ANBAR-IRAQ,Gavana wa mkoa wa Anbar atekwa nyara siku chache baada ya kukamata wadhifa huo.
11 Mei 2005Gavana wa mkoa wa Anbar nchini Iraq amekamatwa mateka.Gavana huyo Nawaf Raja Farhan al-Mahalawi,alikamatwa katika barabara kuu karibu na mpaka wa Syria,siku chahe tu baada ya kukabidhiwa wadhifa wa Ugavana wa mkoa huo.
Watu waliomteka inasemekana wametoa madai kutaka majeshi ya Marekani yasitishe mashambulizi yake makali dhidi ya waasi katika mkoa wa Anbar.
Nao maofisa wa jeshi la Marekani wamesema kiasi cha wanamgambo 100 wamekwishauawa hadi sasa katika operesheni iliyoanza siku chache zilizopita huko Anbar.
Katika hatua nyingine hadi sasa hakuna taarifa yoyote iliyokwishatolewa kuhusu hali ya mateka raia wa Australia,Douglas Wood anayeshikiliwa mateka nchini Iraq.
Muda uliowekwa na watekaji nyara kutimiziwa madai yao ulikwishamalizika saa kadha zilizopita.Nao maofisa wa serikali ya Japan bado wamo mbioni kutafuta maelezo zaidi kuhusiana na hali ya mateka wa Kijapani ambaye ameripotiwa kujeruhiwa wakati alipokamatwa.