Amman . Wauaji walitokea Iraq, asema mfalme Abdullah 11.
13 Novemba 2005Matangazo
Mfalme Abdullah wa 11 wa Jordan amesema kuwa watu waliofanya shambulio la bomu dhidi ya hoteli tatu siku ya Jumatano mjini Amman walikuwa wanatoka Iraq.
Maafisa wa usalama wa Jordan pia wanasema kuwa mke wa mmoja wa washambuliaji hao waliojitoa mhanga amekamatwa.
Mwanamke huyo anatuhumiwa kuwa huenda ni wa nne kati ya watu watatu ambao walijitoa mhanga katika mashambulio hayo.
Kiasi cha watu 57 wameuwawa wakati watu watatu walipojitoa mhanga katika shambulio la bomu katika hoteli tatu za kifahari katikati ya mji wa Amman .