ANKARA.waziri mkuu asema Uturuki itaendelea kufanya mageuzi
30 Novemba 2006Matangazo
Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema nchi yake itaendelea kufanya mageuzi licha ya pendekezo la kamisheni ya umoja wa ulaya la kusimamisha kwa muda mazungumzo kuhusu nchi yake kujiunga na umoja huo.
Pendekezo hilo lilifikiwa baada ya Uturuki kushindwa kufungua bandari zake kwa Cyprus ambayo ni mwanachama wa umoja wa ulaya.
Mawaziri wa mamabo ya nje wa nchi za umoja wa ulaya watakutana Desemba 11 kutoa uamuzi iwapo watazingatia pendekezo hilo.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema amefurahishwa na hatua ya kuishinikiza Uturuki.