ANKARA: Waziri mkuu wa Iraq ziarani Uturuki
20 Mei 2005Matangazo
Waziri mkuu wa Iraq Ibrahim Al Jafaari amewasili nchini Uturuki kwa mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo juu ya masuala yanayohusu usalama na biashara.
Ziara hii maalum ya kiserikali ndio ya kwanza kufanywa na waziri mkuu Jafaari tangu kuundwa kwa serikali mpya ya Iraq.
Kiongozi huyo wa Iraq amekutana na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kabla ya kufanya mkutano wa pamoja na waandishi habari.
Katika ziara hiyo waziri mkuu wa Iraq ameandamana na ujumbe wa mkubwa wa mawaziri wake ikiwa ni pamoja na mawaziri wa mafuta ,Fedha,Biashara,Nishati na viwanda.
Suala linalotarajiwa kuzungumziwa kwenye mkutano huo ni juu ya uamuzi wa waasi wakikurdi wenye asili ya kituruki waliojificha kwenye milima ya Kaskazini mwa Iraq.