You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
App
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
12.09.2024 - Matangazo ya Jioni
Marekani imesema hivi leo kuwa itaendelea kuishinikiza Israel kuchukua hatua zaidi ili kuepusha maafa kwenye maeneo ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza+++Kinara wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amekabidhi uongozi wa chama cha ODM kwa gavana wa Kisumu Profesa Peter Anyang Nyong'o.
12.09.2024 - Matangazo ya Mchana
Hali inarejea kuwa ya kawaida katika viwanja vya ndege nchini Kenya baada ya wafanyakazi wa sekta hiyo kuusitisha mgomo uliodumu kutwa nzima hapo jana+++Marekani imesema inaunga mkono kuanzishwa kwa viti viwili vya kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya nchi za Afrika.
11.09.2024 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema upinzani unalitumia swala la uhamiaji kama mtaji wa kisiasa nchini humo/ Wafanyakazi wa uwanja wa ndege Kenya wakubali kusitisha mgomo
11.09.2024 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Mamia ya wafanyakazi katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi JKIA wamegoma dhidi ya mkataba kati ya serikali na mwekezaji wa kigeni/ Harris amkaanga Trump kwenye mdahalo wa televisheni
10.09.2024 - Matangazo ya Jioni
Waziri wa Ulinzi wa Israel amesema makubaliano ya muda ya kusitisha mapigano Gaza yanawezekana lakini akasisitiza kuwa suala la kumaliza vita ni jambo jingine+++Wanaharakati na watendaji katika masuala ya uchaguzi barani Afrika wameelezea utumiaji wa fedha nyingi katika kampeni za uchaguzi ni moaja ya kizingiti katika juhudi za kufanikisha demokrasia.
Mahakama kuu ya Ulaya yaamuru Google na Apple kulipa kodi
Hukumu hii inahitimisha mizozo ya muda mrefu ya kisheria kati ya pande hizo.
10.09.2024 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Wawakilishi wa kundi la mataifa yanayoinukia kiuchumi duniani BRICS wanatarajiwa kujadili juu ya vita vinavyoendelea nchini Ukraine/ Mkutano wa kilele wa kimataifa unaondelea Korea Kusini umetangaza "muongozo wa hatua" zitakazosimamia matumizi na uwajibikaji wa akili mnemba katika jeshi
EU, Marekani: Tutajibu ikiwa Iran inapeleka makombora Urusi
Umoja wa Ulaya umesema umepokea taarifa za kuaminika zinazoonesha kwamba Iran imeipatia Urusi makombora ya masafa.
09.09.2024 Matangazo ya Jioni
Masauni atakiwa kujiuzulu kufuatia kifo cha kada wa CHADEMA+++Ulimwengu uko kwenye njia panda asema Volker Turk+++Papa Francis awasihi viongozi,Timor Mashariki wawalinde watoto dhidi ya unyanyasaji wa kingono+++China yatamba katika michezo ya Olimpiki kwa walemavu Paris
Lishe bora katika kuandaa unyonyeshaji bora
Lishe bora ni kitu cha muhimu wakati mama anapokuwa mjamzito ili kujiandaa kwa ajili ya kumnyonyesha mwanae. Kama wengi tujuavyo, kila mama anahamasishwa kumnyonyesha mtoto wake miezisita ya mwanzo ili kupata lishe bora kabisa anayoihitaji katika ukuaji wake. Kuna mengi ambayo yatakunufaisha ukisikiliza makala ya Afya yako.
09.09.2024 Matangazo ya Mchana
Mwanasiasa wa upinzani 'alietekwa' Tanzania akutwa amekufa+++DNA kufanywa kutambua miili ya waliofariki Endarasha, Kenya+++ Volker Turk azitaka nchi kuchukua hatua dhidi ya Israel+++Ni wakati wa kuishirikisha Urusi kwenye mazungumzo ya kumaliza vita Ukraine - Olaf Scholz
09.09.2024 - Matangazo ya Asubuhi
Katika matangazo yetu ya asubuhi hivi leo utasikia makala zetu za Mbiu ya Mnyonge, Makala yetu Leo, Mtu na Mazingira, Vijana Tugutuke na Jukwaa la manufaa+++Sikiliza ya Dunia Yetu Leo Asubuhi kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW Bonn.
Watu 21 wauawa kwenye shambulizi la sokoni Sudan
Mashambulizi ya makombora yamewaua watu wasiopungua 21 kwenye soko moja kusini mashariki mwa Sudan jana Jumapili.
Mgombea urais wa upinzani Venezuela akimbilia Uhispania
Aliyekuwa mgombea urais wa upande wa upinzani nchini Venezuela Edmundo Gonzalez ameikimbia nchi hiyo.
Matangazo ya jioni: 07.09.2024
Maelfu waandamana Ufaransa kupinga kuteuliwa Barnier kuwa waziri mkuu. Polisi Kenya yaongeza kasi uchunguzi mkasa wa moto shuleni. Wakuu wa ujasusi wa Uingereza na Marekani wasifu shambulizi la Ukraine ndani ya Urusi. Kimbunga Yagi chasababisha vifo vya watu 4 Vietnam.
