You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
App
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
27.08.2025 Matangazo ya Jioni
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) leo, Jumatano, imefanya zoezi la uteuzi wa wagombea wa nafasi ya Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania// Kenya inaadhimisha miaka 15 ya katiba mpya//Hatima ya wapi mwili wa Rais wa zamani wa Zambia, Edgar Lungu, utazikwa bado haijulikani.
27.08.2025 Matangazo ya Mchana
Tume huru ya uchaguzi nchini Tanzania (INEC) imekiandikia chama cha upinzani cha ACT Wazalendo kuwa hakitaweza kumteua mgombea wa urais kupitia chama hicho, Luhaga Mpina// Serikali ya Kenya imeanzisha rasmi jopo la wataalamu litakalosimamia fidia kwa waathiriwa wa maandamano na ghasia za umma yaliyoshuhudiwa nchini tangu mwaka 2017
27.08.2025 Matangazo ya Asubuhi
Nchi za Magharibi ambazo ni washirika wakuu wa Kiev, zimekuwa zikijadili uwezekano wa kupelekwa kwa wanajeshi nchini Ukraine// Uhaba wa maji unaotokana na ongezeko la viwango vya joto na ukame duniani huenda ukavuruga mifumo ya uchumi wa mataifa na kusababisha ukosefu wa chakula, uhamiaji na misukosuko ya kisiasa.
27.08.2025 Taarifa ya Habari Asubuhi
Jeshi la Israel lasema shambulizi la hospitali ya Nasser liliilenga kamera ya Hamas // Mazungumzo ya nyuklia yaliyofanyika Geneva yakamilika bila mafanikio // Na Morocco kuvaana na Madagascar katika fainali ya CHAN jijini Nairobi
26.08.2025 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Watu kadhaa wameandamana Jumanne huko Israel wakiishinikiza serikali kumaliza vita vya Gaza na kurejeshwa kwa mateka / Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney ametangaza ubia kati ya Ujerumani na Norway ni mojawapo wa wawaniaji wakuu wa kandarasi ya manowari mpya za Canada
26.08.2025 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Viongozi wa kidini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamewasilisha mpango wa kuanzisha mchakato shirikishi na wa kitaifa wa amani / Rais Xi Jinping wa China ameusifu uhusiano kati ya China na Urusi
26.08.2025 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Israel iliishambulia kwa makombora mojawapo ya hospitali kuu katika Ukanda wa Gaza / Kenya inasherehekea baada ya kufanikiwa kutokomeza ujangili unaolenga faru katika kipindi cha miaka mitano iliyopita
26.08.2025 Taarifa ya Habari Asubuhi
Israel yaishambulia hospitali Gaza na kuuwa watu 20, wakiwemo waandishi habari na waokoaji // Rais Trump wa Marekani akutana na rais mpya wa Korea Kusini katika Ikulu ya White House // Na Botswana yatangaza dharura ya afya ya kitaifa kutokana na uhaba wa dawa
25.08.2025 Matangazo ya Jioni
Israel yatuhumiwa kuwalenga wanahabari huko Gaza+++Warohingya wataka wahakikishiwe usalama kurudi kwao+++Hali ya kibinadamu Sudan yazorota kufuatia mashambulizi ya RSF
Warohingya wataka wahakikishiwe usalama kurudi kwao
Warohingya wanaoishi nchini Bangladesh wamefanya kumbukumbu ya miaka minane tangu walipolazimishwa kuihama Myanmar.
25.08.2025 Matangazo ya Mchana
Wanahabari kadhaa wauawa Gaza kufuatia mashambulizi ya Israel+++Jeshi la Urusi ladai kuteka kijiji kingine cha Ukraine kwenye jimbo la Dnipropetrovsk+++Tanzania- Dirisha la fomu za ubunge kwa wanachama wa CCM lafunguliwa rasmi+++ M23 yaishutumu serikali ya Kongo kwa kutumia mamluki kushambulia ngome zao+++Berlin yabadilisha jina lenye utata wa ubaguzi wa rangi
Jukwaa la manufaa
Yasikie maoni uliyotutumia msikilizaji yakijumuisha kero, ushauri na hata pongezi kuhusu masuala kadha wa kadha yanayoendelea kwenye jamii yako kupitia Jukwaa la Manufaa. Ungana naye Angela Mdungu kwa takriban dakika tisa za kipindi hiki akiyapeperusha hewani maoni yako.
