You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
App
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
15.04.2025 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Mgogoro kati ya majenerali wawili umeitumbukiza Sudan katika vita ambavyo havionekani kumalizika hivi karibuni / Umoja wa Afrika umemteua Faure Gnassingbé kuwa mpatanishi mpya wa mgogoro kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
14.04.2025 Matangazo ya Jioni
Duru ya pili ya mazungumzo ya nyuklia kati ya Marekani na Iran imepangwa kufanyika Roma, Italia// Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Othman Masoud Othman hapo jana alichukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania urais wa Zanzibar kwenye uchaguzi utakaofanyika mwaka huu//Rais wa China Xi Jinping amesema 'hakutokuwa na mshindi' katika vita vya kibiashara.
14.04.2025 Matangazo ya Mchana
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hali ya utulivu imerudi katika kijiji cha Kavumu//Ukraine imeishtumu Moscow kuwalenga raia// Mashirika ya kimataifa ya misaada yamelaani vikali shambulizi lililofanywa na wanamgambo wa RSF kwenye kambi ya wakimbizi ya Zamzam nchini Sudan.
14.04.2025 Matangazo ya Asubuhi
Katika matangazo yetu ya asubuhi hivi leo utasikia makala zetu za Makala yetu Leo, Mtu na Vijana Tugutuke na Jukwaa la manufaa.Sikiliza ya Dunia Yetu Leo Asubuhi kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW Bonn.
13.04.2025 Matangazo ya Mchana
CHADEMA yaenguliwa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba Tanzania ++ Zaidi ya watu 100 wameuwawa katika shambulio la RSF nchini Sudan ++ Israel yashambulia jengo la hospital kuu Ukanda wa Gaza
Matangazo ya Jioni: 12.04.2025
Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz ametangaza kuwa jeshi lake linapanga kuongeza mashambulizi kwenye maeneo mengi ya Ukanda wa Gaza. Iran yasema imefanya mazungumzo yasiyo ya ana kwa ana na Marekani. Mawaziri wa mambo ya nje wa Urusi na Uturuki wajadili juhudi za kusitisha vita Ukraine
Matangazo ya Mchana: 12.04.2025
Marekani na Iran zinaanza mazungumzo kuujadili mpango wa nyuklia wa Iran huko nchini Oman. Wawakilishi wa kundi la Hamas wanaelekea mjini Cairo kufanya mazungumzo na maafisa wa Misri juu ya kusitisha vita katika Ukanda wa Gaza. Urusi yaishambulia Ukraine kwa droni 88
Hamas waelekea Misri kwa mazungumzo ya kusitisha vita Gaza
Ujumbe wa viongozi wa ngazi ya juu wa wanamgambo wa Hamas unaelekea Cairo kwa mazungumzo ya kusitisha vita Gaza.
11.04.2025 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: UN imesema wanawake na Watoto ndio wamekuwa wahanga katika mashambulizi ya hivi karibuni kwenye ardhi ya Palestina / Waasi wa M23 kwa sasa wanajaribu kuwafurusha wapiganaji wa Mai-mai Wazalendo wilayani Kalehe nchini Kongo
11.04.2025 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Wito wa Ujerumani kwa vijana kujiunga na jeshi unaonekana kama ushajiishaji kwa vijana kuhudumu kwenye sekta ya ulinzi / Mapigano ya Khartoum yalienea katika maeneo mengine ya Sudan, likiwemo eneo kubwa la Darfur Magharibi
Ujerumani kusajili wanajeshi wapya
Serikali inaanza na hatua za awali zinazojumuisha kurejesha taratibu za uandikishaji wanajeshi na usimamizi,
Singo: Desturi ya kale kwa jamii za Waswahili
Kusingwa ni utamaduni wa kale wa urembo unaozidi kuibuka tena kwa kishindo katika Pwani ya Kenya.
11.04.2025 - Matangazo ya Asubuhi
Kesi iliyoanzishwa na Sudan dhidi ya Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ ilianza kusikilizwa hapo jana+++Takriban wanawake 129 waliuawa kote nchini Kenya katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2025.
