You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
App
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
29.04.2025 Matangazo ya Mchana
Siku 100 za Trump: Marekani yakabiliwa na mabadiliko makubwa+++Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney ashinda uchaguzi+++Burundi yatoa orodha ya wahanga wa migogoro mbalimbali+++Amnesty: Haki za binadamu duniani ziko hatarini
29.04.2025: Matangazo ya Asubuhi
Shirika la Amnesty lakosoa hatua za rais wa Marekani Donald Trump wakati akitimiza siku 100 madarakani. Chama cha kiliberali cha Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney chashinda uchaguzi wa Bunge. Watu 26 wafariki nchini Nigeria kufuatia mripuko wa bomu la kutegwa ardhini.
28.04.2025 Matangazo ya Jioni
Israel imekataa kushiriki katika kesi iliyoanza mapema leo Jumatatu katika mahakama Mahakama Kuu ya Kimataifa ya Haki ya ICJ kuhusu hatua yake ya kuzuia misaada kuingizwa katika Ukanda wa Gaza// Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ya ECOWAS inaadhimisha miaka hamsini tangu kuasisiwa kwake mnamo Mei 28, 1975 huko Lagos.
28.04.2025 Matangazo ya Mchana
Jeshi la polisi nchini Tanzania limeizingira nyumba ya Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani, CHADEMA, Tundu Lissu na Makamu Mwenyekiti wake upande wa Bara, John Heche, wakati shauri la kesi dhidi ya Jamhuri ya kupinga kusikilizwa kwa kesi ya Lisu ya uchochezi na uhaini kwa njia ya mtandao.
28.04.2025: Matangazo ya Asubuhi
Rais wa Marekani Donald Trump awatolea wito Putin na Zelensky kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano. Watu wanane wauawa nchini Yemen kufuatia mashambulizi ya Marekani dhidi ya waasi wa Kihouthi. Na ripoti ya SIPRI imesema matumizi ya kijeshi duniani kote yameongezeka mwaka jana na kwa kasi zaidi tangu kumalizika kwa Vita Baridi.
27.04.2025 - Matangazo ya Jioni
Sikiliza matangazo ya Dunia Yetu Leo Jioni Aprili 27, 2025 moja kwa moja kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW, Bonn.
27.04.2025 - Matangazo ya mchana
Sikiliza matangazo ya Dunia Yetu Leo Mchana Aprili 27, 2025 moja kwa moja kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW, Bonn.
26.04.2025: Matangazo ya Jioni
Papa Francis azikwa katika Kanisa la Mtakatifu Maria Majjore mjini Roma. Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine asme amekuwa na mazungumzo mazuri na Rais Donald Trump. Mlipuko mkubwa na moto waitikisa bandari nchini Iran na kujeruhi watu zaidi ya 500
26.04.2025: Matangazo ya Mchana
Zaidi ya watu 200,000 wahudhuria mazishi ya kiongozi wa Kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis huko mjini Vatican. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda wakubaliana kuandaa rasimu ya makubaliano ya amani ifikapo Mei 2. Rais Donad Trump akutana na Rais Volodymyr Zelensky wafanya mazungumzo ya ana kwa ana huko Vatican.
25.04.2025 - Matangazo ya Jioni
Moscow na Kiev zimeendelea kushambuliana kwa makombora na droni wakati Mjumbe wa Marekani akikutana hivi leo na rais wa Urusi Vladimir Putin+++Vikosi vya usalama vya India hii leo vimeongeza msako dhidi ya waasi huko Kashmir, baada ya watu 26 kuuawa kikatili mapema wiki hii katika eneo la Pahalgam.
25.04.2025 - Matangazo ya Mchana
Wakazi wa Roma na maelfu yawaumini kutoka duniani kote wanaendelea kumiminika Vatican kwa mara ya mwisho kumuaga Papa Francis+++Wanajeshi wa Pakistan na India wamefyetuliana risasi usiku wa kuamkia leo katika eneo linalozozaniwa la Kashmir.
25.04.2025: Matangazo ya Asubuhi
Maelfu ya watu wameendelea kujitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican++Uongozi wa Palestina unaonekana kuchukua hatua za ndani za kurekebisha muundo wake wa kisiasa.
24.04.2025 Matangazo ya Jioni
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kundi la waasi la M23 jana Jumatano walitoa tamko la pamoja na kutangaza kuwa wamekubaliana kusitisha mapigano// (Ni rasmi sasa serikali ya Tanzania imeweka zuio la kusafirishwa kwa mazao ya kilimo Kwenda nchi za Malawi na Afrika Kusini// Mvutano kati ya mataifa hasimu ya India na Pakistan umeongezeka kwa kasi.
24.04.2025 Matangazo ya Mchana
Ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi umeimarishwa katika viunga vya mahakama ya mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na maeneo mengine jijini hapa wakati kesi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema-Taifa Tundu Lissu ikisikilizwa leo kwa njia ya mtandao//Kenya na China zimeimarisha upya ushirikiano wao wa kidiplomasia.
