ANKARA: Mwanajeshi mmoja na waasi wawili wauwawa nchini Uturuki
21 Julai 2005Matangazo
Mwanajeshi mmoja na waasi wawili wa kikurdi wameaga dunia katika mapigano makali kusini mashariki mwa Uturuki. Mapigano hayo yaliyotokea katika mkoa wa Van, yalizuka wakati wanamgambo wa chama kilichopigwa marufuku cha Kurdistan Worker´s, walipowafyatulia risasi wanajeshi.
Mapigano hayo yamefanyika wakati Uturuki inapokaribia kuifanyika marekebisho sheria yake ya kupambana na ugaidi ili kuwadhibiti waasi wa kikurdi, ambao wameongeza mashambulio yao dhidi ya serikali. Waziri wa sheria Cemil Cicek amesema marekebisho ya sheria hiyo yanakaribia kukamilika.