You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
App
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
21.02.2025 Matangazo ya Mchana
Hali ya wasiwasi inaonekana kutanda mjini Kinshasa, wakongomani wanaozungumza kiswahili mjini humo, baadhi yao wakidhaniwa kuwa ni waasi+++Waziri Mkuu wa israel Benjamin Netanyahu ameapa kwamba Hamas italipa kwa kushindwa kuutoa mwili wa mateka Shiri Bibas kama ilivyokubaliwa.
21.02.2025 Taarifa ya Habari Asubuhi
China yasema inaunga mkono 'makubaliano ya hivi karibuni' yaliyofikiwa na Marekani na Urusi kuhusu vita vya Ukraine // Waziri Mkuu wa israel Benjamin Netanyahu aagiza operesheni kali dhidi ya vituo vya kigaidi kwenye Ukingo wa Magharibi // Vyama vya siasa vya Ujerumani vyakabiliana kwa mara ya mwisho kwenye mdahalo kuelekea uchaguzi
21.02.2025 Matangazo ya Asubuhi
Mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka Kundi la mataifa tajiri na yanayoinukia kiuchumi duniani la G20, wanakutana kwa siku ya pili leo mjini Johannesburg+++Serikali mpya ya Ujerumani inakabiliwa na changamoto kubwa za sera ya nje baada ya uchaguzi wa mwishoni mwa wiki hii.
Hamas wakosolewa kuhusu miili ya mateka wa Israel
Vongozi wa nchi za Kiarabu watakutana Riyadh kujadili mpango wa kuujenga upya Ukanda wa Gaza.
20.02.2025 Matangazo ya Jioni
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, amesisitiza kuwa migogoro inayoendelea ulimwenguni inazidi kuathiri maisha ya binadamu na kuongeza hatari ya usalama duniani+++Burundi inakabiliwa na wimbi kubwa zaidi la wakimbizi huku maelfu wakikimbia mgogoro unaozidi kuongezeka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
20.02.2025 Matangazo ya Mchana
Urusi na Marekani zinajadili uwezekano wa uchaguzi wa Ukraine. Haya yanajiri huku mzozo wa Ukraine na Urusi ukionekana kuchukua mkondo tofauti kufuatia mazungumzo yaliyofanywa kati ya wanadiplomasia wa Marekani na Urusi mjini Riyadh+++Wizara ya mambo ya nje ya Kenya, imesema kuwa iko tayari kuunga mkono juhudi za kutafuta amani nchini Sudan.
Hamas yakabidhi miili 4 ya mateka wa Israel
Shughuli hii imefanyika chini ya uangalizi wa Shirika la Msalaba Mwekundu.
20.02.2025 - Matangazo ya Asubuhi
Wakaazi wa kambi ya wakimbizi inayokumbwa na njaa iitwayo Zamzam ya nchini Sudan inayokumbwa na njaa wanarejea katika eneo la al-Fashir+++Friedrich Merz ni mpinzani mkuu wa Kansela wa SPD na kwa sasa anachukuliwa kuwa mgombea mwenye nafasi kubwa zaidi ya kushinda.
20.02.2025: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Ungana nasi hapa kusikiliza taarifa ya habari ya leo asubuhi.
19.02.2025 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu amemwambia waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani kuwa nchi yake inalipinga pendekezo la kuwahamisha Wapalestina kutoka Gaza / Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemshutumu Rais Donald Trump kwa kushawishiwa na kile alichokiita "habari potofu" za Urusi
19.02.2025 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Kiongozi wa Kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis, ambaye amegundulika kuwa na nimonia kwenye mapafu yake mawili / Sudan inamshutumu Rais William Ruto wa Kenya kwa kukiuka ahadi katika ngazi ya juu kabisa, ikidai kuwa Kenya iliruhusu mazungumzo ya kuanzisha serikali sambamba kuendelea licha ya kuhakikisha vinginevyo
19.02.2025 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Maafisa wa ngazi za juu wa Marekani na Urusi walikutana kwa takriban masaa manne katika kasri la Diriyah mjini Riyadh, Saudi Arabia / Ripoti ya Shirika la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch imesema vikwazo vikali vilivyowekwa na Marekani, Umoja wa Ulaya, Uingereza na nchi nyingine vinazuia kurejeshwa kwa huduma muhimu nchini Syria
19.02.2025: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Marekani na Urusi zaafikiana kwenye mazungumzo ya Riyadh kuanzisha rasmi mchakato wa amani katika mzozo wa Ukraine. Waasi wa M23 waelekea katika miji ya Butembo na Kamanyola, huku Burundi ikikanusha kuwaondoa wanajeshi wake mashariki mwa Kongo. Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro ashtakiwa kwa jaribio la mapinduzi na kutaka kumuua rais Lula da Silva.
