You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
App
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
16.03.2025: Matangazo ya Jioni
Zelensky aituhumu Urusi kwa kutoonyesha nia ya kuvimaliza vita. Huko Macedonia, idadi ya watu waliofariki kutokana na moto uliotokea katika klabu ya usiku imefikia watu 59. Maelfu ya watu waandamana nchini Mexico kuwakumbuka waliopotea.
16.03.2025: Matangazo ya Mchana
Trump aamuru kufungwa kwa muda kituo cha habari cha Sauti ya Amerika VOA. Angola yatoa wito wa kusitisha mapigano mashariki mwa Kongo. Mashambulizi ya Marekani huko Yemen yaua watu 31.
Matangazo ya Jioni: 15.03.2025
Keir Starmer asema Putin hana budi kuketi kwenye meza ya mazungumzo. Watu 9 wauwawa katika shambulio lililofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza. HRW yahusisha makundi yanayoiunga mkono serikali na mauaji magharibi mwa Burkina Faso. Raia wa nchi 43 kupigwa Marufuku kuingia Marekani. Ujerumani yaweka hadharani rasimu ya mpango mpya wa matumizi ya fedha
Raia wa nchi 43 kupigwa Marufuku kusafiri Marekani
Utawala wa Rais Donald Trump umependekeza marufuku mpya ya kusafiri itakaowaathiri watu kutoka mataifa 43.
Meza ya Duara: Je, Raila ni bingwa wa miafaka au msaliti?
Mwanasiasa mashuhuri wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, ameingia kwenye muafaka mwengine wa kisiasa na mahasimu wake. Safari hii ikiwa ya nne, amesaini muafaka na Rais William Ruto, baada ya huko nyuma kuingia kwenye miafaka kama hiyo na Rais Daniel arap Moi, Rais Mwai Kibaki na Rais Uhuru Kenyatta.
A.Kusini yafadhaishwa balozi wake kufukuzwa Marekani
Ofisi ya Rais Cyril Ramaphosa imesema imesikitishwa na uamuzi wa Marekani wa kumfukuza balozi wa Afrika Kusini.
Matangazo ya Mchana 15.03.2025
Afrika Kusini yasikitishwa na kufukuzwa kwa balozi wake kutoka nchini Marekani. Katibu Mkuu wa UN asema kuna ongezeko kubwa la Chuki dhidi ya Uislamu. Mashambulizi ya droni yatikisa Ukraine na Urusi usiku kucha. Kundi la G7 lataka mateka waachiliwe, misaada ipelekwe Gaza
Guterres: Kuna ongezeko kubwa la chuki dhidi ya Uislamu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuna ongezeko kubwa la ubaguzi dhidi ya Uislamu kote duniani.
Nchi za G7 zataka mateka waachiliwe, misaada iingie Gaza
Kundi la mataifa 7 yaliostawi zaidi kiviwanda la G7 limetoa wito wa uachiliwa kwa mateka wote wanaoshikiliwa na Hamas.
Mashambulizi ya droni yarindima tena Ukraine na Urusi
Ukraine limesema limezidungua droni 130 kati ya 178 za Urusi wakati Moscow ikiripoti kuwa meziangusha droni 126 za Kyiv.
14.03.2025 Matangazo ya Jioni
Maafisa nchini Sudan wamesema hawakubaliani na mapendekezo ya Marekani kuhusu kuwapokea wakimbizi kutoka Ukanda wa Gaza+++Serikali ya kijeshi ya Sudan jana Alhamisi ilitangaza kupiga marufuku bidhaa zote kutoka Kenya kutokana na kile kinachoonekana kuwaunga mkono wanamgambo wa RSF.
Sudan, Somaliland zaukana mpango wa kuwapokea Wapalestina
Maafisa nchini Sudan wamesema hawakubaliani na mapendekezo ya Marekani kuhusu kuwapokea wakimbizi kutoka Ukanda wa Gaza.
Afrika katika magazeti ya Ujerumani
Magazeti ya Ujerumani mnamo wiki hii yamezingatia juu ya wasiwasi wa kuzuka tena vita huko Sudan Kusini. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yachukua hatua kwa ajili ya kulinda bei ya madini yake ya Kobalt. Na hatari ya kuzuka vita vingine nchini Ethiopia
14.03.2025 Matangazo ya Mchana
Rais Vladmir Putin amesema Urusi imekubali mapendekezo ya Marekani ya kusitisha vita+++Kuna hofu huenda mahasimu wa muda mrefu Ethiopia na Eritrea wanaweza kuingia kwenye vita+++Wanasiasa kadhaa wa upinzani kutoka Tanzania walizuiliwa jana kuingia Angola.
