You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
App
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
09.09.2025 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Bunge la Ufaransa limeiondoa madarakani serikali ya Waziri Mkuu Francois Bayrou baada ya kukaa madarakani kwa miezi tisa na kumwacha Rais Emmanuel Macron akiharakisha kutafuta mrithi anayefaa katika siku zijazo / Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania limethibitisha kuwashikilia watu 18 wa tuhuma za kufanya mikusanyiko kinyume na sheria
08.09.2025 - Matangazo ya Jioni
Israel imeilaumu Uhispania kwa kuendesha kampeni dhidi ya taifa la Israel na chuki dhidi ya Wayahudi+++Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema, Tundu Lissu, leo amepandishwa kwa mara ya kwanza kwenye Mahakama Kuu nchini humo.
Jukwaa la Manufaa
Ni wakati mwingine mzuri kwa wadau wa Jukwaa la manufaa kutoa na kuyasikia maoni yao yanayojumuisha kero dukuduku, ushauri bila kusahau pongezi kuhusu yale yote yanayojiri kwenye jamii. Nahodha jukwaani kwa wakati huu ni Angela Mdungu, ungana naye kusikiliza.
08.09.2025 - Matangazo ya Mchana
Watu wanne wameuawa na wengine 15 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya risasi mjini Jerusalem+++ Mamlaka zinazohusika na mawasiliano nchini Tanzania zimeufungia mtandao maarufu wa Jamii Afrika maarufu kama Jamii Forums.
08.09.2025 Matangazo ya Asubuhi
Katika matangazo yetu ya asubuhi hivi leo utasikia makala zetu za Mbiu ya Mnyonge, Makala yetu Leo, Mtu na Mazingira, Vijana Tugutuke na Jukwaa la manufaa. Sikiliza ya Dunia Yetu Leo Asubuhi kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW Bonn.
08.09.2025 Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Rais wa Marekani Donald Trump aashiria yuko tayari kuongeza shinikizo dhidi ya Urusi kwa awamu ya pili ya vikwazo. Kundi la Hamas lasema liko tayari kwa mazungumzo kufuatia mapendekezo ya Marekani kuhusu mkataba wa kusitisha mapigano.. Na serikali ya Ufaransa yakabiliwa na hatari ya kuanguka katika kura ya imani.
Israel yaamuru Wapalestina kuondoka Gaza City
Jeshi la Israel limewataka Wapalestina kuondoka kwenye mji wa Gaza City na kuhamia upande wa kusini mwa Gaza.
05.09.2025 - Matangazo ya Jioni
Israel imeshambulia leo jengo moja la ghorofa huku jeshi lake likizidisha mashambulizi katika maandalizi ya kulichukua Jiji la Gaza+++Wapiganaji wa kundi la waasi la M23 wanaoungwa mkono na Rwanda pamoja na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanadaiwa kutenda maovu makubwa dhidi ya raia Mashiriki mwa Kongo.
05.09.2025 - Matangazo ya Mchana
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kwamba vikosi vyovyote vya kigeni vitakavyopelekwa Ukraine kabla ya makubaliano ya amani vitachukuliwa kama adui+++Shirika la Afya duniani WHO limeonya kuwa idadi ya watu walioambukizwa ugonjwa wa Ebola huenda ikaongezeka kufuatia mripuko wa ugonjwa huo hatari nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Jishindie zawadi na DW!
Habari ya mjini ni mitandao,nasi huko tumejipanga sawa sawa.
05.09.2025 - Matangazo ya Asubuhi
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema mataifa 26 washirika wa Ukraine yameahidi kupeleka wanajeshi kama “jeshi la kuhakikisha usalama” kwa taifa hilo+++Baada ya miezi kadhaa ya kuwa katika kambi za wakimbizi wa ndani karibu na Goma na Minova, mamia ya familia sasa wanarudi taratibu kwenye vijiji vyao.
05.09.2025 - Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Miongoni mwa utakayoyasikia ni pamoja na Rais Macron kusema mataifa 26 yako tayari kupeleka jeshi la usalama Ukraine baada ya Vita, Mlipuko mpya wa Ebola nchini DRC wauwa watu 15, Israel yalaani matamshi ya afisa wa Umoja wa Ulaya kuhusu 'mauaji ya halaiki' Gaza, Mapigano nchini Ghana yauwa watu 31, yawahamisha 48,000 na Mike Tyson na Floyd Mayweather kukutana ulingoni 2026
04.09.2025 - Matangazo ya Jioni
Viongozi wa Ulaya wamezungumza na rais wa Marekani Donald Trump baada ya mkutano wao wa kilele na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kuhusu dhamana za usalama kwa Kiev+++Wizara ya usalama wa ndani ya Kenya imekanusha madai kwamba vikosi vya JubaLand vimeingia nchini Kenya kutoka Somalia.
