Ankara: Fischer ziarani Uturuki
24 Novemba 2003Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani, Joschka Fischer, amewasili Ankara, Uturuki leo kwa lengo la kuonyesha mshikamano baada ya nchi hiyo kukabiliwa na mashambulio ya kigaidi mjini Istanbul. Fischer atakutana na Waziri mwenzake wa Uturuki, Abdullah Gül na kuzungumza pamoja na Wandishi wa Habari kabla ya kurudi nyumbani baadaye leo. Mazungumzo yao yatahusu pia uanachama wa Uturuki katika Umoja wa Ulaya. Bw. Fischer atakutana ubalozini na Wanadiplomasia wa Kijerumani kutoka Ankara, Istanbul na Izmir na kutathmini hatua za ulinzi baada ya masinagogi mawili, ubalozi mdogo wa Uingereza na Benki moja ya Uingereza kushambuliwa mjini Istanbul. Mashambulio hayo ya Novemba 15 na 20 yamesababisha watu 53 kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.