ANKARA: Miripuko ya bomu imeua watu 27
28 Agosti 2006Matangazo
Si chini ya watu 27 wamejeruhiwa katika mfululizo wa miripuko ya bomu nchini Uturuki.Waingereza 10 na Waturuki 11 waliokuwa wakisafiri kwa basi ni miongoni mwa wale waliojeruhiwa katika mji wa utalii Marmaris.Maafisa wa Kituruki wamesema,bomu moja liliripuka chini ya kiti ndani ya basi hilo.Watu wengine 6 walijeruhiwa na mripuko uliotokea katika mji wa biashara wa Uturuki, Istanbul.Hakuna ye yote aliedai kuhusika na mashambulio hayo.Polisi lakini imewalaumu wanamgambo wa Kikurd kwa mashambulio hayo.