You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
App
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
26.05.2025 Matangazo ya Jioni
Ujerumani yaikosoa Israel kwa vita vyake huko Gaza+++Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amesema Rais wa Urusi, Vladmir Putin anaona mapendekezo ya mazungumzo ya amani na Ukraine kama ''ishara dhaifu'' +++Rais wa zamani wa Kongo Joseph Kabila awasili Goma
Trump aahirisha ushuru wa 50% kwa Ulaya
Rais Trump ameahirisha utozaji ushuru wa 50% kwa bidhaa zinazotoka Umoja wa Ulaya uliokuwa uanze Juni 1.
26.05.2025 Matangazo ya Mchana
Kundi la waasi wa M23 huko mashariki mwa Kongo limesema kwamba rais wa zamani wa Kongo Joseph Kabila amewasili katika mji wa Goma unaodhibitiwa na waasi hao+++Mashariki ya kati mashambulizi ya Israel yaliyofanyika alfajiri ya leo katika Ukanda wa Gaza, yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 50+++Trump asema Putin anawazimu kwa kuendelea na mashambulizi Ukraine
Taarifa ya Habari za Ulimwengu Asubuhi 26 Mei 2025
Sikiliza Taarifa ya Habari za Ulimwengu Asubuhi ya 26 Mei 2025 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW.
Matangazo ya Dunia Yetu Leo Asubuhi ya 26 Mei 2025
Sikiliza Matangazo ya Dunia Yetu Leo Asubuhi ya 26 Mei 2025 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW.
Mkuu wa shirika la misaada kwa Gaza ajiuzulu
Mkuu wa shirika lenye utata la Kimarekani lililopanga kupeleka misaada kwenye Ukanda wa Gaza amejiuzulu ghafla.
Urusi yauwa watu 13 Ukraine
Watu 13 wameuawa kufuatia mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine, wakati Kiev na Moscow zikibadilishana wafungwa.
Chama cha Maduro kushinda ubunge, ugavana Venezuela
Chama tawala nchini Venezuela kinatazamiwa kupata ushindi mkubwa baada ya upinzani kugomea uchaguzi wa bunge na ugavana.
Wahamiaji 500 waokolewa Ugiriki
Mamlaka nchini Ugiriki zinasema wahamiaji zaidi ya 500 wameokolewa kwenye kisiwa cha kusini mwa nchi hiyo cha Crete.
Matangazo ya Jioni: 25.05.2025
Watu 22 wauwawa kwenye mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza. Urusi na Ukraine zabadilishana wafungwa wakati mashambulizi makali yakiendelea. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Alexander Dobrindt, kuwasilisha kwenye Baraza la Mawaziri mapendekezo ya sheria ya kuzuia familia kuungana tena ambayo itawaathiri baadhi ya wakimbizi
25.05.2025 Matangazo ya Mchana
Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Joseph Kabila, asema Kongo inaendeshwa kidikteta. Mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine yamesababisha vifo vya watu12. Jeshi la Israel limesema limedungua kombora lililorushwa nchini mwake na waasi wa Houthi wa Yemen.
Kabila: Demokrasia lazima irejeshwe Kongo
Rais wa zamani wa Kongo, Joseph Kabila amewataka raia wa nchi hiyo kupambana na kile amekiita "utawala wa udikteta"
Iran na Marekani zarejea tena mezani mazungumzo ya nyuklia
Iran na Marekani zimeanza leo duru ya tano ya mazungumzo juu ya mradi tata wa nyuklia wa Iran mjini Roma, Italia.
Msichana Jasiri: Mwanzilishi wa programu ya afya ya Akili
Adila Nassoro wa Tanzania aliamua kuanzisha programu ya kipekee dhidi ya unyanyapaa wa afya ya akili
23.05.2025 - Matangazo ya Jioni
Iran na Marekani zimeanza leo duru ya tano ya mazungumzo juu ya mradi tata wa nyuklia wa Iran huku utawala mjini Tehran ukitahadharisha kuwa kupatikana makubaliano itakuwa suala gumu+++Serikali ya Sudan imekanusha vikali madai mapya ya Marekani kwamba ilitumia silaha za kemikali dhidi ya wapinzani wake wa vikosi vya RSF.
