MigogoroNigeria
Amnesty: Watu 30 wauawa na wapiganaji wenye silaha Nigeria
10 Mei 2025Matangazo
Hayo yameelezwa na shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International ambalo limeongeza kuwa zaidi ya magari 20 pamoja na malori kadhaa yalichomwa moto wakati wa shambulio la Alhamisi katika eneo la Okigwe-Owerri kwenye barabara kuu ya jimbo la Imo. Polisi wamethibitisha tukio hilo lakini lakini hawakutoa taarifa yoyote kuhusu vifo.
Hakuna kundi lolote lililodai kuhusuka na shambulio hilo, lakini polisi wanawashuku wapiganaji wa kundi lililopigwa marufuku la Watu wa Asili ya Biafra ambao kwa miongo kadhaa sasa wamekuwa wakidai haki ya kujitenga na taifa la Nigeria.