ANKARA. Uturuki yasema bila uanachama kamili haitakubali vinginevyo
2 Septemba 2005Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki amesema, kwamba nchi yake huenda ikajitoa katika juhudi zake za kutaka kuwa mwanachama wa umoja wa ulaya iwapo nchi yake haitapewa nafasi ya kuwa mwanachama kamili wa umoja huo.
Gazeti la maswala ya kibiashara mjini Ankara limemnukuu bwana Abdullah Gul waziri wa mambo ya nje wa Uturuki, kwamba Uturuki itajitoa katika mazungumzo hayo iwapo hoja ya baadhi ya wanachama wa umoja wa ulaya ambao wanapendelea Uturuki ipewe uanachama maalum badala ya uanachama kamili itapitishwa katika mazungumzo yanayotarajiwa kuanza tarehe 3 Octoba.
Kwengineko waziri mkuu wa Uturuki Recep Erdogan nae amesema nchi yake hatikubali kuvurutwa juu ya swala la nchi hiyo kuitambua Cyprus.
Uingereza kama mwenyekiti wa tume ya umoja wa ulaya inaitaka Uturuki iitambue Cyprus lakini kwa upande wake Uturuki inataka ufumbuzi upatikanu juu ya Cyprus.