23.05.2025 - Matangazo ya Mchana
Baraza la Seneti ya Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limeruhusu kuondolewa kwa kinga ya aliyekuwa rais wa taifa hilo, Joseph Kabila+++Mwanahakarati wa pili kati ya wawili wa kigeni waliongia Tanzania kwa kumunga mkono kiongozi wa upinzani anaeshitakiwa kwa uhaini, Agather Atuhaire ameachiwa huru
Ni wapi aliko Joseph Kabila?
Saleh Mwanamilongo amemuuliza hilo Ferdinand Kambere, Naibu Katibu Mkuu wa chama cha Kabila cha PPRD.
23.05.2025 - Matangazo ya Asubuhi
Upinzani nchini Kongo umelalamikia hatua ya serikali ya kutaka kumfungulia mashitaka rais wa zamani Joseph Kabila+++Umoja wa Ulaya umesema utaanza mchakato rasmi wa kupitia upya uhusiano wake wa kibiashara na Israel.
22.05.2025 - Matangazo ya Jioni
Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Musalia Mudavadi athibitisha kuwa mwanaharakati Boniface Mwangi ameachiwa huru na maafisa wa Tanzania+++Ujerumani na Nigeria zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wao katika nyanja za uchumi, nishati na uhamiaji.
22.05.2025 - Matangazo ya Mchana
Marekani, Israel, Umoja wa Ulaya pamoja na nchi kadhaa duniani zimelaani shambulizi la mjini Washington, ambalo wafanyakazi wawili wa ubalozi wa Israel nchini Marekani waliuwawa+++Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wameeleza matumaini mapya kuhusu kupatikana amani ya kudumu kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
22.05.2025 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Rais Donald Trump kwa mara nyingine aliiitumia ofisi yake ya Oval kumshambulia kiongozi mwingine wa ngazi za juu aliyezuru ofisi hiyo. Na mara hii alikuwa ni Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika Kusini / Ukosefu wa ajira kwa vijana nchini Afrika Kusini umefikia viwango vya kutisha
21.05.2025 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Afrika Kusini yatarajia kufikia maelewano na Marekani / Mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza yameendelea licha ya hasira ya kimataifa kuongezeka
21.05.2025 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Rais Vladmir Putin amelitembelea jimbo la Urusi la Kursk kwa mara ya kwanza tangu Moscow ilipodai kuwa imevifurusha vikosi vya Ukraine kutoka eneo hilo mwezi uliopita. Mkoa huo ulikamatwa na Ukraine Agosti 2024 / Bunge la Uganda limepitisha miswaada miwili tata ambayo, kwa mujibu wa wachambuzi, inalenga kudhoofisha vyama vya siasa
Umoja wa Ulaya kupitia upya makubaliano na Israel
Umoja wa Falme za Kiarabu ukisema umefikia makubaliano na Israel kuingiza misaada ya kibinaadamu kwenye Ukanda wa Gaza.
Ipi tofauti ya sonona, msongo wa mawazo na afya ya akili?
Afya ya akili ni hali ya jumla ya ustawi wa akili kihisia, na inahusiana na uwezo wa mtu katika kufikiri, kuhisi na kudhibiti hisia. Hakuna tofauti kubwa sana kati yake msongo wa mawazo na Sonona. Makala ya Afya yako ina mengi zaidi.