10.04.2025 - Matangazo ya Jioni
Wapalestina wapatao 23 wameuawa katika mashambulizi ya Israel yaliyolilenga jengo moja la ghorofa katika Ukanda wa Gaza+++Rais wa Marekani, Donald Trump amesitisha kwa siku 90 agizo la kuzitoza ushuru baadhi ya bidhaa kutoka kwenye nchi kadhaa duniani.
Utamaduni wa Singo ya kisasa kwa maharusi Mombasa
Ujue utamaduni wa singo, desturi ya kale yenye mizizi ndani ya jamii za waswahili wa Pwani ya Afrika Mashariki, Kwa karne nyingi, kusingwa ilikuwa sehemu muhimu ya maandalizi ya bibi harusi. Fathiya Omar anayo mengi katika makala ya Utamaduni na Sanaa.
Wanaofanya kazi na AI wanavyohatarisha afya ya akili Kenya
Nyuma ya mapinduzi ya teknolojia ya akili mnemba yanayoonekana, kuna kikosi kazi kisichoonekana kinachoundwa na mamilioni ya wafanyakazi wanaoainisha na kutathmini taarifa kwa ajili ya kuilisha teknolojia hiyo.
Ulihimili vipi kishindo cha kuwachwa na mpenzi wako?
Katika kipindi cha vijana mubashara 77 asilimia, Suleiman Mwiru anajadiliana nawe kuhusu masuala ya mahusiano, na anakuuliza je umeshawahi kuacha au kuachwa na mpenzi wako na ulikimudu vipi kishindo hicho?
10.04.2025 - Matangazo ya Mchana
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Tanzania Tundu Lissu yumo mikononi mwa polisi tangu jana jioni +++Rais wa Marekani, Donald Trump amesitisha kwa siku 90 agizo la kuzitoza ushuru baadhi ya bidhaa kutoka kwenye nchi kadhaa duniani.
10.04.2025 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Visa vya dhulma dhidi ya watoto vimeongezeka katika jimbo la Marsabit nchini Kenya / Utafiti mpya umebaini kuwa, wafugaji hasa wa kuku wa kisasa na nguruwe nchini Tanzania, wanatumia dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARV) kuongeza utagaji wa mayai kwa kuku na kuongeza kuzaliana kwa nguruwe
09.04.2025 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Kansela ajaye wa Ujerumani, Friedrich Merz ameapa kuwa serikali mpya ya mseto itaisogeza tena mbele Ujerumani / Utafiti mpya umebaini kuwa, wafugaji hasa wa kuku wa kisasa na nguruwe nchini Tanzania, wanatumia dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARV)
09.04.2025 Matanagazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema Gaza imekuwa kama uwanja wa mauaji kwa sababu Israel inaendelea kuzuia misaada / Matumaini ya Bayern Munich kushinda mataji mawili msimu huu yameingia mashaka baada ya kulazwa 2-1 na Intermilan nyumbani
Waliotaka kuipindua serikali ya Kongo warudishwa nyumbani
Marekani inasema inaunga mkono mazungumzo ya amani ya mashariki mwa Kongo yanayosimamiwa na Qatar.
09.04.2025 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Baada ya Marekani kuyawekea mataifa mbalimbali duniani ushuru mkubwa, China imeapa kulipiza kisasi na sasa inajiandaa na vita vya kiuchumi na Washington / Iran na Marekani zinatarajiwa kufanya mazungumzo siku ya Jumamosi nchini Oman katika juhudi za kuanzisha upya majadiliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran
09.04.2025 Taarifa ya Habari Asubuhi
Mkuu wa Umoja wa Mataifa asema Gaza imegeuka kuwa kiwanja cha mauaji // Kiasi ya watu 79 wakufa baada ya paa la klabu ya usiku kuporomoka Jamhuri ya Dominika // Na Kongo yawarejesha nyumbani Wamarekani watatu waliokuwa wamehukumiwa kifo
08.04.2025 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Watu wasiopungua 25 wameuwawa katika mashambulizi yaliyofanywa na Israel usiku wa kuamkia Jumanne kwenye Ukanda wa Gaza / Mvutano wa kidiplomasia umezuka kati ya mataifa ya Mali,BurkinaFaso na Niger dhidi ya Algeria ambayo hivi karibuni iliiangusha droni ya Mali, ikidai iliingia kwenye anga yake
08.04.2025 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amethibitisha kuwa majeshi yake yako katika mkoa wa Belgorod nchini Urusi / Uganda imetia saini hivi karibuni mkataba wa ujenzi wa mtambo wa kusafisha mafuta na kampuni moja kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu UAE
Ruge: Hatukai kwenye chama kisichowasikiliza wengine
Nchini Tanzania chama kikuu cha upinzani CHADEMA kinaonekana kimekumbwa na mpasuko kuhusu sera yao mpya ya "no reform no election" sehemu fulani ya wanachama inaonekana hawakubaliani na sera hiyo. Zaidi juu ya hilo, Mohammed Khelef amezungumza na aliyekuwa katibu wa masuala ya kijamii na kijinsia, Catherine Ruge.