Meza ya Duara: SCO na nafasi yake kwenye ulimwengu wa sasa
Mohammed Khelef anaongoza mjadala juu ya nafasi na nguvu za Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO).
04.09.2025 - Matangazo ya Mchana
Viongozi wa mataifa ya Magharibi ambayo ni washirika wa Ukraine katika mzozo wake na Urusi, wanakutana leo Alhamisi mjini Paris+++Serikali ya Kenya imechukua uamuzi wa kusitisha zoezi ya kufukua miili katika kaunti ya Kilifi ili kutoa nafasi kwa wataalam wa vijinasaba kushughulikia miili 34 iliyopatikana.
Watu 60 wafa katika ajali ya boti nchini Nigeria
Kwenye kadhia hiyo watu wengine kadhaa wameokolewa.
04.09.2025 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Kundi la Hamas Hamas, limesema liko "tayari kwa makubaliano ya kina" na Israel kuhusu kusitisha vita vya Gaza / Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imethibitisha kuwa wanawake watatu kutoka vyama tofauti vya siasa wamechukua fomu za uteuzi kwa kiti cha urais wa Zanzibar
04.09.2025 -Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Miongoni mwa utakayosayisia ni pamoja na Hamas yasema iko tayari kwa makubaliano, Israel yasema ni maneno matupu'.Mashirika ya huduma za jamii yataka misaada zaidi kwa Afghanistan na IAEA: Iran iliongeza akiba yake ya urani iliyoboreshwa hadi karibu na kiwango cha kutengeneza.
03.09.2025 - Matangazo ya Jioni
Waandamanaji wamemiminika kwenye mitaa ya Israel+++Wakati viongozi wa Ulaya wakitarajiwa kukutana hapo kesho mjini Paris kujadili hakikisho la usalama kwa Ukraine+++Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, polisi waliopewa mafunzo na waasi wa AFC/M23 wamerejea katika mji wa Bukavu.
03.09.2025 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Rais wa China Xi Jinping ameonya kuwa dunia inakabiliwa na uamuzi wa kuchagua amani au vita / Utafiti uliofanywa kwenye mataifa mbalimbali umebainisha kuwa binadamu wanaandamwa na jinamizi la kutumia simu za mkononi za kisasa kila wakati
Dunia inakabiliwa na chaguo la amani ama vita - Xi
Putin na Kim wamefanya mazungumzo ya pande mbili, ambayo wote wameyaita yenye tija.
03.09.2025 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Takriban wanajeshi wanne na wanamgambo 10 wameuawa kufuatia mapigano mapya yaliyozuka Sudan Kusini / Wilaya ya Monduli iliyopo mkoani Arusha kaskazini mwa Tanzania, inakumbwa na tatizo la ukame kutokana na kutopata mvua za kutosha
03.09.2025 - Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Sikiliza Taarifa ya Habari za Ulimwengu Asubuhi 03 Septemba 2025 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW Bonn.
02.09.2025 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Zaidi ya watu 1,000 wameangamia nchini Sudan, baada ya maporomoko ya udongo kutokea katika jimbo la Darfur / Kwa mara ya kwanza Rwanda imeidhinisha sheria ya kumruhusu mtu kubeba mimba kwa niaba ya mwingine
02.09.2025 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Rais wa China na mwenzake wa Urusi wameikosoa mitazamo ya nchi za Magharibi wakati wa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya SCO / Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz ameamua kuwa msimu unaofuata wa mapukutiko ndiyo wakati sahihi wa kuzishughulikia changamoto za ndani zinazohitaji suluhisho la haraka
02.09.2025 - Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Sikiliza Taarifa ya Habari za Ulimwengu Asubuhi 02 Septemba 2025 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW Bonn.
01.09.2025 - Matangazo ya Jioni
Mashambulizi ya ardhini na ya anga yanayoendelea kufanywa na jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza+++Hali ya usalama kaunti ya Mandera huko nchini Kenya ni ya wasiwasi baada ya wapiganaji wa Jubaland Forces kutoka Somalia kuingia katika eneo la BP1.
