Guterres ataka uchunguzi huru wa mauaji ya Rafah
2 Juni 2025Matangazo
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, AntonioGuterres,ametowa mwito wa kufanyika uchunguzi huru kuhusu mauaji ya Wapalestina yaliyotokea karibu na kituo cha kugawa msaada kinachosimamiwa na Marekani katika Ukanda wa Gaza.
Timu ya Gaza ya ulinzi wa raia ilisema wanajeshi wa Israel ndio waliofyetuwa risasi na kuwauwa takriban watu 31 na kuwajeruhi 176 katika mji wa Kusini waRafah.
Hata hivyo jeshi la Israel limekanusha kuhusika na shambulio hilo la Jumapili.Katika taarifa yake,Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa,Antonio Gutteres amesema haiwezi kukubalika kuwaona Wapalestina wakihatarisha maisha yao kwaajili ya chakula.