Philo Tsoungui, mpiga ngoma wa kike Ujerumani
Makala ya Utamaduni na sanaa inamuagazia kwa undani Philo Tsoungui, mmoja wa wapigangoma maarufu zaidi wa kike nchini Ujerumani. Akitokea katika familia mchanganyiko, mama Mjerumani na Baba kutoka Kameruni, Philo, sio tu anapambana kuvuka vizuizi vya mfumo dume, bali pia changamoto za ubaguzi dhidi ya watu weusi.
Jukwaa la Manufaa
Sikiliza maoni yako msikilizaji katika kipindi cha Jukwaa la Manufaa, kilichoandaliwa na kuongozwa na Angela Mdungu. Kipindi hiki kinatoa nafasi kwa msikilizaji kusema kile kilicho moyoni mwake, kinachomkera na kinachomfurahisha. Kuna nafasi pia ya kuwasikia wanajukwaa wengine watakaotoa dukuduku lao kupitia njia ya simu.
08.04.2025 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliwasili mjini Washington na kukutana na rais wa Marekani Donald Trump / Mataifa matatu ya magharibi mwa Afrika yaliyounda kile kijuilikanacho kama Mfungamano wa Sahel yanaonekana kuchukuwa juhudi za makusudi za kujiondowa kwenye utegemezi wa kigeni katika kuendesha chumi zao kwa kuelekea kwa wawekezaji wazalendo
08.04.2025 Taarifa ya Habari Asubuhi
Rais Trump asema Marekani inaanzisha mazungumzo na Iran ya mpango wake wa nyuklia // Ukraine yataka kufikia makubaliano na Marekani kuhusu mkataba wa madini // Na Rais Kagame azilaani nchi zinazoiwekea Rwanda vikwazo kutokana na mzozo wa mashariki ya Kongo
07.04.2025 - Matangazo ya Jioni
Mvua zilizonyesha kwa siku karibia tatu mfululizo mjini Kinshasa, zimesababisha vifo vya watu ishirini na mbili na wengine arobaini na sita wakiwa wamejeruhiwa+++Umoja wa Ulaya umeafikiana kuyapa msukumo zaidi mazungumzo yanayonuwia kuondoa kodi mpya za kulipiza kisasi zilizotangazwa na rais Donald Trump wa Marekani.
Macron: Hamas haipaswi kuitawala Gaza baada ya vita
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kundi la Hamas halipaswi kuitawala Gaza baada ya vita kumalizika.
07.04.2025 - Matangazo ya Mchana
Watu wasiopungua 15 ikiwemo mwandishi habari mmoja wameuawa leo kwenye Ukanda wa Gaza kutokana na mashambulizi ya vikosi vya Israel+++Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, kinaonekana kuingia kwenye mtikisiko mkubwa wa ndani wakati huu viongozi wakuu wa chama hicho wakiendelea kufanya mikutano ya nchi nzima
Idadi ya Wapalestina waliouawa Gaza yafikia 50,700
Idadi ya Wapalestina waliouawa tangu kuanza kwa mzozo wa Gaza mnamo Oktoba 2023 imepindukia 50,000.
