You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
App
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Matangazo ya Mchana: 26.01.2025
Walinda amani 9 wauwawa katika mapambano na waasi wa M23 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Donald Trump azitaka nchi za kiarabu kuwakubali wakimbizi zaidi kutoka Gaza. Idadi ya waliouwawa Sudan katika shambulio hospitalini yafikia watu 70
Makala ya Afrika wiki hii
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mapigano yanaendelea kuripotiwa kati ya jeshi la FARDC na waasi wa M23. Umoja wa Afrika ulieleza kusikitishwa na uamuzi wa Rais Donald Trump wa kuiondoa Marekani kwenye Shirika la Afya Duniani WHO. Na siasa za huko Tanzania zilipamba moto. Ungana na Bakari Ubena Bakari Ubena.
24.01.2025 Matangazo ya Jioni
Mapambano yanaendelea karibu na mji wa Goma, huku taarifa zikielezea kuuliwa kwa gavana wa kijeshi wa jimbo hilo, Jenerali Peter Chirimwami+++Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC) imependekeza kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa zaidi ya wabunge 10 kwa matamshi ya chuki.
Afrika katika Magazeti ya Ujerumani
Juma hili, mwenendo wa vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umemulikwa, maafa yaliyotukia kwenye mgodi wa zamani wa Stilfontein Afrika ya Kusini yameangaziwa na Tanzania imethibitisha uwepo wa virusi vya marburg nchini humo.
24.01.2025 Matangazo ya Mchana
Hali ya mambo Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inazidi kuwa mbaya+++Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema usiku wa kuamkia leo imefanikiwa kudhibiti mashumbulizi ya droni za Ukraine.
Gavana: Watu wanakimbia operesheni ya Israel mji wa Jenin
Afisa mmoja amesema watu wanazikimbia nyumba zao huko Ukingo wa Magharibi baada ya Israel kufanya uvamizi wa kijeshi.
23.01.2025 Matangazo ya Jioni
Afisa mmoja wa Kipalestina amesema mamia ya watu wameanza kukimbia nyumba zao kwenye mji wa Jenin ulioko Ukingo wa Magharibi ambako vikosi vya Israel vinafanya operesheni kubwa ya kijeshi+++Uchaguzi ndani ya Chama Kikuu cha upinzania Tanzania (CHADEMA) umemalizika huku ukiibua maswali lukuki ikiwamo uwakilishi finyu wa wanawake katika safu ya uongozi
23.01.2025 Matangazo ya Mchana
Mji wa Sake ulioko kilomita 20 kutoka Goma huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umetekwa na waasi wa M23+++Rais wa Marekani Donald Trump anatazamiwa hii leo kuhutubia kwa njia ya video kwenye mkutano wa Jukwaa la Kimatifa la Uchumi, katika kitongoji cha DAVOS.
Rubio asema msaada wa Marekani kwa Israel "hautayumba"
Waziri mpya wa mambo ya kigeni wa Marekani, Marco Rubio, amesisitiza "uungaji mkono usioyumba" wa Washington kwa Israel.
22.01.2025 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametilia mkazo onyo lake kuhusu mabadiliko ya tabia nchi na kusema kiu ya dunia katika matumzi ya nishati ya visukuku ni hatua mbaya ambayo haitamuacha yeyote salama/ Kiongozi mpya wa Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania CHADEMA, Tundu Lissu amesema ananuwia kufanya mabadiliko makubwa ndani ya chama hicho
22.01.2025 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania kimechagua Tundu Lissu kuwa kiongozi mpya kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba, wakati ambapo kinakabiliwa na ongezeko la ukandamizaji wa kisiasa/ Makubaliano legelege ya kusitisha mapigano kwenye Ukanda wa Gaza yanaendelea kutekelezwa
Makubaliano ya Gaza yaendelea, Israel yaishambulia Jenin
Usitishaji mapigano ya Gaza yanaendelea kutekelezwa, huku Israel ikiendesha ya kijeshi kwenye Ukingo wa Magharibi.