Njia za kukabiliana na hofu ya kujifungua kwa mara ya kwanza
Kwa wanaojifungua kwa mara ya kwanza wakati mwengine wanakuwa na hofu kubwa ya kupitia mchakato mzima wa kujifungua. Wengi wanakuwa na uwoga baaada ya kuwasikia wanawake wengine wakizungumzia mchakato huo wa uzazi. Makala ya Afya Yako inakueleza njia za kukabiliana na hofu hiyo.
Ngoma za Njuga na jinsi zinavyorithishwa kupitia sanaa
Ngoma za Njuga ni aina ya ngoma za asili zinazochezwa kwa kuvaa njuga miguuni au mikononi, zikitamba kwa sauti ya kipekee inayochochea furaha, heshima na mdundo wa kuvutia. Alex mchovu anakupa umuhimu wa ngoma hizo na jinsi ya kuendeleza na kurithisha mila na tamaduni kupitia vipengele vya sanaa.
01.09.2025 - Matangazo ya Mchana
Idadi ya watu ambao wamefariki nchini Afghanistan kufuatia tetemeko baya la ardhi imeongezeka na kufikia zaidi ya 800+++Rais wa China Xi Jinping ameahidi kuwa nchi yake itatoa msaada zaidi kwa ajili ya maendeleo bora ya Jumuiya ya ushirikiano wa Shanghai SCO.
Israel inafanya jinai ya kimbari Gaza - wasomi
Mashambulizi ya Gaza yameripotiwa kuuwa na kujeruhi Wapalestina kadhaa katika kile Israel inachokiita "eneo la kivita".
01.09.2025 - Matangazo ya Asubuhi
Karibu uweze kuyasikiliza matangazo ya asubuhi kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW, na miongoni mwa yale utakayoyasikia ni makala zetu mtu na mazingira, vijana tugutuke na jukwaa la manufaa.
01.09.2025 - Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Sikiliza Taarifa ya Habari za Ulimwengu Asubuhi 01 Septemba 2025 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW Bonn.
31.08.2025 Matangazo ya Jioni
Israel yathibitisha kuuawa kwa msemaji wa kundi la Hamas huko Gaza // India yatangaza kuwa imedhamiria kuimarisha mahusiano na China // Na Indonesia yapunguza posho za wabunge huku rais akijaribu kutuliza maandamano
31.08.2025 Matangazo ya Mchana
Viongozi wa ulimwengu wawasili China kuhudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai // Waziri Mkuu wa serikali ya Houthi nchini Yemen auawa katika shambulizi la Israel // Na Mkuu wa wanamgambo wa RSF Hemedti aapishwa kuwa kiongozi wa serikali sambamba ya Sudan
Makala ya Afrika Wiki Hii
Joto la kisiasa Tanzania linaendelea kupanda kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29. Rais anaetetea kiti chake, Samia Suluhu Hassan, haonekani kuwa na mtihani mkubwa sana kwa kuwa vyama vikuu viwili vya upinzani hadi sasa havina wagombea. Katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo Jeshi bado linapambana na makundi ya wanamgambo na Morocco ndio mabingwa wa mashindano ya Kombe la CHAN-2024
Matangazo ya Jioni 30.08.2025
Ulaya yatoa wito kwa Marekani kufikiria uamuzi wake wa kuwanyima viza wapalestina kuhudhuria mkutano wa UN++++Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limelitaka Baraza la Usalama kuchukua hatua za dharura kuwalinda raia wa Sudan dhidi ya mashambulizi na njaa+++++Watu 13 wamezama baada ya kukimbia mashambulizi ya Kaskazini Magharibi ya Nigeria.
29.08.2025 - Matangazo ya Jioni
Jeshi la Israel limeanza oparesheni kubwa za kijeshi pembezoni mwa mji wa Gaza+++Kesho dunia inaadhimisha siku ya kimataifa ya waathirika wa matukio ya kutoweka na utekaji+++Ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga inaingia mzunguko wa pili wa mechi zake mwishoni mwa wiki hii.
29.08.2025 - Matangazo ya Mchana
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres ameitolea wito Israel kujizuia na kuachana na mpango wake wa kuuteka na kuudhibiti Mji wa Gaza+++Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wanatarajiwa kuongoza kikao cha baraza la mawaziri la pande mbili hii leo nchini Ufaransa.