25.08.2025 Matangazo ya Asubuhi
Katika matangazo yetu ya asubuhi hivi leo utasikia makala zetu za Mbiu ya Mnyonge, Mbio ya Munyonge, Mtu na Mazingira, Vijana Tugutuke na Jukwaa la manufaa. Sikiliza ya Dunia Yetu Leo Asubuhi kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW Bonn.
25.08.2025 Taarifa ya Habari Asubuhi
Mashambulizi ya Israel kwenye mji mkuu wa Yemen, Sanaa yauwa watu sita // Rais Zelensky wa Ukraine atoa wito wa mkutano na Rais Putin wa Urusi huku juhudi za amani zikikwama // Na Jeshi la Nigeria lawaokoa watu 76 waliotekwa na genge la majambazi
Matangazo ya Jioni 24.08.2025
Watu kadhaa wauawa Gaza kufuatia mashambulizi ya Israel++++Urusi: Nchi za Ulaya zinalenga "kuzuia" mchakato wa amani++++Jeshi la anga la Nigeria lauua magaidi 35 wa Boko Haram++++Khamenei: Raia wa Iran tuungane dhidi ya mipango ya Marekani.
Matangazo ya Mchana 24.08.2025
Ukraine yaadhimisha miaka 34 ya uhuru wake++++Netanyahu akabiliwa na shinikizo la kumaliza vita huko Gaza+++Sudan: Watu 158 wafariki kwa kipindupindu huko Darfur++++Korea Kaskazini yafanya jaribio la makombora mapya+++++Morocco na nchi zingine 3 zatinga nusu fainali CHAN.
22.08.2025 - Matangazo ya Jioni
Uingereza imeliita janga la njaa kwenye Ukanda wa Gaza kuwa limetengenezwa kwa makusudi+++Mazungumzo kuhusu mkataba wa nyuklia kati ya Iran na mataifa matatu ya Ulaya yataendelea tena Jumanne ijayo+++Joto la soka limepanda timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars wanachuana na Madagascar katika Robo Fainali ya CHAN 2024.
Uingereza, Umoja wa Mataifa wailaumu Israel kwa njaa Gaza
Uingereza imeliita janga la njaa kwenye Ukanda wa Gaza kuwa ni uovu wa kimaadili uliotengenezwa kwa makusudi.
Umoja wa Mataifa waonya athari za joto kali kwa wafanyakazi
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yametaka hatua za haraka zichukuliwe kuwalinda wafanyakazi kote ulimwenguni.
22.08.2025 - Matangazo ya Mchana
Israel inaendeleza mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza+++Uongozi wa Bunge la Taifa nchini Kenya umepuuza matamshi ya Rais William Ruto kuhusu madai ya rushwa bungeni.
Programu inayotumia Akili Mnemba kutafsiri lugha ya alama
Kampuni moja ya nchini Kenya inafanya juhudi za kutafsiri maneno kwenda katika lugha ya alama kwa kutumia picha za kielektroniki zinazofahamika kama Avatar. Ungana na Angela Mdungu katika makala ya Sema Uvume kufahamu zaidi.
Utata kuhusu kura ya mapema Zanzibar
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imesema, kura ya mapema itafanyika kama ilivyo kwenye sheria ya tume hiyo licha ya chama kikuu cha upinzani- ACT Wazalendo kupinga. Mohammed Khelef amezungumza na Ismail Jussa makamu mwenyekiti wa chama hicho kujua ni kwanini wanalipinga hilo.
21.08.2025 - Matangazo ya Jioni
Aliyekuwa Naibu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua amerejea nchini humo baada ya kuwepo katika ziara ya siku 42 nchini Marekani+++Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anaendelea na mpango wa kupanua operesheni ya kijeshi dhidi ya Mji wa Gaza.
21.08.2025 - Matangazo ya Mchana
Mashambulizi mapya ya Urusi dhidi ya Ukraine yamechochea wasiwasi mpya kuhusu mustakabali wa vita vinavyoendelea kwa zaidi ya miaka mitatu+++Rais wa Kenya, William Ruto amepata pigo kwenye mpango wake wa kukabiliana na ufisadi baada ya Mahakama Kuu nchini humo kuahirisha utekelezaji wa agizo lake la kuunda kikosi kazi cha kupambana na ufisadi.
20.08.2025 - Matangazo ya Jioni
Ujerumani yaukemea mpango wa kijeshi wa Israel wa kutaka kuidhibiti Gaza+++Wadau wa amani, haki na demokrasia kutoka kona mbalimbali nchini Tanzania wamekutana nchini humo kwa ajili ya kumulika uchaguzi mkuu ujao.