Waandishi Habari wahatarisha maisha kuripoti mzozo wa Sudan
Hali ya usalama kwa waandishi wa habari wanaoripoti mapigano nchini Sudan inazidi kuwa tete kutokana na vikwazo.
Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Ukraine wagonga mwamba
Mkutano uliolenga kuwakutanisha pamoja mawaziri wa mambo ya kigeni haujafanyika mjini London, Uingereza.
23.04.2025 - Matangazo ya Mchana
Mwili wa Papa Francis ukiwa kwenye jeneza la wazi, umehamishwa hivi leo hadi kwenye Kanisa la Mtakatifu Peter ambapo maelfu ya watu watapata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho//Nchini Tanzania, wakati jeshi la polisi likunukuliwa na vyombo vya habari kukana kumshikilia Makamu mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini humo, CHADEMA, John Heche.
Heche: Kukamatwa kwangu ni jaribio la utekaji nyara
Sudi Mnette amezungumza na mwanasiasa wa upinzani Tanzania, John Heche kuhusu kukamatwa kwake na kuachiwa.
23.04.2025 Matangazo ya Asubuhi
Dunia inaendelea kuomboleza kifo cha kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis// Taifa la Tanzania limeendelea kukabiliwa na changamoto ya ongezeko la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani// Madaktari wa Syria ambao wamekuwa wakihudumu Ujerumani wanagharamika kurejea kwao kutoa huduma bila Malipo ili kuujenga upya mfumo wa afya uliovurugwa na vita.
23.04.2025 Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Mwili wa Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani, Baba Mtakatifu Francis kupelekwa katika kanisa la Mtakatifu Petro. Ukraine yamtaka balozi wa China atoe maelezo kuhusu wapiganaji wa China katika jeshi la Urusi. Na Umoja wa Mataifa wakosoa mauaji ya watu kiasi 26 katika eneo la India la Kashmir.
22.04.2025 - Matangazo ya Jioni
Italia imetangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis+++Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, TEC limeitaka serikali ya Tanzania kuwaachia bila masharti viongozi wa kisiasa waliokamatwa kwa kudai haki ili kulinda amani.
Msaada wa chakula wasitishwa kwa malaki Ethiopia
WFP imesema inasitisha msaada wa matibabu kwa wanawake na watoto 650,000 wenye utapiamlo nchini Ethiopia.
Burkina Faso yadai kutibua njama ya mapinduzi
Utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso umetangaza kuwa idara yake ya ujasusi imezuia njama za mapinduzi.
22.04.2025 - Matangazo ya Mchana
Ulimwengu na waumini wa Kanisa Katoliki kwa ujumla wake wanaendelea kuomboleza kifo cha kiongozi mkuu wa kanisa hilo duniani Papa Francis+++Shirika la ulinzi wa raia Gaza limesema mashambulizi kadhaa ya anga ya Israel yaliyoanza tangu alfajiri ya leo yamewauwa takriban watu 25 katika eneo hilo linaloongozwa na Hamas.
Tetesi za Kabila kuwasili Goma zazusha mivutano Kongo
Taarifa za kuwasili rais wa zamani wa Kongo, Joseph Kabila, mjini Goma wiki iliyopita zimezusha mivutano nchini humo.
Wakatoliki wa Tanzania waomboleza kifo cha Papa Francis
Sikiliza ripoti ya Veronica Natalis kuhusu namna Wakristo Wakatoliki wa Tanzania wanavyoomboleza kifo cha Papa Francis.
22.04.2025 - Matangazo ya Asubuhi
Karibu kusikiliza matangazo ya asubuhi kutoka Idhaa ya Kiswahili, utakayo yasikia ni pamoja na uchambuzi wa ripoti pamoja na makala.
Hamas wahimizwa wakubali mkataba ili misaada iingie Gaza
Mpatanishi mkuu wa Hamas anataka makubaliano kamili ya kukomesha vita na Israel iondoke Gaza.
21.04.2025: Matangazo ya Jioni
Waumini kuanza kuuaga mwili wa Papa Francis. Utasikia pia wasifu wa Kiongozi huyo Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani aliyekuwa mhafidhina aliyependa mabadiliko.
21.04.2025: Matangazo ya Mchana
Yaliyomo: Kifo cha Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis, Vita vya Urusi na Ukraine, mazungumzo kati ya Iran na Marekani kuhusu mpango wa nyuklia na mengine mengi.
Israel yasema mauaji ya maafisa wa afya Gaza lilikuwa kosa
Mafisa wa afya waliuliwa mnamo Machi 23 mwaka 2025 mjini Rafah.
Watu 12 wauawa na shambulizi la Marekani nchini Yemen
Mashambulizi mengine yameripotiwa maeneo ya Marib, Hodeida na Saada.
JD Vance aanza ziara ya siku nne nchini India
Vance naambatana na mke wake na watoo wao watatu katika ziara hiyo India kabla kurejea Washington Alhamisi.
