Amnesty: Haki za binadamu duniani ziko hatarini
29 Aprili 2025Ripoti hiyo inaangazia chuki za kidini na za kijinsia, na mashambulizi ya kibaguzi yanayoilenga mifumo ya kimataifa ya haki za binadamu iliyojengwa baada ya kushindwa kwa utawala wa kinazi na kumalizika kwa vita vikuu vya pili.
Mashirika ya haki za binadamu yakosoa kamatakamata Niger
Kwa mujibu wa shirika la Amnesty International lenye makao yake makuu nchini Uingereza, ulimwengu uko katika "wakati mgumu" linapohusika suala la haki za binadamu duniani kote.
Nguvu kubwa inatumika kuhujumu maadili ya haki za binadamu
Agnes Callamard, Katibu Mkuu wa Kimataifa wa shirika hilo, amebainisha kuwa nguvu isiyo na kifani inatumika kuhujumu maadili ya haki za binadamu, ikitaka kuharibu mfumo wa kimataifa ulioundwa baada ya maafa ya Vita vya Pili vya Dunia.
Amnesty International imetathmini hali ya haki za binadamu katika jumla ya nchi 150 kila mwaka.
Masuala yanayowaathiri watu
Kuhusu matukio ya kuongezeka kwa vurugu dhidi ya raia na makundi ya walio wachache, ripoti ya kila mwaka ya Amnesty inabainisha mienendo mitatu inayojitokeza; Kwanza, raia wanakabiliwa na shinikizo kubwa katika maeneo ya vita kama Sudan, Gaza, Ukraine na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Makundi ya kutetea haki za binaadamu yaitaka Tunisia kuimarisha uhuru wa kujieleza
Julia Duchrow (Dakh-rov), katibu mkuu wa Amnesty International tawi la Ujerumani, ameiambia DW kuwa sheria zinazopaswa kutumika katika migogoro, na kanuni ambazo jumuiya ya kimataifa imejiwekea, zinapuuzwa zaidi na zaidi,"
Pili, jamii za walio wachache wako hatarini katika nchi nyingi, hasa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, wakimbizi na walio kwenye upinzani.
Na, tatu, mataifa yamezidi kushindwa kuchukua hatua kukabiliana na mgogoro huu wa haki za binadamu. Hii inajidhihirisha hasa kwa mataifa ambayo hapo awali yalijitolea kwa haki za binadamu kwa wote, kama vile Marekani.
Marekani yashtumiwa kwa kuchochea mgogoro
Julia Duchrow ameituhumu serikali ya Marekani kuchochea mgogoro huu wa haki za binadamu, na kuweka mabilioni ya watu duniani kote hatarini".
Aliongeza kuwa vikwazo dhidi ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu na kujiondoa kwaMarekani katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, ni sawa na kuvunja mhimili wa sheria za kimataifa.
Israel yashtumiwa kwa madai ya mauaji ya kimbari
Shirika hilo lisilo la serikali la haki za binadamu linaishutumu Israel kwa kufanya lilichokiita "mauaji ya kimbari" dhidi ya Wapalestina.
Ripoti hiyo ilisema, "Nchi zilitazama kana kwamba hazina nguvu, wakati Israeli ilipoua maelfu kwa maelfu ya Wapalestina, ikiangamiza familia zote za vizazi vingi, ikiharibu nyumba, riziki, hospitali na shule".
Israel yakanusha shtuma dhidi yake
Serikali ya Israel hata hivyo inakanusha shutuma hizo, na baadhi ya wataalamu wa sheria za kimataifa pia wametilia shaka matumizi ya neno hilo. Mtaalamu wa Ujerumani na Uingereza Stefan Talmon anasema maelezo ya kisheria ya ripoti ya Amnesty yana dosari.
Mgogoro wa Sudan watajwa kuwa janga la kibinadamu
Mgogoro nchini Sudan pia unaangaziwa katika ripoti ya mwaka huu kama janga la kibinadamu. Nchi hiyo imekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miaka miwili.
"Watu wengi wamekimbia makazi yao nchini Sudan kuliko mahali pengine popote duniani”, inasema Amnesty International.
Amnesty Int: Sera za Trump zimerudisha nyuma harakati za haki za binadamu
Utawala uliopita wa Marekani ulilikosoa kundi la waasi lililohusika kwa "mauaji ya kimbari," lakini Amnesty International inaitaja badala yake kuwa ni vurugu kwa pande zote mbili na kutoa wito wa kuwekewa vikwazo vya silaha.
Ujerumani yashtumiwa kuhusiana na sera za wakimbizi
Ujerumani imekabiliwa na ukosoaji kwa mfululizo wa mabadiliko yanayohusiana na haki za wahamiaji na wakimbizi.
HususanAmnesty International inaelezea kuanza tena kuwarudisha nyumbani kwao raia wa Afghanistan na Syria, kusimamishwa kwa maombi ya hifadhi kwa Wasyria, na kurejeshwa kwa ukaguzi wa mpaka katika nchi za ukanda wa Schengen bila "sababu za kuridhisha."