Je dunia inafanya vya kutosha kulinda uhuru wa kuabudu?
Siku ya kumbukumbu ya waathirika wa ukatili wa kidini ni siku inayowakumbuka wale wote walioteseka, kujeruhiwa au kupoteza maisha kwasababu ya imani zao. Siku hii pia inaibua masuali mazito ya iwapo dunia inafanya juhudi za kutosha kulinda uhuru wa kuabudu. Mbiu ya Myonge inaangazia hilo, mtayarishaji ni Najjat Omar.
Mkataba wa amani Ukraine wanukia?
Maafisa wa ngazi za juu wa kijeshi wa Marekani na Ulaya wamekutana kuzungumzia uwezekano wa mkataba wa amani wa Ukraine.
20.08.2025 - Matangazo ya Mchana
Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz, ameuidhinisha mpango wa kijeshi wa kuuteka mji wa Gaza+++Wabunge nchini Kenya wameonyesha kughadabishwa na madai yaliyotolewa na Rais William Ruto kwamba baadhi yao huchukua hongo kutoka kwa mawaziri na magavana.
Vyanzo: Msimamo wa Israel kuhusu vita haujabadilika
Israel bado haijatoa majibu ya uhakika kuhusu mapendekezo mapya ya kusitisha vita kwenye Ukanda wa Gaza.
19.08.2025 - Matangazo ya Jioni
Mjadala wa kusaka amani ya Ukraine umechukua sura mpya baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza mpango wa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya marais Volodymyr Zelensky na Vladimir Putin+++Leo ni maadhimisho ya siku ya watoa misaada ya kibinadamu duniani huku dunia ikiendelea kushuhudia majanga ya asili na migogoro mbalimbali ya kivita ikiathiri utoaji wa misaada.
Changamoto za vijana kufikia soka ya kulipwa
Katika sabini na saba asilimia tunakuuliza, je, ni changamoto gani zinazowakabili vijana wa mashinani katika azma yao ya kutaka kufikia kiwango cha kuwa wachezaji wa kulipwa? Jacob Safari ameyaangazia hayo na mengi katika Makala ya Vijana Mubashara.
19.08.2025 - Matangazo ya Mchana
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, sasa imepelekwa Mahakama Kuu+++Kundi la Hamas pamoja na makundi mengine ya wapiganaji wa Kipalestina yamekubali pendekezo la kusitisha mapigano lililowasilishwa na Misri na Qatar.
Trump, Zelensky wasifu matokeo ya mkutano wa Washington
Marais Donald Trump na Volodymyr Zelensky wameyasifu matokeo ya mkutano kutafuta suluhu ya vita vya Ukraine.
18.08.2025 Matangazo ya Jioni
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amewasili mjini Washington kwa ajili ya mkutano wake na Rais wa Marekani Donald Trump// Wakati matarayisho ya uchaguzi mkuu nchini Tanzania yakiendelea, Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imesema, kura ya mapema itafanyika kama ilivyo kwenye sheria ya tume hiyo licha ya chama kikuu cha upinzani- ACT Wazalendo kupinga,
Wapinzani wa Urusi wazuiwa viza Ujerumani?
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ujerumani inasema inatekeleza makubaliano ya vyama vinavyounda serikali ya mseto.
18.08.2025 Matangazo ya Mchana
Mamia kwa maelfu ya waandamanaji waliteremka mitaani kwenye mji wa Tel Aviv na maeneo mengine nchini Israel usikuwa kuamkia leo kupaza sauti za kutaka kumalizwa kwa vita vinavyoendelea Ukanda wa Gaza// Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru mashahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili, Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu kufichwa.
Malaki waandamana Israel kutaka vita visitishwe Gaza
Mamia kwa maelfu ya waandamanaji wameandamana nchini Israel kutaka vita vya Gaza visitishwe.
16.08.2025 - Matangazo ya Jioni
Duru ya mwisho ya hatua ya makundi CHAN kuanza Jumamosi++++Viongozi wa Ulaya waunga mkono mkutano wa pande tatu kati ya Putin, Zelensky na Trump++++Waandamanaji mkoani Sweida wataka haki ya kujitawala++++Watu 22 wauawa kutokana na shambulizi la Israel katika ukanda wa Gaza.
16.08.2025 - Matangazo ya Mchana
Trump na Putin hawakufikia makubaliano kuhusu Ukraine+++++Rais wa Ukraine Volodymr Zelensky kukutana na Trump Jumatatu++++ Israel na Sudan Kusini zajadili makazi kwa Wapalestina wa Gaza.+++Zaidi ya watu 300 wafariki dunia katika mafuriko Pakistan.
