ANKARA:Ziara ya Kansella wa Ujerumani nchini Uturuki
4 Mei 2005Kansella wa Ujerumani Gerhard Schroeder amewasili Uturuki kwa ziara yake ambapo anatarajiwa kumuhimiza waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kuongeza mara dufu jitihada za mageuzi kabla ya kufanyika mazungumzo juu ya kujiunga kwa Uturuki katika Umoja wa Ulaya hapo mwezi Oktoba.
Katika mahojiano yaliyochapishwa na gazeti moja kabla ya Kansella kuwasili Ankara alisema Uturuki lazima iimarishe rekodi yake juu ya haki za binadamu.
Lakini wapinzani nchini Ujerumani wanasema Uturuki haijawa tayari kujiunga na Umoja wa Ulaya kwa sababu haijafanya juhudi zozote za mageuzi.
Mapema hapo jana Kansella Schroeder aliitembelea Bosnia ambako alitaka mazungumzo juu ya uhusiano maalum na kukutana kwa muda mfupi na jamaa za wahasiriwa wa mauaji makubwa ya halaiki yaliyofanyika nchini Bosnia.