06.09.2024 - Matangazo ya Jioni
Washirika wa Ukraine wa nchi za Magharibi wanaokutana katika kambi ya kijeshi ya Marekani hapa Ujerumani,wameahidi kuisadia nchi hiyo katika mapambano yake dhidi ya Urusi+++Papa Francis leo Ijumaa amewasili nchini Papua New Guinea baada ya kuhitimisha ziara yake nchini Indonesia.
Afrika katika magazeti ya Ujerumani
Yaliyoandikwa kwenye magazeti ya Ujerumani juu ya Afrika wiki hii ni pamoja na swali lililoulizwa na gazeti la die tageszeitung, jee nani ni rafiki mkubwa kabisa wa China? Juu ya kifo cha mwanariadha wa Uganda Rebecca Cheptegei. Nchi tano ndizo hasa zinahusika kupeleka silaha zinazokoleza vita nchini Sudan.
06.09.2024 - Matangazo ya Mchana
Nchini Kenya wanafunzi 17 wa shule ya msingi ya Hillside Endarasha wamefariki dunia baada ya bweni lao kuunguwa moto usiku wa kuamkia leo+++Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine ameshiriki mkutano nchini Ujerumani uliowakusanya waungaji mkono wa kimataifa wa nchi yake.
06.09.2024 - Matangazo ya Asubuhi
Mkutano wa kilele unaoendelea mjini Beijing kati ya China na Afrika unamalizika hii leo+++Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu zinashika nafasi ya juu ya usalama wa mitandaoni katika orodha ya Umoja wa Mataifa.
06.09.2024 - Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Ujerumani inapanga kuongeza msaada zaidi wa kibinadamu kwa Ukanda wa Gaza// Polisi mjini Munich wamuua kijana aliyefyatua risasi karibu na ubalozi mdogo wa Israel // Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatazamiwa kukutana na Kansela Olaf Scholz hii leo mjini Frankfurt.
05.09.2024 - Matangazo ya Jioni
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemteua Michel Barnier kuwa Waziri Mkuu mpya+++Dozi za kwanza za chanjo dhidi ya homa ya nyani Mpox zimewasili leo katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Kinshasa+++Afisa wa polisi anayetuhumiwa kulituma na kulifadhili genge la vijana kumbaka na kumlawiti msichana mmoja nchini Tanzania amefikishwa mahakamani leo.
Mwangaza wa Ulaya:Viongozi wa EU wajadili msaada kwa Ukraine
Mzozo kati ya Urusi na Ukraine ambao unaelekea kuingia katika mwaka wa tatu unazidi kutokota. Mwishoni mwa mwezi Agosti, mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya walijadiliana kuhusu kuongeza msaada wa kijeshi kwa Ukraine. Lakini pia mzozo huo umezusha hali ya hofu kwa mataifa ya Baltic yanayopakana na Urusi ambayo yanahofia kwamba wakati wowote wanaweza pia kushambuliwa. Ungana na Bakari Ubena.
Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa
Kusikiliza matangazo, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi: kiswahili@dw.com
05.09.2024 - Matangazo ya Mchana
Rais Xi Jinping wa China leo hii ametoa ahadi ya kitita cha zaidi ya dola bilioni 50 kwa ufadhili wa mataifa ya Afrika katika kipindi cha miaka mitatu ijayo+++Mwanariadha wa Olimpiki wa Uganda Rebecca Cheptegei ambaye alichomwa moto na mpenzi wake huko nchini Kenya siku ya Jumapili amefariki dunia.
05.09.2024 - Matangazo ya Asubuhi
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekutana na mwenzake wa Misri Abdel Fattah el-Sisi mjini Ankara huku viongozi hao wakilenga kuimarisha uhusiano wao katika sekta ya gesi asilia na nishati ya nyuklia+++Huko nchini China kumesainiwa makubaliano ya mwanzo kuhusu mradi wa reli unaolenga kuimarisha mtandao wa usafiri wa reli na bahari katika kanda ya Afrika Mashariki.
04.09.2024 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Rais Zelensky amesema serikali yake inahitaji nguvu mpya na hatua ya kulifanyia mageuzi baraza lake la mawaziri/ Serbia yamuahidi Putin kwamba kamwe haitaigeuzia mgongo
04.09.2024 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Bobi Wine kupasuliwa baada ya kujeruhiwa mguuni/ China, Zambia, Tanzania zasaini makubaliano ya ukarabati wa reli
Mashambulizi ya Urusi yauwa 7 Lviv
Kremlin inapitia upya itifaki yake ya nyuklia kwa sababu mataifa ya Magharibi yanatishia maslahi ya usalama ya Moscow.
