Ankara. Waziri mkuu mpya wa Iraq ziarani Uturuki.
21 Mei 2005Waziri mkuu wa Iraq Ibrahim Jaafari amekuwa na mazungumzo nchini Uturuki jana katika ziara yake ya kwanza rasmi tangu kuundwa kwa serikali mpya. Maafisa wa Uturuki wamesema kuwa Bwana Jaafari na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wamefikia makubaliano ya ushirikiano wa masuala ya usalama na upatikanaji zaidi wa nishati.
Mauzo ya umeme yataongezeka zaidi ya mara tatu na kuongeza kiasi cha umeme nchini Iraq na kusaidia kupunguza upungufu uliopo hivi sasa wa umeme nchini humo.
Uturuki pia imekubali kusaidia katika mafunzo ya jeshi na jeshi la usalama. Bwana Erdogan pia amempa Bwana Jaafari orodha ya majina ya watu, wanaosadikiwa kuwa ni wabunge wa Kikurd, ambao Uturuki inawahitaji warejeshwe nchini humo kwa madai ya kufanya mashambulizi.