18.02.2025 Matangazo ya Jioni
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, amesema kumaliza vita vya Urusi dhidi ya Ukraine kutahitaji pande zote kufanya maridhiano+++Umoja wa Mataifa umeonya kwamba hali mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inazidi kuzorota kwa kasi, na kusababisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
18.02.2025 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Raia wa Israel wameadhimisha siku 500 za vita Gaza kwa kufanya maandamano ya kudai hatua zaidi za usitishaji mapigano / Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waasi wa M23 wanaendelea kusonga mbele katika jimbo la Kivu kusini, ambapo wameuteka mji wa Bukavu
18.02.2025 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Mzozo unaoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umezusha hofu ya vita vya kikanda / Mzozo unaoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
18.02.2025: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Viongozi wa Ulaya wakutana mjini Paris kwa mazungumzo kuhusu usalama wao. Umoja wa Mataifa wahitaji msaada wa dola bilioni 6 ili kuisaidia Sudan mwaka huu wa 2025. Israel kuanzisha shirika maalum la kuwawezesha Wapalestina kuondoka Gaza kwa hiari yao.
17.02.2025 Matangazo ya Jioni
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema usalama wa Ulaya uko katika mabadiliko muhimu//Mjadala unashika kasi kuhusu suala la ujenzi mpya wa Ukanda wa Gaza//Raia wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo wapatao elfu 10 wamevuka mpaka na kuingia kuomba hifadhi nchini Burundi.
17.02.2025 Matangazo ya Mchana
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakutana leo Jumatatu kwa ajili ya mkutano maalumu wa dharura// Waasi wa M23 waingia mjini Bukavu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo// Wagombea wakuu wanne wa ukansela nchini Ujerumani Friedrich Merz, Olaf Scholz, Robert Habeck, na Alice Weidel, wamefanya mdahalo wa moja kwa moja wa televisheni jana Jumapili.
17.02.2025 Matangazo ya Asubuhi
Katika matangazo yetu ya asubuhi hivi leo utasikia makala zetu za Mbiu ya Mnyonge, Makala yetu Leo, Mtu na Mazingira, Vijana Tugutuke na Jukwaa la manufaa. Sikiliza ya Dunia Yetu Leo Asubuhi kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW Bonn.
Taarifa ya Habari ya Asubuhi: 17.02.2025
Marekani yatangaza kuwa mataifa ya Ulaya yatajumuishwa kwenye mazungumzo ya amani kuhusu mzozo wa Ukraine. Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yathibitisha kuwa M23 imechukua udhibiti wa mji wa Bukavu. Silaha nzito zilizotolewa na Marekani zawasili Israel.
Matangazo ya JionI: 16.02.2025
Umoja wa Afrika waonya dhidi ya kugawika kwa taifa la Kongo. Israel yasema itaishambulia vikali Gaza iwapo mateka wake wote hawatoachiliwa na Hamas. Viongozi wa Ulaya wakutana Paris kujadili usalama wa Ukraine
Matangazo ya Mchana: 16.02.2025
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amehimiza umuhimu wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuepushwa na vita vya kimaeneo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, amewasili mjini Jerusalem kukutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Mkutano wa usalama wa mjini Munich waingia siku yake ya mwisho
Matangazo ya Mchana: 15.02.2025
Waasi wa M23 waingia mjini Bukavu. Guterres atoa wito wa amani katika mzozo wa Mashariki mwa Kongo. Kansela Scholz ahutubia mkutano wa kimataifa wa usalama wa Munich.
Makala ya Afrika Wiki Hii
Mzozo wa Mashariki mwa Kongo unaendelea kufukuta. Mkutano wa viongozi wa Afrika wafanyika Addis Ababa Ethiopia, ajenda kuu ni mzozo wa DRC, lakini nafasi ya kufanikiwa juhudi za kidiplomasia za kuutatua mzozo huo ni ndogo, je ni kwanini? Kwa haya na mengine mengi sikiliza Afrika wiki hii na Amina Abubakar.