21.05.2025 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anaituhumu serikali ya mjini Moscow kwa kuvuta muda / Sekta ya bodaboda nchini Kenya inachangia asilimia 4.4 ya pato la taifa na kuwapa mamilioni mkate wao wa kila siku
20.05.2025 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Viongozi wa Ufaransa, Uingereza na Canada wamekosoa vikali operesheni mpya ya kijeshi ya Israel katika Ukanda wa Gaza na kutishia kuchukua hatua madhubuti ikiwa haitoyasitisha / Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa yuko nchini Marekani katika ziara muhimu itakayomkutanisha ana kwa ana na rais Donald Trump
20.05.2025 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Israel imeishambulia Gaza usiku wa kuamkia Jumanne huku mashambulizi hayo yaliyofanywa katika nyumba ya makaazi na shule yakisababisha vifo vya takriban watu 60 / Mapigano mapya yameibuka kati ya Jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF mjini Omdurman
20.05.2025 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Rais wa Marekani Donald Trump amezungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Urusi Wladimir Putin katika hatua ya kuelekea kufikia makubaliano ya kusitisha vita hivyo / Kushamiri kwa visa vya wanafunzi kujitoa uhai nchini Uganda kumeibua mjadala mzito
20.05.2025 Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Rais wa Marekani Donald Trump asema mazungumzo ya amani kati ya Urusi na Ukraine kuanza mara moja. Uingereza, Canada na Ufaransa zaionya Israel kuhusu mwenendo wake katika Ukanda wa Gaza. Na afisa wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kamil Idris ateuliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Sudan.
19.05.2025 Matangazo ya Jioni
Tanzania - Samia Suluhu Hassan amewaonya wanaharakati ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki kuingia Tanzania na kutoa matamko yanayoweza kuchochea uvunjifu wa amani katika taifa hilo+++DR Congo - Katika wilaya ya Lubero, vituo vya afya vinakabiliwa na uhaba wa madawa+++Uingereza na Umoja wa Ulaya wafikia makubaliano ya kihistoria
19.05.2025 - Matangazo ya Mchana
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini Tanzania, chadema-Tundu Lissu amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo+++Rais Donald Trump wa Marekani anatazamia kuzungumza kwa njia ya simu kwa nyakati tafauti na marais wenzake wa Urusi, Vladimir Putin, na Volodymyr Zelensky wa Ukraine
19.05.2025 - Matangazo ya Asubuhi
Karibu uweze kuyasikiliza matangazo yetu ya asubuhi na miongoni mwa yale tuliyokuandalia asubuhi hii ni pamoja na makala zetu ikiwemo, Makala Yetu Leo, Vijana Tugutuke na Jukwaa la Manufaa.
Zaidi ya Wapalestina 100 wameuawa Ukanda wa Gaza
Zaidi ya Wapalestina 100 wameuawa kwa mashambulizi ya Israel siku ya Jumapili kwenye Ukanda wa Gaza.
Je, ni nani anayenufaika kweli na madini adimu ya Rubaya?
Mashariki mwa Kongo kuna mji wa Rubaya ambao unajulikana kwa utajiri wa madini ya coltan, manganezi na kadhalika.
17.05.2025: Matangazo ya Jioni
Viongozi wa nchi za kiarabu walaani operesheni za Israel huko Gaza. Umoja wa mataifa wapunguza mipango ya misaada katika nchi za Yemen na Somalia. Kimbunga chaua zaidi ya 20 katika majimbo mawili ya kusini mwa Marekani.
17.05.2025: Matangazo ya Mchana
Shambulio la Israel laua watu 10 huko Gaza leo Jumamosi. Urusi yaendeleza mashambulizi yake huko Ukraine licha ya mazungumzo ya amani hapo jana huko Istanbul. tNa leo ni Simba ya Tanzania dhidi ya RS Berkane katika mchezo wa fainali kombe la shirikisho Afrika.
16.05.2025 - Matangazo ya Jioni
Mazungumzo kati ya Urusi na Ukraine yamefanyika leo mjini Istanbul na kumalizika kwa muda usiozidi masaa mawili huku wawakilishi wa Ukraine wakiilaumu Urusi kwa kushinikiza matakwa ambayo hayatekelezeki+++Mpeperusha bendera wa Tanzania, katika fainali ya Kombe la Shirikisho "Simba Sports Club," leo hii ipo katika maandalizi ya mwisho huko Morocco kwa ajili ya mchuano wake wa kesho na RS Berkane
Kutana na msichana anayepiga vita rushwa ya ngono
Joanitha ni mwanafunzi anayesomea masuala ya ustawi wa jamii. Anapinga masuala ya rushwa ya ngono kwa wasichana.