Chad yasaini mkataba wa amani na waasi kuhusu dhahabu
Shughuli zote za uchimbaji madini zimesitishwa kupisha utafiti mpya.
Polisi wa Ujerumani wawasaka washukiwa wa mauaji ya Nauheim
Vikosi maalumu vimetumwa pamoja na magari ya huduma za dharura na helikopta ya polisi
21.04.2025 Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Ukraine yaripoti visa karibu 3,000 vya ukiukaji wa makubaliano ya usitishaji mapigano uliofanywa na Urusi. Israel yasema mauaji ya maafisa wa afya katika Ukanda wa Gaza lilikuwa kosa na itamuajibisha kamanda aliyehusika. Na makamu wa rais wa Marekani JD Vance aanza ziara ya siku nne nchini India.
20.04.2025 Matangazo ya Jioni
Sikiliza Matangazo ya Dunia Yetu Leo Jioni Aprili 20, 2025 moja kwa moja kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW, Bonn.
19.04.2025 Matangazo ya Jioni
Sikiliza Matangazo ya Dunia Yetu Leo Jioni Aprili 19, 2025 moja kwa moja kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW, Bonn.
19.04.2025 Matangazo ya Mchana
Sikiliza Matangazo ya Dunia Yetu Leo Mchana Aprili 19, 2025 moja kwa moja kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW, Bonn.
13.04.2025 Matangazo ya Jioni
Sikiliza Matangazo ya Dunia Yetu Leo Jioni 13 Aprili 2025 moja kwa moja kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW, Bonn.
Matangazo ya Jioni: 18.04.2025
Marekani yatishia kujiondoa kwenye mchakato wa amani katika mzozo wa Ukraine. Mahakama ya ICC yaanzisha uchunguzi dhidi ya Hungary kwa kushindwa kumkamata Netanyahu. Kikosi cha SAMIDRC kwenda Tanzania kupitia Rwanda
Matangazo ya Mchana: 18.04.2025
Watu zaidi ya 20 wauawa katika mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza. Makamu wa Rais wa Marekani kufanya ziara Roma na Vatican. Maafisa wa usalama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wavamia na kufanya upekuzi kwenye mali za rais wa zamani Joseph Kabila
17.04.2025 - Matangazo ya Jioni
Wajumbe wa Marekani wakiongozwa na waziri wa mambo ya nje Marco Rubio wameanza mazungumzo na wenzao wa Umoja wa Ulaya mjini Paris,kuhusu namna ya kupata njia ya kumaliza vita nchini Ukraine+++Wizara ya kilimo Tanzania imesema hatua ya kuzuia wakulima nchini humo kutouza mazao yao nchi za Malawi na Afrika Kusini, si ishara ya mgogoro kati ya mataifa hayo.
Iran: Duru ya pili mazungumzo na Marekani itafanyika Roma
Iran imethibitisha kuwa awamu ya pili ya mazungumzo na Marekani kuhusu mradi wake wa nyuklia itafanyika Roma.
16.04.2025- Matangazo ya Jioni
Chama Kikuu cha Upinzani nchini Tanzania CHADEMA kimesema kitashinikiza uchaguzi huru bila kuhusisha mahakama+++ Israel imesema kuzuwia misaada ya kiutu kuingia Gaza ni shinikizo kwa Hamas kuachilia mateka inayowashikilia+++ M23 yatumia rasilimali za mashariki mwa Kongo kujinufaisha.
16.04.2025 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden, ameukosoa mwenendo wa utawala mpya wa Marekani kuhusu Usalama wa Jamii / Barcelona na Paris Saint Germain wametinga nusu fainali ya Ligi ya Vilabu Bingwa Ulaya licha ya kushindwa katika mechi zao za robo fainali
16.04.2025 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Viongozi kutoka nchi kadhaa duniani walikutana jana Jumanne mjini London, Uingereza, kutathmini njia za kumaliza mzozo nchini Sudan / Mtandao wa biashara haramu ya figo umefichuliwa nchini Kenya ambapo wanufaika hulipa hadi dolla laki mbili kupandikizwa kiungo hicho
15.04.2025 - Matangazo ya Jioni
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema mataifa hayatakiwi kuupa mgongo mzozo mkubwa kabisa wa kibinaadamu unaosambaa nchini Sudan+++Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amerejelea msimamo wake wa kupinga kuundwa kwa dola la Wapalestina.
15.04.2025 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Miaka miwili tangu vilipozuka vita vya Sudan / Umoja wa Afrika umemteua Faure Gnassingbé kuwa mpatanishi mpya wa mgogoro kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Rais wa Togo anamrithi mwenzake wa Angola, João Lourenço
15.04.2025 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Mgogoro kati ya majenerali wawili umeitumbukiza Sudan katika vita ambavyo havionekani kumalizika hivi karibuni / Umoja wa Afrika umemteua Faure Gnassingbé kuwa mpatanishi mpya wa mgogoro kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 12 wa 152
Ukurasa unaofuatia