21.01.2025 Matangazo ya Jioni
Viongozi wanaomaliza muda wao ndani ya CHADEMA, Freeman Mbowe na Tundu Lissu, wametoa salamu zao za mwisho kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho leo+++Shirika la Afya duniani WHO limeilalamikia hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kusaini amri ya kuanza mchakato wa kuiondoa nchi yake katika Shirika hilo
21.01.2025 - Matangazo ya Mchana
Trump amewasamehe takribani watu 1,500 waliovamia majengo ya bunge mnamo Januari 6, 2021, katika ishara muhimu kwa watu waliowashambulia polisi walipokuwa wakijaribu kuwazuia wabunge kuthibitisha kushindwa kwake katika uchaguzi wa 2020+++Makubaliano ya usitishaji vita kwenye Ukanda wa Gaza yameingia siku yake ya tatu hivi leo
20.01.2025 Matangazo ya Jioni
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametangaza hii leo kuwepo kwa mlipuko wa virusi hatari vya Marburg kaskazini magharibi mwa nchi hiyo// Rais mteule Donald Trump ataapishwa kuwa rais wa 47 wa Marekani// Idara ya Huduma za Dharura za Kiraia ya Palestina, imesema leo kuwa shughuli inaendelea ya kutafuta miili ya maelfu ya Wapalestina wanaoaminika kufukiwa chini ya vifusi.
Je, CCM imekiuka taratibu za teuzi zake kuelekea uchaguzi?
Chama tawala nchini Tanzania, CCM kimemteua Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu ujao. Hata hivyo kuna sauti zinazolalamikia kukiukwa kwa utaratibu wa chama kutokana na mchakato huo kuonekana kufanyika mapema kuliko kawaida. Mohammed Khelef amezungumza na Katibu mwenezi na Itikadi taifa Amos Makalla kuhusu udharura huo. Sikiliza.
20.01.2025 Matangazo ya Mchana
Mkutano mkuu wa chama cha Mapinduzi CCM umemalizika huku chama hicho kikimteua Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu ujao// Makubaliano tete ya usitishaji vita Gaza kati ya Israel na Hamas yameendelea kuheshimiwa//Hali ya wasiwasi inashuhudiwa katika eneo la Molo nchini Kenya baada ya mauaji ya mwanaharakati kijana aliyekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali.
Matangazo ya Jioni: 18.01.2025
Stephen Wasira apitishwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara. Israel yasema itawaachilia zaidi wafungwa 1900 wa Kipalestina kutoka kwenye magereza yake. Lebanon yasema vikosi vya Israel lazima viondoke nchini mwake kabla ya Januari 26.
Matangazo ya Mchana:18.01.2025
Baraza la mawaziri la Israel laidhinisha makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza. Urusi yaushambulia mji mkuu wa Ukraine, watu watatu wauawa. Zaidi ya watu laki mbili wamekimbia ghasia mashariki mwa DRC tangu Januari 1 mwaka huu.
Matangazo ya Asubuhi: 18.01.2025
Taarifa ya Habari ya Asubuhi: 18.01.2025
Baraza la mawaziri la Israel laidhinisha makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza na kuachiliwa kwa mateka.+++ Makundi ya kutetea haki za binadamu yanahofia kufanyika kwa "maovu makubwa" huko Uganda wakati nchi hiyo inapojiandaa kwa uchaguzi mkuu mwaka ujao. +++ Umoja wa Mataifa umesema kuwa watu wapatao 230,000 wamekimbia ghasia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tangu kuanza kwa 2025.
17.01.2025 Matangazo ya Jioni
Baraza la usalama la Israel limependekeza kukubaliwa kwa mkataba wa usitishaji vita kwenye Ukanda wa Gaza na kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Kipalestina+++Rais wa Iran Masoud Pezeshkian na mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin wamesaini ''mkataba wa ushirikano wa kina wa kimkakati'' hatua ambayo huenda ikasababisha wasiwasi kwa serikali za Magharibi.
17.01.2025 Matangazo ya Mchana
Rais Paul Kagame wa Rwanda kwa mara nyingine tena ameilaani jamii ya kimataifa ambayo imekuwa ikikosoa demokrasia nchini Rwanda+++Wapalestina kwenye Ukanda wa Gaza wameanza kurudi kwenye shughuli za maisha ingawa kwa tahadhari wakati wakingojea uamuzi wa baraza la mawaziri la Israel.
