Angela Merkel ni mwanasiasa mashuhuri nchini Ujerumani, aliyekuwa Kansela wa Ujerumani kati ya mwaka 2005 hadi 2021. Alikuwa pia mwenyekiti wa chama cha Christian Democratic Union CDU, ndani ya muda huo.