Angola yajiondoa kwenye upatanishi wa mzozo wa Kongo
24 Machi 2025Matangazo
Angola imetangaza hivi leo kuwa kujiondoa katika nafasi ya upatanishi kwenye mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati ya jeshi la serikali na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda.
Umoja wa Afrika sasa utalazimika kuiteua nchi nyingine ili kuchukua nafasi hiyo ya kuendeleza juhudi za mazungumzo katika dhamira ya kuvimaliza vita vitavyotishia amani kwenye eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini.
Angola iliyoteuliwa na Umoja wa Afrika katika nafasi hiyo ya upatanishi, imesema rais wa nchi hiyo João Lourenço amefanya kila aliwezalo na bila mafanikio kuzisulihisha pande hasimu katika mzozo huo wa mashariki mwa Kongo ambao umesababisha maafa makubwa.