04.09.2024 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Mkutano wa kilele kati ya China na Afrika unaanza rasmi hii leo mjini Beijing/ Asilimia 60 ya vijana wa Kiafrika wanatazamia kuzihama nchi zao kutokana na rushwa isiyodhibitiwa ambayo inatishia maisha yao ya baadaye
04.09.2024 Taarifa ya Habari ya Asubuhi
China na Nigeria kuhimiza ushirikiano katika masuala ya fedha. Umoja wa Ulaya waikosoa Mongolia kwa kutomkamata rais wa Urusi, Vladimir Putin. Na Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine apigwa risasi na kujeruhiwa mguuni.
03.09.2024 - Matangazo ya Jioni
Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema limefanikiwa kuwapatia chanjo ya polio watoto wengi zaidi kwenye Ukanda wa Gaza+++Mkutano wa kilele kati ya viongozi wa Afrika na China unaanza kesho mjini Beijing, huku China ikiahidi kuimarisha ushirikiano wa ngazi ya juu na nchi za Afrika.
WHO yapindukia malengo ya chanjo ya polio Gaza
WHO imefanikiwa kuwapatia chanjo ya polio watoto wengi zaidi kwenye Ukanda wa Gaza kuliko iliyokuwa imetarajia.
Kukatika kwa mawasiliano baina ya marafiki, tatizo ni nini?
Hali ya kupotezeana imekuwa jambo la kawaida hasa baada ya marafiki kuunganishwa kupitia mitandao ya kijamii.
03.09.2024 Matangazo Ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Rais wa Urusi Vladimir Putin aizuru Mongolia licha ya waranti wa kukamatwa na ICC/ China yawakaribisha viongozi wa Afrika kwenye kongamano la kilele la China-Afrika
Netanyahu alemewa na shinikizo kufikia makubaliano
Shinikizo linazidi kumuelemea Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wa Israel kumtaka afikie makubaliano ya kusitisha mapigano.
Matangazo ya Asubuhi 03.09.2024
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Meli mbili zashambuliwa nje ya eneo linalodhibitiwa na Wahouthi/ Viongozi wa Afrika wanakutana mjini Beijing,katika mkutano wa kilele kati ya China na Afrika
03.09.2024 Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Rais wa Marekani Joe Biden na makamu wake Kamala Harris wafanya kampepni ya pamoja kwa mara ya kwanza Pennsylvania.
Biden na Harris wafanya kampeni kwa pamoja
Harris anatafuta kuungwa mkono na vyama vya wafanyakazi na tabaka la wafanyakazi, kundi ambalo Trump analitegemea.
Marekani yaikamata ndege ya rais wa Venezuela Nicolas Maduro
Mchakato wa kuinunua ndege hiyo ulikiuka vikwazo ilivyowekewa Venezuela.
Uturuki yawakamata watu 15 waliowashambulia Wamarekani
Vuguvugu la vijana wazalendo limekiri limewashambulia wanajeshi hao wa Marekani kupinga wasiitie najisi nchi yao.
Umoja wa Mataifa wautanzua mgogoro wa benki kuu ya Libya
Mazungumzo hayo yamedumu kwa muda mrefu lakini yameleta tija.
Watu 10 wauwawa katika shambulizi la baa mashariki mwa Congo
Msemaji wa jeshi ngazi ya mkoa amesema washambuliaji waliwavizia wanajeshi hao.
Watu zaidi ya 400 wamenyongwa Iran mwaka huu
Iran ni nchi inayonyonga watu wengi zaidi ulimwenguni mbali na China.
Meli mbili zashambuliwa nje ya eneo la Wahouthi
Hakuna uhabifu mkubwa uliotokea wala maafa au majeruhai.
02.09.2024- Matangazo ya Jioni
Biden asema haamini Netanyahu anafanya vya kutosha mzozo wa Gaza+++China yawalaki viongozi wa Afrika kuelekea mkutano wa kilele +++Kongo yazika miili ya watu 200 waliouwawa vitani na M23
Wanawake na Maendeleo
Bi. Asawar Mustafa, mwanamke mkimbizi kutoka Sudan anayefanya kazi ya ufundi wa magari nchini Libya amefanikiwa kwa vitendo na kuonesha kwamba mwanamke pia anaweza kuwa fundi gereji hodari na kwamba kazi hiyo si ya wanaume pekee. Makala hii imeandaliwa na Zainab Aziz.
China yaihimiza EU kuhusu bahari ya China Kusini
Ni baada ya umoja wa Ulaya kutoa kauli kuhusu tukio lililotokea wikendi kati ya China na Ufilipino.
02.09.2024 Matangazo ya Mchana
Waisraeli waanzisha mgomo wakishinikiza kuachiliwa kwa mateka+++Serikali ya muungano ya Ujerumani kuyumbishwa na matokeo ya majimbo+++Kongo: Walimu wagoma wakishinikiza mazingira bora ya kazi+++Uganda yatangaza kusambaa kwa homa ya nyani
Mgomo wafanyika Israel kushinikiza kuachiliwa kwa mateka
Mgomo huo unaoongozwa na muungano wa mashirika ya wafanyakazi ya Israel, Histadrut.
Algeria yawakamata watu saba kwa tuhuma za ujasusi
Waendesha mashitaka wanasema uchunguzi wa mahakama umeanzishwa.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 33 wa 152
Ukurasa unaofuatia