14.02.2025 Matangazo ya Jioni
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR limeelezea wasiwasi wake kuhusu hali inayozidi kuwa mbaya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, likisema, likisema vita katika eneo hilo limewaacha takriban watu 350,000 bila makazi+++Jumuiya ya kimataifa imeapa kuwa itaiunga mkono Syria
14.02.2025 Matangazo ya Mchana
Bunge la Ulaya limeutaka Umoja wa Ulaya kusitisha kuiunga mkono moja kwa moja bajeti ya umoja huo kwa Rwanda hadi nchi hiyo itakapovunja uhusiano wake na waasi wa kundi la M23+++Viongozi mashuhuri wa kisiasa, wanadiplomasia, na wataalamu wa usalama wanakutana leo Ijumaa kwenye Mkutano wa Usalama wa Munich.
Mzozo wa Kongo kutawala mkutano wa kilele wa AU
Mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Afrika, AU kutawaliwa na mzozo wa Kongo na uchaguzi wa viongozi wapya.
13.02.2025 Matangazo ya Jioni
Kundi la Hamas limesema kuwa litawaachilia mateka wengine Jumamosi kama ilivyokuwa imepangwa+++Watu wasiopungua 28 wamejeruhiwa, baadhi yao vibaya, baada ya gari dogo aina ya Mini Cooper kuwagonga waandamanaji katikati mwa jiji la Munich.
13.02.2025 Matangazo ya Mchana
Ujumbe wa Maaskofu wa Kanisa katoliki na wale wa Kiprotestanti katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, umekutana na waasi wa M23 katika juhudi za kutafuta amani+++Serikali ya Ujerumani na Tanzania kwa pamoja zimezindua wiki ya ubinifu wa Teknolojia ya Kijani.
Wapatanishi wapambana kunusuru makubaliano ya Gaza
Wapatanishi wanajaribu kuyaokoa makubaliano legelege ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Kundi la Hamas.
12.02.2025 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Mkutano wa kilele uliokuwa ukijadili teknolojia ya akili mnemba (AI) umekamilika nchini Ufaransa / Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth amesema Marekani haitopeleka wanajeshi wake Ukraine chini ya mkataba wowote wa amani
Vijana wanavutiwa na uhuru wakiwa kazini
Maendeleo ya teknolojia yamewapa vijana nafasi kubwa ya kufanyakazi katika mazingira huru, huku ofisi nyingi zikivutiwa na mtindo huo kutokana na kupunguza gharama za uendeshaji ofisi. Katika makala ya Vijana Mchakamchaka hilo ndio vijana wanajadili linafaida kwao?
DeepSeek Akili Mnemba iliyoteka soko la teknolojia
DeepSeek imeleta mapinduzi katika mukhtadha wa teknolojia ya Akili Mnemba kutokana na namna ambavyo inachakata taarifa zake, lakini upo wasiwasi wa namna inachakata data zake, wataalamu wanaonya kuwa inaweza kutumiwa vibaya katika kutoa taarifa.
Matetemeko ya ardhi yasababisha hofu nchini Ugiriki
Tangu mwanzoni mwa mwezi Februari kumeshuhudiwa mkururo wa matetemeko ya ardhi nchini Ugiriki hasa katika kiswa cha Santorini na kuzusha hofu kulipuka kwa volkano katika siku za usoni. Makala ya Mwanza wa Ulaya inatuama hapo nahodha ni Bakari Ubena
12.02.2025 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Kutokana na mzozo unaoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, serikali ya kinshasa imepiga marufuku ndege zote zilizosajiliwa nchini Rwanda kutumia anga yake / Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema yuko tayari kubadilishana ardhi katika mazungumzo na Urusi
12.02.2025 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Rais wa Marekani Donald Trump amekutana na Mfalme Abdullah wa Jordan katika Ikulu ya White House / Sekta ya afya nchini Burundi inakabiliwa na changamoto
Mwangaza wa Ulaya: Matetemeko ya ardhi kisiwani Santorini
Tangu Februari 1,2025, mamia ya matetemeko ya ardhi yamekuwa yakishuhudiwa katika kisiwa cha Santorini nchini Ugiriki, na hivyo kuzusha hofu miongoni mwa wananchi kuwa huenda hali hiyo inaashiria uwezekano wa tetemeko kubwa zaidi na hata mripuko wa volkano kama ilivyotokea miongo sita iliyopita. Matetemeko hayo ya ardhi huko Santorini yamepelekea maelfu ya watu kulazimika kuyahama makazi yao.