Gaza wasubiri kwa hadhari utekelezaji wa usitishaji mapigano
Makubaliano yalifikiwa baada ya miezi 15 za ukanda huo kushambuliwa takribani kila siku na jeshi la Israel.
17.01.2025 Matangazo ya Asubuhi
Ukanda wa Gaza umekumbwa na uharibifu mkubwa kufuatia vita vya zaidi ya miezi 15 kati ya Israel na Hamas+++Nchini Rwanda, malalamiko ya wananchi yanaendelea kufuatia ongezeko la matumizi ya dola za Marekani katika soko la ndani.
17.01.2025 Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Marekani imesema ina imani kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza yatatekelezwa kama ilivyopangwa. +++ Makumi ya watu wamejeruhiwa na wengine kadhaa wameyakimbia makazi yao kufuatia mapigano mashariki mwa DRC. +++ Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer anatarajiwa kuwasili Poland hivi leo baada ya ziara yake nchini Ukraine.
16.01.2025 Matangazo ya Jioni
Wanamgambo wa Hamas wamepinga madai ya Israel kwamba kundi hilo linajaribu kuzuia makubaliano ya kusitisha mapigano na kurejeshwa kwa mateka yaliyoatangazwa jana Jumatano na wapatanishi wa mzozo baina yao+++Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA leo kinakamilisha hatua yake ya kwanza ya uchaguzi wa mabaraza yake ya uongozi:
16.01.2025 Matangazo ya Mchana
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Baraza la Mawaziri halitakutana hii leo kuidhinisha makubaliano ya kusitisha mapigano huko Ukanda wa Gaz+++Rais mpya wa Msumbiji ameahidi kuiunganisha nchi yake iliyogawika vibaya kufuatia uchaguzi uliomuweka madarakani.
Chapo aahidi kuiunganisha Msumbiji
Rais mpya wa Msumbiji ameahidi kuiunganisha nchi yake iliyogawika kufuatia uchaguzi uliomuweka madarakani
16.01.2025 Matangazo ya Asubuhi
Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza kuwa makubaliano ya usitishaji vita na kuachiliwa kwa mateka yamefikiwa kati ya Israel na Hamas+++Joto la uchaguzi katika chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, linazidi kushika kasi.
16.01.2025 Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Israel na Hamas wafikia makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza. +++ Waasi wa ADF waua watu 10 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. +++ Rais wa Marekani Joe Biden atoa hotuba ya kuaga na kuelezea wasiwasi wake kuhusu utawala ujao wa Trump.
15.01.2025 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Shirika la Afya Duniani, WHO limesema mripuko wa ugonjwa unaoshukiwa kuwa ni Marburg umewauwa watu wanane katika vijiji vya mkoa wa Kagera, ulioko kaskazini-magharibi mwa Tanzania/ Makubaliano ya kuvimaliza vita vya Gaza bado yasubiriwa
15.01.2025 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Hamas yakubali rasimu ya makubaliano ya kusitisha vita Gaza/ Urusi yaishambulia Ukraine kwa makombora, droni
Taarifa ya Habari za Ulimwengu Asubuhi Januari 15, 2025
Sikiliza Taarifa ya Habari za Ulimwengu Asubuhi Januari 15, 2025 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW, Bonn.
14.01.2025 Matangazo ya Jioni
Jumuiya ya Kujihami ya NATO imetangaza kikosi kipya kitakachoilinda miundombinu muhimu ya chini ya bahari katika Bahari ya Baltic+++Takribani watu 100 wameripotiwa kufariki dunia baada ya kukwama kwa miezi kadhaa katika mgodi wa dhahabu uliotelekezwa kaskazini magharibi mwa Afrika Kusini.
14.01.2025 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Makubaliano ya kusitisha vita vya Gaza yanukia/ Waziri wa ulinzi wa Ujerumani aizuru Kiev
14.01.2025 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Mazungumzo ya kusitisha vita kati ya Israel na Hamas yapiga hatua kubwa/ Serikali ya mseto ya Kansela Olaf Scholz imeporomoka
13.01.2025 Matangazo ya Jioni
Mwanaharakati na mkosoaji wa serikali ya Tanzania Maria Sarungi amewaambia waandishi wa habari kwamba kamwe hatotishika wala kunyamazishwa// Bunge jipya la Msumbiji limezinduliwa leo Jumatatu sambamba na hafla ya kuwaapisha wabunge wapya// Wazima moto huko Los Angeles nchini Marekani wanaendelea kupambana kuudhibiti moto wa nyika.