14.03.2025 Matangazo ya Asubuhi
Wabunge wanaomaliza muda wao nchini Ujerumani wamefanya kikao maalum kujadili mpango wa euro bilioni 500 katika kushughulikia miundombinu na mabadiliko makubwa katika sheria za kukopa+++Umoja wa Mataifa umezindua mpango utakaouwezesha kufanya shughuli zake kwa ufanisi wakati huu unapokabiliwa na upungufu wa fedha
Bunge la Ujerumani lajadili ukomo wa deni la taifa
Merz alisema Ujerumani lazima ikope mabilioni ya fedha kufadhili ulinzi na miundombinu na lazima iwe tayari kujilinda.
13.03.2025 Matangazo ya Jioni
Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC imechukua uamuzi wa kusitisha uwepo wa kikosi chake huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo+++Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa Afrika (Africa CDC) kimesema kinafanya uchunguzi wa kina ili kubaini kiwango cha maambukizi ya homa ya nyani (MPOX)
13.03.2025 Matangazo ya Mchana
Mazungumzo ya usitishwaji mapigano Ukraine yamepiga hatua, huku ujumbe wa Marekani ukielekea Moscow na NATO ikijadili uwezekano wa vikosi vya amani iwapo mkataba utaafikiwa+++Mamlaka mpya ya Syria imetangaza kwamba inaunda Baraza la Usalama wa Kitafa litakaloongozwa na Rais wa mpito wa nchi hiyo Ahmed al-Sharaa
Mgomo mkubwa wa viwanja vya ndege waendelea Ujerumani
Viwanja 13 vikiwemo vikubwa vya ndege vimelazimika kufuta maelfu ya safari za ndege za ndani na za kimataifa.
Msimamo wa CHADEMA 'No Reforms, No Elections'
Wakati Tanzania ikijipanga kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, upinzani kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki umegawika baina ya wale wanaotaka kuingia kwenye uchaguzi na wale wanaosema bila ya kufanyiwa marekebisho mfumo na mwenendo mzima wa uchaguzi, basi hakupaswi kuwepo kabisa kwa uchaguzi wenyewe. Ansbert Ngurumo ni mwandishi, mchambuzi na kada wa chama cha CHADEMA.
13.03.2025 Matangazo ya Asubuhi
Syria imeshuhudia vita vibaya zaidi tangu kuanguka kwa utawala wa kidikteta+++Rais wa Ghana John Mahama anakabiliwa na shinikizo kutoka Shirika la Fedha Ulimwenguni IMF la kupunguza matumizi ya serikali
13.03.2025 Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Raisi Vladimir Putin wa Urusi aagiza jeshi lake livifurushe vikosi vya Ukraine kutoka ardhi ya Urusi. Marekani yalihimiza baraza la usalama liilaani Iran kuhusiana na mpango wake wa nyuklia. Na mazungumzo ya kutafuta amani ya Congo kufanyika Luanda wiki ijayo.
12.03.2025 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Ukraine imefanya mazungumzo ya amani na Marekani baada ya zaidi ya miaka mitatu ya vita kati yake na jirani yake Urusi / Wanasayansi wanasema: "Kuvuta hewa chafu kwa muda mrefu kunasababisha magonjwa."
11.03.2025 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Rais wa zamani wa Ufilipino Rodrigo Duterte atapelekwa Mahakama ya ICC baada ya kukamatwa / Ukraine imesema mazungumzo na Marekani nchini Saudi Arabia yameanza kwa mwelekeo mzuri hii leo
11.03.2025 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Syria chini ya rais wa mpito Ahmed al-Sharaa imeyavunja makundi yenye silaha na kuwezesha udhibiti wa serikali / Ripoti iliyotolewa siku ya Jumanne na shirika linalofuatilia takwimu za uchafuzi wa hewa, imeeleza kuwa idadi kubwa ya watu duniani huvuta hewa chafu na hivyo kuwa hatarini kupata magonjwa makubwa
11.03.2025 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewasili Saudi Arabia kwa mazungumzo juu ya uwezekano wa makubaliano ya amani kati ya nchi yake na Urusi, ambayo iliivamia zaidi ya miaka mitatu iliyopita / Mahakama ya Rufaa Kenya imesimamisha mpango wa serikali wa kuagiza vyakula vilivyobadilishwa vinasaba.