07.04.2025 - Matangazo ya Asubuhi
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anajiandaa kuanza ziara yake Ikulu ya White House leo+++Mawaziri wa biashara wa nchi za Umoja wa Ulaya wanakutana Luxembourg
07.04.2025 Taarifa ya Habari Asubuhi
Mataifa 50 yasaka mazungumzo ya kibiashara na Marekani kuhusu ushuru wa Trump // Wabunge wa Uingereza warejea London baada ya kuzuiwa kuingia Israel // Na mvua kubwa yauwa watu 30 katika mji mkuu wa Kongo, Kinshasa
Matangazo ya Jioni: 06.04.2025
Watu 15 wauwawa katika mashambulizi ya anga ya Israel katika Ukanda wa Gaza. Mazungumzo yajayo ya Urusi na Marekani huenda yakafanyika wiki ijayo. Uingereza yalaani Israel kuwashikilia wabunge wake wawili. Ujerumani yaadhimisha miaka 80 ya kukombolewa kwa kambi ya mateso ya Buchenwald
Matangazo ya Mchana: 06.04.2025
Maelfu ya waandamanaji wajitokeza Marekani kupinga sera za Rais Donald Trump. Ujumbe wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakutana na waasi wa M23 Qatar. Iran yakataa mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani kuhusu mpango wake wa nyuklia
Matangazo ya Dunia Yetu Leo Jioni 5 Aprili 2025
Sikiliza Matangazo ya Dunia Yetu Leo Jioni 5 Aprili 2025 moja kwa moja kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW Bonn.
Urusi, Ukraine zaendelea kushambuliana kwa makombora
Ukraine na Urusi zinaendelea kushambuliana, kila upande ukiripoti madhara makubwa kutoka kwa mwenzake.
Matangazo ya Dunia Yetu Leo Mchana 5 Aprili 2025
Sikiliza Matangazo ya Dunia Yetu Leo Mchana 5 Aprili 2025 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW.
04.04.2025 - Matangazo ya Jioni
Watia nia wa nafasi za ubunge ndani ya CHADEMA, nchini Tanzania wameandika waraka maalum kwa chama chao wakishauri kuhusu ajenda ya bila mabadiliko, hakuna uchaguzi, wakisisitiza, chama kishiriki uchaguzi mkuu ujao+++Rais wa Uganda Yoweri Museveni alifika nchi jirani ya Sudan Kusini jana Alhamisi ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu yalipoanza machafuko ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo
Mark Rutte asema Urusi bado ni kitisho kwa NATO
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Mark Rutte amesema Urusi bado ni kitisho kikubwa kwa jumuiya hiyo.
04.04.2025 - Matangazo ya Mchana
Mahakama ya kikatiba ya Korea Kusini imeidhinisha uamuzi wa kumuondosha madaraka Rais Yoon Suk Yeol ambaye alisimamishwa kazi na bunge+++Jeshi la Israel limetangaza kuwa limeanzisha mashambulizi mapya ya ardhini kaskazini mwa Ukanda wa Gaza
Israel yatanua mashambulizi ya ardhini kaskazini mwa Gaza
Jeshi la Israel limeanzisha mashambulizi mapya ya ardhini kaskazini mwa Ukanda wa Gaza mapema Ijumaa.
04.04.2025 - Matangazo ya Asubuhi
Mawaziri wa mambo ya nje wa Jumuiya ya kujihami ya NATO wanakutana mjini Brussels kwa siku mbili kujadiliana njia za kuufanya mfungamnao huo wa kijeshi kuwa "madhubuti+++Tathmini za awali polisi nchini Ujerumani kwa mwaka 2024, zimeonesha kuimarika kwa hali ya usalama.
04.04.2025: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Umoja wa Mataifa umesema mauaji ya wahudumu wa afya huko Gaza yanazusha wasiwasi wa "uhalifu wa kivita". Nchi wanachama wa Jumuiya ya kujihami ya NATO waahidi kuongeza matumizi yao ya ulinzi. Upinzani nchini Burundi watahadharisha kuwa uhaba wa mafuta utaathiri uchaguzi ujao wa Bunge.
Marekani kuanza utekelezaji wa "ushuru wa kulipiza"
Lengo ni kuyalinda maslahi ya kampuni za Marekani na kuinufaisha nchi hiyo chini ya ajenda yake ya "Marekani Kwanza".
03.04.2025 - Matangazo ya Mchana
Tangazo la Rais wa Marekani, Donald Trump, la ushuru mpya kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka mataifa mbalimbali limezua taharuki duniani+++Mashambulizi katika eneo la mashariki ya kati yamechukua sura mpya baada ya watu wasiopungua 50 kuuawa usiku wa kuamkia leo kwenye ukanda wa Gaza.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 13 wa 152
Ukurasa unaofuatia