karibu na mataifa ya Magharibi katika wakati ambapo nchi hiyo inakabiliwa na vikwazo vya kimataifa na kutengwa kisiasa
Walz: Nimeridhia kuwa mgombea mwenza wa Harris
Gavana wa Minnesota Tim Walz amekubali uteuzi wa kuwania umakamu wa rais wa Marekani kupitia chama cha Democrat.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 34 wa 153
Ukurasa unaofuatia