15.08.2025 - Matangazo ya Jioni
Rais wa Marekani Donald Trump amesema hatajadiliana na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin kwa niaba ya Ukraine+++Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa visa vya unyanyasaji wa kijinsia viliongezeka kwa kiwango cha asilimia 25 mwaka 2024.
15.08.2025 - Matangazo ya Mchana
Rais wa Marekani Donald Trump anakutana na mwenzake wa Urusi Rais Vladimir Putin huko Alaska+++Makubaliano ya rasimu ya mkataba wa kuzuia matumizi ya plastiki yamegonga mwamba baada ya majadiliano ya miaka mitatu kumalazika bila kufikia muafaka.
15.08.2025 - Matangazo ya Asubuhi
Rais wa Marekani Donald Trump na mwanzake wa Urusi Vladmir Putin wanakutana hii leo mjini Alaska+++Pendekezo la kuiwekea vikwazo Israeli kupata sehemu ya fedha za Umoja wa Ulaya kutokana na mzozo wa kiutu katika Ukanda wa Gaza limekwama.
15.08.2025 -Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Rais Putin asifu juhudi za dhati za Marekani za kutaka kumaliza vita vya Ukraine kabla ya kukutana na Trump baadae leo///Ujerumani yakataa mipango ya Israel ya ujenzi wa makazi Ukingo wa Magharibi///Mazungumzo ya UN kuhusu mkataba wa plastiki yarefushwa.
14.08.2025 - Matangazo ya Jioni
Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi na Jerusalem wameikataa mipango iliyotangazwa leo na Waziri wa Fedha wa Israel, Bezalel Smotrich+++Umoja wa Afrika umepinga matumizi ya ramani iliyopo kwa madai inapotosha kuhusu ukubwa wa bara la Afrika.
14.08.2025 - Matangazo ya Mchana
hirika la habari la Kipalestina, WAFA, limetangaza kuwa Wapalestina wapatao 89 wameuawa katika mashambulizi mbalimbali ya Israel katika Ukanda wa Gaza+++Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) imesema takriban watu 40 wamefariki katika jimbo la Darfur kutokana na mlipuko mbaya zaidi wa kipindupindu.
14.08.2025 - Matangazo ya Asubuhi
Rais Donald Trump wa Marekani anaonekana kulainisha msimamo wake dhidi ya China, wakati akizikaba koo India na Brazil+++Idadi ya watoto wanaozaliwa nchini Kenya imepungua ikilinganishwa na muongo mmoja uliopita.
13.08.2025 Matangazo ya Jioni
Kiongozi wa chama cha upinzani cha DCP, Rigathi Gachagua anakabiliwa na hatari ya kukamatwa kuhusu kauli alizozitoa akiwa ziarani Marekani// Wizara ya Afya nchini Afrika Kusini hatimaye imezungumza na kukemea vikali wanachama wa vuguvugu la Operation Dudula kwa kuendesha kampeni ya kuwazuia raia wa kigeni wanaoishi nchini humo kupata huduma za afya katika hospitali za umma.
13.08.2025 Matangazo ya Mchana
Mkuu wa Majeshi ya Israel, Luteni Jenerali Eyal Zamir, ameidhinisha mpango wa mashambulizi katika Ukanda wa Gaza// Chama kinachotawala nchini Tanzania, CCM chafanya harambee kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba// Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekiri makosa ya nchi yake katika makoloni yake kabla wakati na baada ya uhuru wa mataifa hayo ikiwemo Cameroon na Senegal.
13.08.2025 Matangazo ya Asubuhi
Upinzani wa umma dhidi ya kampeni ya kijeshi ya serikali ya Israel huko Gaza unaongezeka//Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuliweka Jeshi la Polisi la jiji la Washington, D.C., chini ya udhibiti wa serikali kuu//Shirika la Kijamii la Royal Foundation nchini Uganda limeanzisha mpango wa mazoezi ya kijamii kwa kundi la wananwake wazee kwa lengo la kuimarisha afya zao.
13.08.2025: Taarifa ya Habari za Asubuhi
Israel yaendelea kushambulia Gaza, huku juhudi za kusaka amani zikiendelea. Trump na Putin kukutana Ijumaa katika mji wa Anchorage huko Alaska. Marekani yaliwekea vikwazo kundi lenye silaha la Pareco-FF mashariki mwa DRC
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 2 wa 152
Ukurasa unaofuatia