10.03.2025 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Ukraine inatazamiwa kupendekeza usitishaji mapigano ya anga na majini na Urusi katika mazungumzo yake na maafisa wa Marekani wanaokutana kesho nchini Saudi Arabia / Mahakama ya Rufaa Kenya imesimamisha mpango wa serikali wa kuagiza vyakula vilivyobadilishwa vinasaba
10.03.2025 Matangazo ya Asubuhi
Katika matangazo yetu ya asubuhi hivi leo utasikia makala zetu za Mbiu ya Mnyonge, Makala yetu Leo, Mtu na Mazingira, Vijana Tugutuke na Jukwaa la manufaa
Matangazo ya Jioni 09.03.2025
Sikiliza Matangazo ya Dunia Yetu Leo Jioni 09 Machi 2025 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW.
Matangazo ya Jioni: 08.03.2025
Kongo yatangaza dau kwa watakaofanikisha kukamatwa kwa viongozi wa M23. Mataifa manne ya Ulaya yaunga mkono mpango wa kuijenga upya Gaza. Rais wa Ukraine atoa mwito wa Urusi kuwekewa vikwazo zaidi. Sudan yaipeleka UAE kwenye Mahakama ya Haki (ICJ) kwa kuhusika na mauaji ya halaiki
Matangazo ya Mchana: 08.03.2025
Zaidi ya watu 300 wa jamii ya Waalawi wameuawa na vikosi vya utawala mpya wa Syria. Kundi la Wazalendo lawaua watu 35 mashariki mwa Kongo. Watu 12 wameuawa kwenye shambulio la Urusi, mashariki mwa Ukraine. Mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba yaingiwa na kiwingu
Kiongozi wa Syria awataka Waalawi kuweka chini silaha
Kiongozi wa Syria, Ahmed al-Sharaa amewataka wapiganaji wa kikabila kuweka chini silaha au wataandamwa na mkono wa dola.
07.03.2025 Matangazo ya Jioni
Ujumbe wa ngazi ya juu wa kundi la wanamgambo la Hamas umewasili mjini Cairo ili kuendeleza juhudi za makubaliano yanayosuasua ya kusitisha mapigano huko Gaza+++Rais William Ruto wa Kenya na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga wameweka rasmi saini kwenye mkataba wa kisiasa, ishara ya azma yao ya kufanya kazi pamoja
07.03.2025 Matangazo ya Mchana
Viongozi wapya wa Syria wameanzisha operesheni kubwa ya usalama baada ya zaidi ya watu 70 kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mapigano yaliyotokea nchini humo+++Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Patrick Muyaya amesema Congo inapambana na Rwanda katika maeneo tofauti na kwamba inatafuta haki kwa haraka.
Viongozi wa Ulaya waridhia kuongeza matumizi ya ulinzi
Viongozi wa nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya walikutana jana jioni mjini Brussels, Ubelgiji kujadili hatma ya ulinzi.
06.03.2025 Matangazo ya Jioni
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanashiriki katika mkutano wa dharura mjini Brussels+++Miaka 30 tangu viongozi wa dunia walipopitisha mpango wa kihistoria wa kufanikisha usawa wa kijinsia, ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inaonyesha kuwa haki za wanawake na wasichana ziko katika hatari kubwa.
06.03.2025 - Matangazo ya Mchana
Rais wa Marekani Donald Trump ametoa onyo kali kwa kundi la Hamas akitishia kwamba kutakuwa na uharibifu mkubwa zaidi kwenye Ukanda wa Gaza+++Shirika la haki za binaadamu la Amnesty International limetowa wito wa kuandikwa mkataba wa kimataifa ambao utaratibu utengenezaji wa vifaa vya umeme vinavyotumika kwa ajili ya utesaji.
Amnesty International yataka udhibiti 'vifaa vya shoti'
Amnesty International imetaka mkataba wa kimataifa kuratibu vifaa vya umeme vinavyotumika kwenye utesaji.
Macron: Enzi ya ´unyonge wa Ulaya´ imekwisha
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ameitaja Urusi kuwa "kitisho kwa Ufaransa na Ulaya".