29.08.2025 - Matangazo ya Asubuhi
Israel bado inaendeleza mashambulizi Gaza huku kukiwa na hofu ya kutokea janga la kiutu // Vikwazo vya kibiashara vilivyowekwa na Rais wa Marekani, Donald Trump, dhidi ya mataifa ya BRICS vimezaa matokeo yasiyotarajiwa // Kamatakamata ya waandishi habari Ethiopia yasababisha hofu miongoni mwa jumuiya ya wanahabari
29.08.2025 - Taarifa ya Habari Asubuhi
Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa Israel kujizuia kuuteka na kuudhibiti Mji wa Gaza // Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema mashambulizi makubwa ya anga ya Urusi mjini Kiev, yanaonyesha kuwa Rais Vladimir Putin anataka kuendeleza vita // Na takribani nchi nne za Afrika zitakosa chakula maalum cha kuokoa maisha ya watoto wenye utapiamlo katika kipindi cha miezi mitatu ijayo
28.08.2025 - Matangazo ya Jioni
Mashambulizi ya Israel dhidi ya Wapalestina yanaendelea kushuhudiwa kwa kasi kubwa Gaza+++Shangwe, nderemo na nyimbo za hamasa zilitawala leo jijini Dar es Salaam wakati Chama cha Mapinduzi (CCM) kikizindua rasmi kampeni zake kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29.
Vijana wanavyoichangamkia teknolojia ya Akili Mnemba Nigeria
Vijana wadogo wakiwemo wanafunzi wa shule za Sekondari nchini Nigeria wanajituma kufanya ubunifu katika teknolojia hasa ya akili mnemba ili kupata ufumbuzi wa masuala mbalimbali kwenye jamii yakiwemo ya elimu, nishati, usalama, kilimo na huduma za afya. Ungana naye Angela Mdungu kwenye makala ya Sema Uvume kusikiliza zaidi.
28.08.2025 - Matangazo ya Mchana
Urusi imefanya mashambulizi makubwa ya droni na makombora yaliyoulenga mji wa Kyiv ambako takriban watu 14 wameuawa+++Rwanda na Msumbiji zimetia saini makubaliano ya "amani na usalama" wakati wa ziara ya rais Daniel Chapo mjini Kigali nchini Rwanda.
Matangazo ya Asubuhi 28.08.2025
Jeshi la Israel limeendeleza operesheni zake za kijeshi katika Mji wa Gaza // Wanasiasa wa Iraq wanalenga kufanya mageuzi ya sheria inayowahusu wanamgambo walio nje ya udhibiti wa serikali // Rais wa Marekani, Donald Trump amedai kwamba amefanikiwa kuvimaliza vita vya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
Taarifa ya Habari Asubuhi 28.08.2025
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa tamko la pamoja kuhusu jaa katika Ukanda wa Gaza // Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky ametangaza kuwa maafisa wa Marekani na Ukraine wanatarajia kukutana kesho Ijumaa // Mapigano kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na wapiganaji wanaojiita Wazalendo yamesababisha vifo vya watu watano karibu na mpaka wa Burundi.
27.08.2025 Matangazo ya Jioni
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) leo, Jumatano, imefanya zoezi la uteuzi wa wagombea wa nafasi ya Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania// Kenya inaadhimisha miaka 15 ya katiba mpya//Hatima ya wapi mwili wa Rais wa zamani wa Zambia, Edgar Lungu, utazikwa bado haijulikani.
27.08.2025 Matangazo ya Mchana
Tume huru ya uchaguzi nchini Tanzania (INEC) imekiandikia chama cha upinzani cha ACT Wazalendo kuwa hakitaweza kumteua mgombea wa urais kupitia chama hicho, Luhaga Mpina// Serikali ya Kenya imeanzisha rasmi jopo la wataalamu litakalosimamia fidia kwa waathiriwa wa maandamano na ghasia za umma yaliyoshuhudiwa nchini tangu mwaka 2017
27.08.2025 Matangazo ya Asubuhi
Nchi za Magharibi ambazo ni washirika wakuu wa Kiev, zimekuwa zikijadili uwezekano wa kupelekwa kwa wanajeshi nchini Ukraine// Uhaba wa maji unaotokana na ongezeko la viwango vya joto na ukame duniani huenda ukavuruga mifumo ya uchumi wa mataifa na kusababisha ukosefu wa chakula, uhamiaji na misukosuko ya kisiasa.
27.08.2025 Taarifa ya Habari Asubuhi
Jeshi la Israel lasema shambulizi la hospitali ya Nasser liliilenga kamera ya Hamas // Mazungumzo ya nyuklia yaliyofanyika Geneva yakamilika bila mafanikio // Na Morocco kuvaana na Madagascar katika fainali ya CHAN jijini Nairobi
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 1 wa 152
Ukurasa unaofuatia