Urusi, Iran kusaini mkataba wa ushirikiano wa kimkakati
Urusi imelaumu vikwazo vipya vya Marekani na Uingereza ikisema vinahatarisha biashara ya kimataifa.
Licha ya hali ngumu, Scholz aapa kupambana hadi mwisho
Sabine Kinkartz anasema SPD inategemea siasa za kimataifa zitaibeba kwenye uchaguzi wa Februari 23.
13.01.2025 Matangazo ya Mchana
Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limesema limeyakomboa maeneo kadhaa wilayani Masisi ambayo yalikuwa yamedhibitiwa na waasi wa M23// Mwanasheria mkuu wa zamani katika serikali ya Rais William Ruto wa Kenya, Justin Muturi amekuwa wa kwanza kuzungumzia wimbi la utekaji nyara vijana wanaoikosoa serikali// Tamasha la ibada linalofahamika kama Kumbh Mela lafunguliwa India.
Ulaya, Arabuni wakutana kuijadili Syria
Mkutano huu unafungua mlango wa ujenzi mpya kwa taifa hilo muhimu kimkakati katika eneo la Mashariki ya Kati.
Taarifa ya Habari za Ulimwengu Asubuhi Januari 13, 2025
Sikiliza Taarifa ya Habari za Ulimwengu Asubuhi Januari 13, 2025 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW, Bonn.
Matangazo ya Jioni: 12.01.2025
Jeshi la Israel limesema litashambulia kambi ya wakimbizi iliyopo kaskazini mwa Ukanda wa Gaza ya Nuseirat. +++ Umoja wa Ulaya kuamua juu ya kuilegezea vikwazo Syria mwishoni mwa mwezi Januari.+++ Na Urusi yadai kuviteka vijiji viwili mashariki mwa Ukraine.
Matangazo ya Mchana: 12.01.2025
Wanadiplomasia wa nchi za Kiarabu na Ulaya wakutana Saudia kuisaidia Syria.+++ Korea Kusini yathibitisha madai ya Ukraine ya kukamatwa wanajeshi wa Korea Kaskazini huko Kursk.+++ Waliofariki katika moto wa nyika California wafikia 16.
Matagazo ya Jioni 11.01.2025
Ukraine imekuwa ikiwahoji wanajeshi wawili wa Korea Kaskazini+++++Kisiwa cha Mayotte kukabiliwa na kimbunga kipya Jumamosi jioni++++Biden kuongeza muda wa kukaa Marekani kwa wahamiaji wa Venezuela na Sudan++++Ethiopia kufungua soko la hisa ili kuwavutia wawekezaji++++Watu 21 wauawa katika shambulizi la genge nchini Nigeria
Wanajeshi wa Korea Kaskazini wakamatwa na Ukraine
Ukraine imetangaza kuwakamata wanajeshi wawili wa Korea Kaskazini waliokuwa wanapigana upande wa Urusi.
Matangazo ya Dunia Yetu Leo Mchana 11 Januari 2025
Sikiliza Matangazo ya Dunia Yetu Leo Mchana 11 Januari 2025 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW.
11.01.2025 Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aitaka Venezuela kuwaachia huru watu wanaoendelea kuzuiliwa bila kufunguliwa mashitaka. Amri ya kutotembea nje yatangazwa Los Angeles, California kufuatia matukio ya moto mkali. Na Marekani na Uingereza zaiwekea vikwazo vipya Urusi.
10.01.2025 Matagazo ya Jioni
Rais wa Venezuela Nicholas Maduro aapishwa kwa muhula wa tatu wa miaka sita+++ Kremlin imesema Rais Vladimir Putin yuko tayari kufanya mazungumzo na Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, kuvijadili vita vya Urusi nchini Ukraine +++ UN yasema watoto milioni 3 Sudan wanakabiliwa na utapiamlo mkali +++ Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani kuhudhuria Mkutano wa Syria Saudi Arabia.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 20 wa 152
Ukurasa unaofuatia