16.05.2025 - Matangazo ya Mchana
Wawakilishi wa Urusi na Ukraine wanatarajiwa kukutana hivi leo mjini Istanbul+++Baraza la Seneti la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limekutana kujadili hatma ya rais wa zamani Joseph Kabila
15.05.2025 - Matangazo ya Jioni
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema hatosafiri kwenda Istanbul kuhudhuria mazungumzo ya amani kati ya nchi yake na Urusi yaliyopangwa kufanyika leo nchini Uturuki+++Nchini Sudan hofu imezidi kutanda kufuatia kundi la wapiganaji wanamgambo la Rapid Support Forces (RSF)
15.05.2025 - Matangazo ya Mchana
Ujumbe wa Urusi umewasili Istanbul kwa ajili ya kuhudhuria mazungumzo ya amani kati yake na Ukraine+++Aliyekuwa Naibu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua amezindua chama chake kwa jina Democratic Citizen Party.
14.05.2025 - Matangazo ya Jioni
Rais wa Marekani Donald Trump amewasili mjini Doha, Qatar leo, na kupokelewa na kiongozi wa taifa hilo, Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani+++Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amesema serikali yake mpya itaweka kipaumbele kikubwa katika usalama, mshikamano, mafanikio na maendeleo kwa wote.
14.05.2025 - Matangazo ya Mchana
Rais wa Marekani Donald Trump amekutana leo mjini Riyadh na Rais wa mpito wa Syria, Ahmed al-Sharaa, katika mkutano wa kihistoria+++kampuni ya ndege ya Rwanda imetangaza kuathiriwa na uamuzi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wa kuweka marufuku ya kuruka katika anga yake.
14.05.2025 - Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Serikali ya kijeshi nchini Mali imetangaza kusitisha shughuli za vyama vyote vya kisiasa katika hilo la Afrika Magharibi+++Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemtolea mwito Rais wa Marekani Donald Trump kusaidia kufanikisha mkutano na kiongozi wa Urusi Vladimir Putin
14.05.2025 - Matangazo ya Asubuhi
Masoko ya hisa yaliimarika huku mzozo wa wiki tano kati ya Marekani na China kuhusu kuongeza ushuru ukipungua+++Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, ZEC imetangaza kupunguza ada kwa wanawake wanaotaka kugombea nafasi za uongozi
Mwangaza wa Ulaya: Juhudi za amani katika mzozo wa Ukraine
Viongozi wa ngazi za juu wa Urusi na Ukraine wanatarajiwa kukutana wiki hii mjini Instanbul nchini Uturuki, kujadili namna ya kuumaliza mzozo wao uliongia mwaka wa tatu na ambao unaendelea kusababisha maafa na uharibifu mkubwa. Ikiwa yatakuwepo, unadhani, kuna ishara zozote za kwamba mara hii mazungumzo hayo kati ya Urusi na Ukraine yatafanikiwa? Ungana na Bakari Ubena.
13.05.2025 - Matangazo ya Jioni
Jeshi la polisi nchini Tanzania limekiri kumkamata Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Bara, Amani Golugwa akiwa safarini kuelekea Ubelgiji+++Israel imeendeleza mashambulizi yake huko Gaza leo Jumanne kwa kukishambulia kituo cha afya na kuwaua watu watatu.
13.05.2025 - Matangazo ya Mchana
Rais wa Marekani Donald Trump ameanza ziara yake ya Mashariki ya kati akiwa amewasili Riyadh, Saudi Arabia leo+++Rais wa Kenya William Ruto amesema wale wote waliotekwa nyara kufuatia maandamano ya vijana dhidi ya serikali nchini humo mwaka jana, wameachiwa.
13.05.2025 - Matangazo ya Asubuhi
Uingereza imekuwa mwenyeji wa mkutano wa mawaziri wa Ulaya uliojadili vita vya Ukraine+++Kundi la kwanza la raia wa Afrika Kusini walio na asili ya walowezi wa kizungu waliopewa hadhi ya ukimbizi wanawasili Marekani kuanza maisha mapya
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 10 wa 152
Ukurasa unaofuatia