Ankara. Lori lalipuka moto nchini Uturuki na kuuwa watu wawili.
6 Agosti 2005Matangazo
Watu wawili wameuwawa na wengine 20 wamejeruhiwa leo wakati lori la kubebea mafuta lilipolipuka katika barabara moja katika jimbo la Gaziantep nchini Uturuki.
Sababu za mlipuko huo bado hazijulikani amesema gavana wa jimbo hilo Lutfullah Bilgin, wakati akihojiwa na shirika la habari la nchi hiyo Anatolia.
Gavana huyo ameongeza kuwa watu wote isipokuwa mmoja kati ya wale waliojeruhiwa ndio yuko katika hali nzuri.
Magari kadha yaliyokuwa yakisafiri mbele ama nyuma ya lori hilo yameungua moto.