05.03.2025 Matangazo ya Jioni
Wanajeshi wa Sudan Kusini wamewakamata waziri wa mafuta na naibu mkuu wa majeshi, wote wakiwa washirika wa Makamu wa Rais Riek Machar// Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, amezungumza na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na kwa pamoja wamekubaliana kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump ana jukumu muhimu la kutekeleza katika mazungumzo yoyote ya amani kati ya Ukraine na Urusi.
05.03.2025 Matangazo ya Mchana
Viongozi wa mataifa ya Kiarabu waliokutana mjini Cairo wameidhinisha pendekezo linalopinga lile la Rais wa Marekani Donald Trump la kuwahamisha Wapalestina wa Gaza na kuugeuza ukanda huo kuwa eneo la kitalii// Wakristo kote duniani leo wameanza kipindi cha mfungo wa siku 40 kijulikanacho kama “Kwaresma” ambapo wanatafakari mateso na kifo cha Yesu Kristo Msalabani.
05.03. 2025 Matangazo ya Asubuhi
Rais wa Marekani Donald Trump amelihutubia Bunge la Marekani// Wizara ya usalama wa ndani nchini Kenya imeweka marufuku ya kutoka nje katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma kufuatia hali tete inayoshuhudiwa kambini humo//Wakaazi wa mji wa Kampala wameingiwa na mashaka kufuatia kushamiri kwa kunguni katika magari ya abiria maarufu kama matatu au teksi.
05.03.2025 Taarifa ya Habari Asubuhi
Rais Trump alihutubia Bunge na kusema ndoto ya Marekani haizuiliki // Mataifa ya Kiarabu yapitisha pendekezo la Misri kuhusu ujenzi mpya wa Gaza // Na Vyama vya CDU na SPD nchini Ujerumani vyakubaliana juu ya mpango mkubwa wa kifedha
04.03.2025 Matangazo ya Jioni
Misri imependekeza mpango wa kuujenga upya Ukanda wa Gaza utakaogharimu dola za Kimarekani bilioni 53 kwa kipindi cha miaka mitano+++Maelfu ya wakimbizi wa ndani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, waliokuwa wamepata hifadhi huko Goma wanalazimika kurejea makwao, mara nyingi katika hali ngumu.
Ukraine yasema inao uwezo wa kuendelea kupambana na Urusi
Ukraine imesema inaweza kuendelea na mapambano dhidi Urusi hata baada ya Marekani kusitisha kwa muda msaada wa kijeshi.
04.03.2025 Matangazo ya Mchana
Marekani imetangaza kusitisha kwa muda msaada wake wa kijeshi wa Ukraine+++Viongozi wa mataifa ya Kiarabu wanakutana mjini Kairo, Misri+++Wakenya na viongozi wa nchi wanaendelea kukosoa mapungufu ya Bima ya Umma ya Afya ya SHA
04.03.2025 Matangazo ya Asubuhi
Mkutano wa dharura wa Umoja wa nchi za Kiarabu unafanyika leo Cairo nchini Misri ili kujadili mchakato wa kuijenga upya Gaza+++Serikali ya Kenya inaendelea na mazungumzo na Serikali ya Thailand ili kufungua tena mpaka wa Thailand na Myanmar.
04.03.2025 Taarifa ya Habari Asubuhi
Rais Trump wa Marekani asitisha msaada wa kijeshi kwa Ukraine baada ya makabiliano na rais Zelensky // Watu wawili wauawa baada ya gari kuvurumishwa kwenye umati wa watu Ujerumani // Na waasi wawateka wagonjwa 130 mashariki mwa Kongo
03.03.2025 Matangazo ya Jioni
Wapalestina wawili wameuwawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel katika eneo la Rafah+++Nchini Guinea Bissau,wasiwasi wa kisiasa unaongezeka kufuatia mvutano wa kisiasa +++Tangu makundi ya AFC/M23 yalipouteka mji wa Goma, mfumo wa elimu nchini DRC umeyumba.
03.03.2025 Matangazo ya Mchana
Viongozi wa Ulaya waliokutana jana katika mkutano wao wa kilele huko Uingereza, wamesema wataendelea kuiunga mkono Ukraine+++Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limekanusha juu ya kukamatwa kwa wapiganaji 20 wanaohusishwa na mauaji ya kimbari ya Rwanda kwenye ardhi yake.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 16 wa 152
Ukurasa unaofuatia