11.02.2025 Matangazo ya Jioni
Muda wa saa 72 uliotolewa na waasi wa M23 kwa wakimbizi wa kivita walioko katika kambi za magharibi mwa mji wa Goma kama Bulengo na Lushagala, unafikia mwisho hii leo+++Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance amewaonya viongozi wa dunia na watendaji wa sekta ya teknolojia dhidi ya udhibiti mkali wa Akili Mnemba.
11.02.2025 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Rais Donald Trump wa Marekani atakutana leo na Mfalme Abdullah II wa Jordan Washington kwa mazungumzo yanayotizamiwa kuwa magumu, kufuatia pendekezo la Trump la kutaka kulichukua eneo la Ukanda wa Gaza / Ripoti ya Shirika la Transparency International imeonya kwamba rushwa inatishia juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
11.02.2025 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Umoja wa Ulaya unajitahidi kuonyesha kuwa uko huru kiuchumi bila kuitegemea Marekani / Viongozi nchini Kenya wameendelea kutofautiana kufuatia hatua ya Rais William Ruto ya kufutilia mbali mchakato wa kuwachunguza kwa undani vijana kutoka kwenye maeneo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo kabla ya kupewa vitambulisho vya taifa.
Taarifa ya habari ya asubuhi 11.02.2025
Muhtasari: Rais Trump asema makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas yanapaswa kufutwa, ikiwa mateka wote hawatoachiwa +++ Rais Zelensky kukutana na Makamu wa Rais wa Marekani mjini Munich +++ Chama cha DA ambacho ni mshirika katika serikali ya umoja ya Afrika Kusini, chaipinga sheria ya kusimamia umiliki wa ardhi.
10.02.2025 Matangazo ya Jioni
Viongozi wa nchi na wadau wengine wanakutana leo na kesho mjini Paris kwenye mkutano wa kilele unaojadili fursa na vitisho vya teknolojia inayokua kwa kasi ya akili mnemba//Mawaziri na maafisa wa ngazi za juu kutoka mataifa 11 ya Mashariki na Pembe ya Afrika wanazingatia kusawazisha sera zao za 'uhamiaji kwa ajili ya ajira' ili kuweza kuzishughulikia changamoto za kuwaingiza watu kinyemela.
10.02.2025 Matangazo ya Mchana
Hali ya utulivu yashuhudiwa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwishoni mwa juma katika maeneo ya mapigano wilayani Kalehe ndani ya jimbo la Kivu kusini// Kiongozi wa kundi la Hamas amesema hivi leo kuwa watakabiliana na mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kuchukua udhibiti wa Gaza na kuwahamisha Wapalestina.
Taarifa ya habari ya asubuhi 10.02.2025
Muhtasari: +++Rais wa Marekani Donald Trump asema Washington, inapiga hatua katika mazungumzo yake ya kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine+++Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na mpinzani wake mkuu Friedrich Merz wachuana vikali katika mdahalo kuelekea uchaguzi +++Wanajeshi wapatao 75 wa Kongo watapandishwa kizimbani leo, kwa kukimbia mapigano baada ya waasi wa M23 kusonga mbele+++
Sudan: Jeshi lakomboa sehemu kubwa ya jiji la Khartoum
Sudan: Jeshi lakomboa sehemu kubwa ya jiji la Khartoum
Misri kuandaa mkutano wa kilele wa dharura kuhusu Gaza
Misri kuandaa mkutano wa kilele wa dharura kuhusu Gaza
Mtu mmoja amekufa katika maporomoko ya ardhi China
Mtu mmoja amekufa katika maporomoko ya ardhi China
Wanajeshi wa Israel waondoka kutoka kwenye eneo la Netzarim
Wanajeshi wa Israel waondoka kutoka kwenye eneo la Netzarim
IMF: Mageuzi ya kiuchumi kuinufaisha Ethiopia pakubwa
IMF: Mageuzi ya kiuchumi kuinufaisha Ethiopia pakubwa
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 18 wa 152
Ukurasa unaofuatia